Sisi Wananchi halali wa Tanzania, tunatuma Ujumbe na Maombi yetu kwako Rais Samia

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
1,824
4,073
Kwanza nianze ujumbe wangu kwa kumtanguliza mwenyezi Mungu alietupa uhai, afya, nguvu na akili ya kusimamia mfumo wa maisha yetu ya kila siku.

Pili nitumie tena nafasi hii kuwasalimu watanzania wenzangu ukiwepo na wewe raisi wetu na Mtanzania namba moja, "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?" (Kazi iendelee)

Tatu nikupongeze kwa kupata ugeni mzito week iliyopita, ugeni ambao nina hakika utaenda kuinufaisha nchi yetu hapo baadae kutokana na ukaribu uliyopo kati ya nchi yetu na ile ya mgeni wetu mama Kamala Harris.

Mheshimiwa raisi, nikiachana na hayo mambo matatu niliyoyatanguliza hapo juu, naomba sasa ruhusa yako ya kuendelea na kile kilichonifanya niandike ujumbe huu kwako.

Mheshimiwa raisi week iliyopita, yani kabla ya ujio wa mgeni wetu mheshimiwa mama Kamala Harris , kulikuwa na upokeaji wa ripoti mbili. Yani ya takukuru na ile iliyohusu ukaguzi wa mali za umma katika ofisi za serikali.
Kitendo kilichosababisha wananchi wengi tufuatilie ripoti ile ili kujua kile kilichojiri katika ripoti ile, lakin pia kufahamu ni hatua gani ambayo serikali itaenda kuchukua kutokana na kile kilichoandikwa katika ripoti ile.

Kweli ripoti ilisomwa, na madudu mengi tuliyasikia kupitia kwako mwenyewe kama kiongozi wa serikali na raisi wa nchi yetu.

Wengi tuliona ni jinsi gani ulivyochukizwa, na kuumizwa na ubadhilifu ule wa mali zetu za umma uliofanywa na watu wachache wanaotumia mianya yenye udhaifu serikalini kuiba, na kulitia hasara taifa. Huku wakijua kwamba endapo itafahamika kwamba wameiba, basi hakuna hatua yoyote ya maana itakayochukuliwa dhidi yao.

Hili la kujiamini kuwa hakuna lolote litakalofanywa dhidi yao linakuja katika akili zao, kutokana na uzoefu waliokuwa nao huko nyuma. Kwamba wizi mwingi ulikuwa ukifanyika na mwisho wa siku wezi waliishia kuhamishwa tu ofisi, au kufukuzwa tu kazi bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kushitakiwa kwa wizi wao unaolitia hasara taifa, na kuifedhehesha serikali iliyopo madarakani kwa kushindwa kufanya lolote juu yao.

Fikiria kama mwizi wa ndala anafikishwa mahakamani, na kufungwa kwa wizi huo ili iwe fundisho kwa wengine kuiba ndala, sasa kwanini hawa wanaotuibia mabilioni yetu ya kodi kila siku inashindikana kuwaadabisha ili liwe funzo pia kwa watumishi wengine wa serikali?

Wengi tunakumbuka wakati ulipoanza kukalia kiti cha uraisi, ulitoa onyo kwa mafisadi na wabadhilifu wa mali za umma.

Uliwataka wezi hao wasijaribu kupima kina cha maji kwa kutumia ugoko, na pia wale ambao wangekuzingua na wewe ungewazingua zaidi.

Sasa kulikoni mheshimiwa raisi mpaka leo ni miaka miwili sasa mafisadi washapima kina na kuvuka kabisa mto bila kuzama au kushikwa miguu!

Wengine washazingua bila na wao pia kuzinguliwa!

Je zile kauli zako ulizotoa kipindi kile zilikuwa ni za kisiasa tu au za utekelezaje?

Kama ni za utekelezaji, je ni lipi ambalo ushatekeleza kwa wabadhilifu hao wa kodi zetu?

Mheshimiwa raisi, mimi mwananchi wa kawaida ambae nina watu nyuma yangu walionituma nilete ujumbe huu kwako kupitia jukwaa letu hili pendwa, ambalo na wewe huwa unapitia pitia mara moja moja kuchungulia na kusoma maoni ya wananchi wako. Ikikupendeza tulikuwa tunashauri mambo haya matatu tu hapo chini.

1. Wewe kama raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na mkuu wa serikali yetu pendwa.
Tunaomba utoe kauli ya kusimamishwa wale wote waliohusika katika kashfa za ubadhilifu wa mali zetu za umma ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yao ufanyike.

