JE NI LAZIMA NIA RAMADHANI KILA SIKU AU INATOSHA KUTIA NIA SIKU MOJA TU MWANZO WA RAMADHANI
هل تجب النيّة لكل ليلة في رمضان أم تكفي نيّة واحدة؟ - الشيخ صالح الفوزان
Muulizaji anauliza: je nia ya funga ya ramadhani inafungamana kila siku katika masiku ya ramadhani au inatosha nia moja kwa usiku wa kwanza katika mwezi wa ramadhani?
Jawabu kutoka kwa Al-allaamah swaaleh Al-fawzan (Allah amhifadhi)
Ndio ni lazima nia ipatikane kila siku kwani hakika ya funga ya kila siku ni ibada yenye kujitegemea, mtume (swallah llahu alayhi wasallam) amesema: hakika ya mtendo ni kwa nia na kwa hakika kila mtu kwa kile alicho kinuia. na anasema mtume (swallah llahu alayhi wasallam): hakuna funga kwa yule ambae hakulala na nia, hukmu hii ni kwa siku zote, sawa sawa ilikua funga ya faradhi au funga ya sunna,
Basi atanuia kila siku nia yenye kujitegemea, pindi akismama mwisho wa usiku na akala daku basi hii ni dalili ya nia, na wala haifai kusema nimenuia kufunga, nia maana yake hakika ya binaadam anaamka anakula na anakunywa kwaajili ya kufunga hii ndio nia, naam."
Skiliza kwa faida clip ina dkk 1 na sekunde 12 tu, ingia katika ya YouTube kuskiliza hii kisha subscribe channel yetu ili kupata faida mpya za shekh fawzan kila zikitoka.
••┈•✿•┈•••••°••○••°••••┈•✿•┈••
Abou huda'a Al-jaziiriyyi حفظه الله
Jiunge na group moja tu la WhatsApp ili kuacha nafasi kwa wengine
FAWA'AID SHEKH FAUZAN