Raisi Samia sio mfalme na sio mungu wa kuombwa kufanya kila kitu katika nchi yetu

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
✳️RAISI WA NCHI SAMIA SULUHU HASSAN SIO MFALME NA SIO MUNGU WA KUOMBWA KUFANYA KILA KITU KATIKA NCHI YETU‼️

🔵Na:Shujaa©️®️Ⓜ️

Ni kawaida katika jamii zetu za kiafrika kusikia wananchi wakikimbilia kwa maraisi wao kueleza shida, kuomba misaada kutoka kwao, kuwaomba wawafanyie maendeleo haya na yale ya hapa na pale kama katika ujenzi, Kilimo au uhitaji wa vyakula na maswala yote ya muhimu katika nchi.Na hata pale Rais wa nchi akishindwa kusuluhisha matatizo aliyoombwa kufanya, basi watu wote watamuona ni Rais dhaifu, watamtukana na wataona kuwa ndiye anayeyasababisha yote kutokea....

Vivyo hivyo katika nchi yetu ya Tanzania, tumejengewa utamaduni mbovu na mbaya sana ulioanzia katika katiba ya nchi yetu, unaotufanya kila matatizo na mahitaji yetu yote ya kimaendeleo katika miji, vijiji na kata na mikoa yetu inategemeana na fadhila za Rais wa nchi yetu, kwamba kila tunalohitaji kufanyiwa basi muamuzi wa mwisho wa sisi wananchi tuwe na maendeleo fulani hapa au pale ni mpaka Rais asikie kilio chetu na ndiye ana mamlaka ya kuamua mkoa gani sasa uendelee na mkoa gani usiendelee, nani apate huduma hizi na nani asipate huduma zile.Maana .Rais ndiye Mpaji(provider) wa kila kitu katika nchi ndio maana kila kinachotokea lazima yeye awajibike!

1652358630480.jpg

Ni ukweli kabisa usiopingika kuwa, Rais wa nchi anawajibu wa kuwahudumia raia wake na kusikiliza kero zao na kuzishughulikia lakini lazima tufahamu URAIS UNA MIPAKA YAKE TOFAUTI NA TAWALA ZA KIFALME, Na ikiwa tutaiondoa hiyo mipaka iliyowekwa, basi tutamfanya Rais kuwa ni Mfalme au tutamfanya Rais kuwa ni Mungu

Tatizo Kubwa la nchi hii ya Tanzania ambalo nalirudia tena na tena, na sitaacha kuwakumbusha kila niandikapo makala kama hizi ni swala la KUKOSA KATIBA MPYA. Katiba hii ya sasa ndio inayompa Rais wa nchi mamlaka kubwa ya Kifalme na ya Kimungu kwamba kila hitaji lolote la nchi lazima tuliombe kwa Rais na ndiye anayepaswa kutuamulia kuwa tupate au tukose!

Katiba yetu ya sasa ndio Imetufanya sisi wananchi tuwe OMBAOMBA KWA RAIS WA NCHI na ndiyo inayomfanya mtu mmoja(Rais) kuwa Mwamuzi wa hatima yetu ya kila kitu tunachokihitaji katika nchi

Leo hii sasa, kumezidi kuongezeka kelele na vilio vingi vya wananchi kuelekea kwa Rais wa nchi Samia Suluhu Hassan katika kila kona ya Tanzania,kwa maskini na matajiri juu kupanda kwa bei za mafuta,na bei za bidhaa mbalimbali na kupelekea mfumuko wa bei ambao unatuumiza wananchi wengi hasa sisi tulio wa hali ya chini.Wananchi wote na Taifa lote sasa , macho yao yapo kwa Rais wetu Samia wanamlilia ili aweze kuwasaidia na kuwatoa katika dimbwi hili na wanaona ndiye mtu pekee wa kuwasaidia na ndiye msababishi wa mambo yote haya kutokea. Kwa bahati mbaya Rais mwenyewe ameonyesha hana analoweza kuwasaidia kwasababu ni janga la kidunia linalotokana na vita vya Urusi na Ukraine

Ila chanzo cha yote haya, sio Rais wa nchi kushindwa kutusaidia kwa tunayomuomba bali ni sisi wenyewe wananchi ndio tumeshindwa kujua lipi la kwanza la kulishughulikia kabla haya mambo hayajatokea.Tumembebesha mzigo mkubwa Rais wa nchi na kumpa mamlaka kubwa kikatiba ambazo hata yeye nyingine hawezi kuzijibu wala kuzitolea maelezo kwasababu tumefanya Rais kuwa kama Mfalme na Kama Mungu ambaye hata dhoruba ikitokea lawama ipo kwake, Watu wengi wakifa ajarini bado lawama zipo kwake