Mheshimiwa raisi tunaomba kauli hiyo iwe ya kimamlaka na kiutekelezaji. Na ikionekana kuwa kauli yako imeshindwa kutekelezeka, basi viongozi wanaohusika kuwasimamia wabadhilifu hao waliwe wao vichwa, ili nafasi zao zichukuliwe na watanzania wengine ambao watakuwa wepesi kufuata maagizo yako ambayo ni yenye faida kwa taifa.

2. Ikibainika kwamba wabadhilifu hao hawakuhusika kwa namna moja au nyingine basi wasamehewe ili waendelee na majukumu yao ya kazi.

Lakini ikibainika kuwa wamehusika na ubadhilifu huo, wasiishie tu kupisha ofisi zao, bali tunaomba serikali yako iwachukulie hatua kali ya kisheria kuwafikisha mahakamani, na huko mahakamani ikibainika uhusika wao, basi serikali iiombe mahakama iwachukulie wahusika hatua kali ya kifungo kirefu na adhabu kali, huku mali zao zote zikizuiliwa na serikali, taratibu za kisheria zifuatwe, na hatiame mali hizo zitaifishwe na fedha zitakazopatikana kutoka katika mchakato huo zirudishwe kwa wananchi kwa kutujengea barabara, shule, hospital au chochote chenye manufaa kwetu.

3. Wahusika baada ya kumaliza vifungo vyao wasiruhusiwe kufanya kazi mahali popote ndani ya ardhi yetu ya Tanzania, isipokuwa kazi ya kilimo tu ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza mfumuko wa bei ndani ya nchi yetu.

Kwa hayo machache mheshimiwa raisi naomba niishie hapa. Nina imani kama raisi mwenye upendo na uchungu wa kweli kwa wananchi wako utafata ushauri huu na kuutekeleza kwa 100%

Ukishindwa kufanya haya, basi turuhusu sisi wananchi wa kawaida tuwafuate huko ofisini kwao tukawachomoe mmoja mmoja, maana sikufichi, sisi raia tuna hasira nao sana.

Nakutakia mafanikio mema katika utekelezaji wa majukumu yako.

Asanteni sana.
 
Hii nchi bado sana itakiwa kuongozwa kwa udikteta hamna haki za wafanyakazi wala demokrasia ...Mtu akazingua basi anafutwa kazini mazima sio kuamishwa ni hasara kubwa sana serikali inaingia kwa uzembe wa wachache yaani mabillion watu wanachota bila wasiwasi.

Kuongoza nchi yenye watu wana maadili mabovu ni hatari sana .
 
What's this ? A Monarchy ?

Hata Mornachy zilizobakia ni just Symbolical..., Sisi tuonaodhania tuna Separation of Powers ndio zaidi ya hata hao wenye Monarchy. Hio sio mbaya, mbaya zaidi ni raia ku-implement haya mambo ya Kale na kuona kana kwamba ni sawa.

We have a long, long, way to go, as things stands we are moving, though not forward but rather backwards.....
 
Hii nchi bado sana itakiwa kuongozwa kwa udikteta hamna haki za wafanyakazi wala demokrasia ...Mtu akazingua basi anafutwa kazini...
Hata mwenye huo udikteta inabidi awe macho maana haya majizi yana mitandao mikubwa mpaka nje huko hasa ukiyatishia kwenye hizi raslimali za bure yanazojichotea kila leo...Ukizubaa tu yanapita na wewe!

Usimwone mama kuwa ni dhaifu kwa kukasirika mpaka kuyaita stupid bila kuyafanya chochote. Anajua gemu hili la hatari linavyochezwa.

IMG-20230405-WA0172.jpg
 
Hii nchi bado sana itakiwa kuongozwa kwa udikteta hamna haki za wafanyakazi wala demokrasia ...Mtu akazingua basi anafutwa kazini mazima sio kuamishwa ni hasara kubwa sana serikali inaingia kwa uzembe wa wachache yaani mabillion watu wanachota bila wasiwasi.


Kuongoza nchi yye watu wana maadili mabovu ni hatari sana .
Wengine tulishasema zamani na tutaendelea kusema tena na tena hii Nchi inahitaji kaudikiteta dikiteta kadogo kadogo ka kudhibiti mali na rasilmali za Nchi zisiibwe na majizi na mafisadi ya siyo na huruma na watu wa kawaida wa Nchi hii!

