Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,045
- 4,325
Tanzania ni nchi moja nzuri sana tena saaana, ila haijabahatika kuwa na mwendelezo wa viongozi wazuri wenye uchungu na nchi
Ukweli napenda nisisitize, 17 march 2023, TANZANIA ilipoteza kiongozi mwenye TANZANIA yake hata kama hatutakubaliana wote.
Kwa mara ya kwanza nilisikia na kuona maajabu makubwa yakitendeka katika nchi yangu hii ya Tanzania.
Inahitaji uthubutu wa hali ya juu mno na nidhamu ya kutosha kufanya yale JPM alifanya kwa huo muda mfupi!
Jiji la Dar, lilibadirika na kuwa la tofauti kabisa, Mwanza nayo ilipendeza saana, kukazaliwa na jiji jipya la Dodoma ambapo yaliyofanyika Dodoma kila mmoja hahitaji kusimliwa! Stend za maana kila mkoa na wilaya, vituo vya afya na hospital za rufaa zilijengwa na zingine kuanzishwa,
Kubwa zaidi, suala la umeme JKNHP ndio mwisho wa matatizo yetu, SGR nayo, doh! Mengine mtasema nyie,
Tanzania, Tunahitaji kina JPM watano tu, ili kuwa na uchumi mzuri kama Singapore!
Nirudi kwenye topic, Raisi wetu Mama Samia, tupige magoti mpaka lini kuombea uongozi wako?
Mbona ambao Mungu anakuonyesha hawafai kuwa kwenye safu yako ya kukusaidia unawatoa na kisha kuwapangia pahala pengine na hawaachi kuharibu?
Mh mtukufu Rais wetu Msikivu Samia, huwenda ungefanikiwa sana ikiwa ungeliondoa uswahiba kwenye kazi
Baba mwenye kujali, hufikiri sana badaye yake na familia yake, katika kuhangaika kwake, yuko tayari kumtenga hata mwanaye inapotokea anafuja mali, huyo ndo baba bora!
Katika ujenzi wa Taifa letu, kiongozi mzuri, hahitaji kuonea aibu wanaoharibu na kufuja fedha za walipa kodi, walipa kodi ndio hao wanaokula mlo mmoja! Mh Rais, nina uhakika, una watu zaidi ya Milioni 20+ ambao ni wasomi wazuri na wenye kukufaaa
Usikae na hao hao kina kipara ambao walishakuwa kama kuku aliyegoma, kutotoa kwake ni hadi umemchoma mdomo, fumbua macho mheshimiwa, hao unaowabadirisha badirisha, hawatabadirika kamwe, tupa kule na kuweka wengine!
Hata kama wakishindikana wote hapo bungeni, kuna walio mtaani, pangua na kupanga upya!
Na ikiwa itakuwa hivi hivi, basi lawama zote ni juu yako!