🔜Lazima tufahamu, ikiwa kweli tunasema nchi yetu ni ya kidemocrasia basi tujue Mamlaka kubwa haipaswi kuwa mikononi mwa Rais bali mamlaka kubwa ya kuamua mustakabadhi wa nchi yetu iendeshweje, ipo mikononi mwetu wananchi.Sisi wananchi ikiwa kweli tungekuwa Mamalaka basi tusingekuwa omba omba kama tulivyosasa wala tusingerusha lawama zote hizi kwa Raisi

Matitizo kama haya yanapotokea inatupasa, washauri na waamuzi wa nini kifanyike, inapaswa yatoke kwa wananchi wenyewe lakini kutokana na Katiba mbovu tuliyo nayo sasa ndio tumemuachia Rais atuamulie kila kitu katika nchi yetu, maana hata akitaka tufe kwa njaa ,Yeye ndiye ataamua wala hatuna nguvu wala mamlaka yeyote ya kumuhoji wala kumuwajibisha....

🔜Pia lazima tujue tofauti ya utawala wa kiraisi na utawala wa kifalme.Mfalme ndiye mtawala mwenye mamlaka ya mwisho ya kila mwananchi, Neno lake ndio sheria, Neno lake ndio katiba, akitaka fulani afe lazima atakufa wala hatahojiwa na pia ndiye anayeamua nani ampe nini na nani asimpe,na watu wote wakitaka lolote ni lazima waliombe moja kwa moja kwa mfalme.Sasa Katiba ya sasa ya nchi yetu pamoja inajipambanua ni nchi ya kidemocrasia lakini imempa Rais wa nchi mamlaka zote za kifalme za kuamua nini tupate na nini tusipate, nani akae pale na nani asikae pale,ndio anatoa maamuzi ya mwisho katika mihimili yote wala hawezi kushtakiwa kwa kosa lolote atakalofanya kipindi chote atakachokuwa madarakani

Kwa msingi wa Katiba yetu ya Sasa,ni Kweli Sisi wananchi ni Ombaomba kwa Rais, Na Rais wa nchi ni Mfalme wa Nchi ya Tanzania , ndio tunasubiri atupe majibu ya nini kifanyike na hata asipofanya, hatuna la kumfanya wala kumuwajibisha..JE TUENDELEE NA UTAMADUNI HUU?JE TUENDELEE NA KATIBA HII ❓

Matitizo kama haya hayatakoma Ikiwa HATUTADAI KATIBA MPYA AMBAYO ITATURUDISHIA MAMLAKA WANANCHI YA KUAMUA NAMNA YA KUENDESHA NCHI YETU KATIKA USTAWI TUNAOTAKA SISI.Sisemi Katiba mpya ndio itatupa maisha mazuri kila mmoja ila Katiba mpya itaturudishia mamlaka umma ya kuamua namna ya kujiendesha wenyewe, hata kama yakitokea majanga kama haya bado hatutakuwa na wa kumlaumu bali tutapaswa tujilaumu sisi wenyewe

Nawakumbusha tu watanzania, tunapoyaona haya yanatokea ndio yatukumbushe kujua Umuhimu wa kudai katiba mpya, Vinginevyo Rais ndio atawaamulia mfukuzwe barabarani, mfukuzwe masokoni mkawe panya Road mitaani.Poleni nyote na changamoto tulizo nazo

NI MUNGU TU NDIYE MPAJI WETU WA KILA KITU NA MTOA RIDHIKI SIO RAIS WA NCHI.Kipindi hichi hakihitaji kurusha lawama kwa yeyote si kwa Rais wala sio kwa viongozi wala sio kwetu wananchi, bali ikiwa una ushauri wa nini kifanyike basi toa ushauri ila ikiwa una imani ,zidi kumuombea Rais wa nchi Samia,ajue namna ya kuingoza nchi katika namna ambayo ataweza kutanguliza vipaumbele vya msingi na vya lazima kwa nchi ili kurudisha nchi katika ustawi na kuaminiana.Acha lawama Ombea Nchi yako , ombea viongozi wako wa nchi.Lawama hazitutoi kwenye matatizo, Rais sio Mungu akupe kila kitu unachohitaji,Ila Tuombe Mungu na tufanye kazi tuinue uchumi wetu wa ndani ili kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa zilizopo sasa