Jamaa wa app plan kufanya wizi wao huwa tayari wameshazifanyia kazi loopholes zote zilizopo katika taratibu na sheria za Nchi !! Kwa kifupi wanajua what is gonna happen !!
 
What's this ? A Monarchy ?

Hata Mornachy zilizobakia ni just Symbolical..., Sisi tuonaodhania tuna Separation of Powers ndio zaidi ya hata hao wenye Monarchy..., Hio sio mbaya, mbaya zaidi ni raia ku-implement haya mambo ya Kale na kuona kana kwamba ni sawa.....

We have a long, long, way to go........, as things stands we are moving, though not forward but rather backwards.....
Thank you a lot for your comment mkuu
 
Hata mwenye huo udikteta inabidi awe macho maana haya majizi yana mitandao mikubwa mpaka nje huko hasa ukiyatishia kwenye hizi raslimali za bure yanazojichotea kila leo...Ukizubaa tu yanapita na wewe!

Usimwone mama kuwa ni dhaifu kwa kukasirika mpaka kuyaita stupid bila kuyafanya cho chote. Anajua gemu hili la hatari linavyochezwa!



View attachment 2578242
upo sahihi

Mpaka sasa naona kiongozi ni Makonda ndiyo anaweza angalia alivyokuwa tu mkuu wa mkoa alikuwa na power.

Tuongee ukweli Makonda ndo ataweza angalau kuendesha hii nchi kwa vile ni mbabe.
 
Hii nchi bado sana itakiwa kuongozwa kwa udikteta hamna haki za wafanyakazi wala demokrasia ...Mtu akazingua basi anafutwa kazini mazima sio kuamishwa ni hasara kubwa sana serikali inaingia kwa uzembe wa wachache yaani mabillion watu wanachota bila wasiwasi...
It's true broh
 
Wengine tulishasema zamani na tutaendelea kusema tena na tena hii Nchi inahitaji kaudikiteta dikiteta kadogo kadogo ka kudhibiti mali na rasilmali za Nchi zisiibwe na majizi na mafisadi ya siyo na huruma na watu wa kawaida wa Nchi hii !! Jamaa wa app plan kufanya wizi wao huwa tayari wameshazifanyia kazi loopholes zote zilizopo katika taratibu na sheria za Nchi !! Kwa kifupi wanajua what is gonna happen !!
Udikteta wa wastani kama wa China ndio njia bora ya kuzuia wizi na ubadhilifu mkubwa wa mali za umma popote pale ulimwenguni.
 
Unaleta ujumbe kama huu leo wakati jana tu Sabaya ameachiwa huru pamoja na ule uhuni wake, kwa ujinga wetu, CCM itaendelea kutuburuza kwa muda mrefu sana ujao, mpaka siku hiyo tutakaposema sasa basi, inatosha..

Samia kwa udhaifu wake kuwa kiongozi wa hili taifa kunaonesha wengi tulivyo mazuzu, Samia hawezi kuongoza taifa la wanaojitambua, angeikimbia ikulu mwenyewe.
 
Mkuu Pascal Mayalla kama una njia nyepesi za kumfikishia mheshimiwa raisi ujumbe huu kupitia taaluma yako ya habari, basi kwa heshima na taadhima tunaomba uitumie njia hiyo pia kufikisha ujumbe wetu kwa raisi.
Mkuu 6 Pack , asante, hili nimelipokea, ila humu JF, Mama anaingia mwenyewe in person na kutusoma, hivyo hoja yako hii, imemfikia.
P
 
upo sahihi !!


Mpaka sasa naona kiongozi ni Makonda ndo anaweza angalia alivyokuwa tu mkuu wa mkoa alikuwa na power....
Japokuwa Makonda anaweza kuwa na uthubutu wa ku deal na hao wabadhilifu, lkn itakuwa ngumu kufikia nafasi hiyo ya maamuzi kwa sababu tayari ashawekwa kwenye blacklist.
 
Unaleta ujumbe kama huu leo wakati jana tu Sabaya ameachiwa huru pamoja na ule uhuni wake, kwa ujinga wetu, CCM itaendelea kutuburuza kwa muda mrefu sana ujao, mpaka siku hiyo tutakaposema sasa basi, inatosha..

Samia kwa udhaifu wake kuwa kiongozi wa hili taifa kunaonesha wengi tulivyo mazuzu, Samia hawezi kuongoza taifa la wanaojitambua, angeikimbia ikulu mwenyewe.
😂😂😂 ni kweli mkuu.
 
Back
Top Bottom