🔵Na:Shujaa Charles Richard Mwaisemba(©️®️Ⓜ️)

stmwaisembac@gmail.com

0712054498/0785248997
 
Alafu huyu sio Mtanganyika ,

Anakuwaje rahisi wa Tanganyika

Ni Bora angebaki kua rahisi wa Muungano
 
RAISI WA NCHI SAMIA SULUHU HASSAN SIO MFALME NA SIO MUNGU WA KUOMBWA KUFANYA KILA KITU KATIKA NCHI YETU

Na:Shujaa

Ni kawaida katika jamii zetu za kiafrika kusikia wananchi wakikimbilia kwa maraisi wao kueleza shida, kuomba misaada kutoka kwao, kuwaomba wawafanyie maendeleo haya na yale ya hapa na pale kama katika ujenzi, Kilimo au uhitaji wa vyakula na maswala yote ya muhimu katika nchi.Na hata pale Rais wa nchi akishindwa kusuluhisha matatizo aliyoombwa kufanya, basi watu wote watamuona ni Rais dhaifu, watamtukana na wataona kuwa ndiye anayeyasababisha yote kutokea....

Vivyo hivyo katika nchi yetu ya Tanzania, tumejengewa utamaduni mbovu na mbaya sana ulioanzia katika katiba ya nchi yetu, unaotufanya kila matatizo na mahitaji yetu yote ya kimaendeleo katika miji, vijiji na kata na mikoa yetu inategemeana na fadhila za Rais wa nchi yetu, kwamba kila tunalohitaji kufanyiwa basi muamuzi wa mwisho wa sisi wananchi tuwe na maendeleo fulani hapa au pale ni mpaka Rais asikie kilio chetu na ndiye ana mamlaka ya kuamua mkoa gani sasa uendelee na mkoa gani usiendelee, nani apate huduma hizi na nani asipate huduma zile.Maana .Rais ndiye Mpaji(provider) wa kila kitu katika nchi ndio maana kila kinachotokea lazima yeye awajibike!!!

Ni ukweli kabisa usiopingika kuwa, Rais wa nchi anawajibu wa kuwahudumia raia wake na kusikiliza kero zao na kuzishughulikia lakini lazima tufahamu URAIS UNA MIPAKA YAKE TOFAUTI NA TAWALA ZA KIFALME, Na ikiwa tutaiondoa hiyo mipaka iliyowekwa, basi tutamfanya Rais kuwa ni Mfalme au tutamfanya Rais kuwa ni Mungu

Tatizo Kubwa la nchi hii ya Tanzania ambalo nalirudia tena na tena, na sitaacha kuwakumbusha kila niandikapo makala kama hizi ni swala la KUKOSA KATIBA MPYA. Katiba hii ya sasa ndio inayompa Rais wa nchi mamlaka kubwa ya Kifalme na ya Kimungu kwamba kila hitaji lolote la nchi lazima tuliombe kwa Rais na ndiye anayepaswa kutuamulia kuwa tupate au tukose!

Katiba yetu ya sasa ndio Imetufanya sisi wananchi tuwe OMBAOMBA KWA RAIS WA NCHI na ndiyo inayomfanya mtu mmoja(Rais) kuwa Mwamuzi wa hatima yetu ya kila kitu tunachokihitaji katika nchi

Leo hii sasa, kumezidi kuongezeka kelele na vilio vingi vya wananchi kuelekea kwa Rais wa nchi Samia Suluhu Hassan katika kila kona ya Tanzania,kwa maskini na matajiri juu kupanda kwa bei za mafuta,na bei za bidhaa mbalimbali na kupelekea mfumuko wa bei ambao unatuumiza wananchi wengi hasa sisi tulio wa hali ya chini.Wananchi wote na Taifa lote sasa , macho yao yapo kwa Rais wetu Samia wanamlilia ili aweze kuwasaidia na kuwatoa katika dimbwi hili na wanaona ndiye mtu pekee wa kuwasaidia na ndiye msababishi wa mambo yote haya kutokea. Kwa bahati mbaya Rais mwenyewe ameonyesha hana analoweza kuwasaidia kwasababu ni janga la kidunia linalotokana na vita vya Urusi na Ukraine

Ila chanzo cha yote haya, sio Rais wa nchi kushindwa kutusaidia kwa tunayomuomba bali ni sisi wenyewe wananchi ndio tumeshindwa kujua lipi la kwanza la kulishughulikia kabla haya mambo hayajatokea.Tumembebesha mzigo mkubwa Rais wa nchi na kumpa mamlaka kubwa kikatiba ambazo hata yeye nyingine hawezi kuzijibu wala kuzitolea maelezo kwasababu tumefanya Rais kuwa kama Mfalme na Kama Mungu ambaye hata dhoruba ikitokea lawama ipo kwake, Watu wengi wakifa ajarini bado lawama zipo kwake

Lazima tufahamu, ikiwa kweli tunasema nchi yetu ni ya kidemocrasia basi tujue Mamlaka kubwa haipaswi kuwa mikononi mwa Rais bali mamlaka kubwa ya kuamua mustakabadhi wa nchi yetu iendeshweje, ipo mikononi mwetu wananchi.Sisi wananchi ikiwa kweli tungekuwa Mamalaka basi tusingekuwa omba omba kama tulivyosasa wala tusingerusha lawama zote hizi kwa Raisi

Matitizo kama haya yanapotokea inatupasa, washauri na waamuzi wa nini kifanyike, inapaswa yatoke kwa wananchi wenyewe lakini kutokana na Katiba mbovu tuliyo nayo sasa ndio tumemuachia Rais atuamulie kila kitu katika nchi yetu, maana hata akitaka tufe kwa njaa ,Yeye ndiye ataamua wala hatuna nguvu wala mamlaka yeyote ya kumuhoji wala kumuwajibisha....

Pia lazima tujue tofauti ya utawala wa kiraisi na utawala wa kifalme.Mfalme ndiye mtawala mwenye mamlaka ya mwisho ya kila mwananchi, Neno lake ndio sheria, Neno lake ndio katiba, akitaka fulani afe lazima atakufa wala hatahojiwa na pia ndiye anayeamua nani ampe nini na nani asimpe,na watu wote wakitaka lolote ni lazima waliombe moja kwa moja kwa mfalme.Sasa Katiba ya sasa ya nchi yetu pamoja inajipambanua ni nchi ya kidemocrasia lakini imempa Rais wa nchi mamlaka zote za kifalme za kuamua nini tupate na nini tusipate, nani akae pale na nani asikae pale,ndio anatoa maamuzi ya mwisho katika mihimili yote wala hawezi kushtakiwa kwa kosa lolote atakalofanya kipindi chote atakachokuwa madarakani

Kwa msingi wa Katiba yetu ya Sasa,ni Kweli Sisi wananchi ni Ombaomba kwa Rais, Na Rais wa nchi ni Mfalme wa Nchi ya Tanzania , ndio tunasubiri atupe majibu ya nini kifanyike na hata asipofanya, hatuna la kumfanya wala kumuwajibisha..JE TUENDELEE NA UTAMADUNI HUU?JE TUENDELEE NA KATIBA HII

Matitizo kama haya hayatakoma Ikiwa HATUTADAI KATIBA MPYA AMBAYO ITATURUDISHIA MAMLAKA WANANCHI YA KUAMUA NAMNA YA KUENDESHA NCHI YETU KATIKA USTAWI TUNAOTAKA SISI.Sisemi Katiba mpya ndio itatupa maisha mazuri kila mmoja ila Katiba mpya itaturudishia mamlaka umma ya kuamua namna ya kujiendesha wenyewe, hata kama yakitokea majanga kama haya bado hatutakuwa na wa kumlaumu bali tutapaswa tujilaumu sisi wenyewe

Nawakumbusha tu watanzania, tunapoyaona haya yanatokea ndio yatukumbushe kujua Umuhimu wa kudai katiba mpya, Vinginevyo Rais ndio atawaamulia mfukuzwe barabarani, mfukuzwe masokoni mkawe panya Road mitaani.Poleni nyote na changamoto tulizo nazo

NI MUNGU TU NDIYE MPAJI WETU WA KILA KITU NA MTOA RIDHIKI SIO RAIS WA NCHI.Kipindi hichi hakihitaji kurusha lawama kwa yeyote si kwa Rais wala sio kwa viongozi wala sio kwetu wananchi, bali ikiwa una ushauri wa nini kifanyike basi toa ushauri ila ikiwa una imani ,zidi kumuombea Rais wa nchi Samia,ajue namna ya kuingoza nchi katika namna ambayo ataweza kutanguliza vipaumbele vya msingi na vya lazima kwa nchi ili kurudisha nchi katika ustawi na kuaminiana.Acha lawama Ombea Nchi yako , ombea viongozi wako wa nchi.Lawama hazitutoi kwenye matatizo, Rais sio Mungu akupe kila kitu unachohitaji,Ila Tuombe Mungu na tufanye kazi tuinue uchumi wetu wa ndani ili kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa zilizopo sasa

Na:Shujaa Charles Richard Mwaisemba()

stmwaisembac@gmail.com

0712054498/0785248997
UMEANDIKA MENGI MPAKA YAMENISHINDA KUSOMA!!
 
Kama hawezi na kazi zimemzidia anaweza kupumzika, kwa mfumo wa Tanzania ndiyo raisi ni Mfalme kwa maana ni Bosi wa kila mtu, hakuna linaloweza kufanyika bila ya raisi kukubali, mfano hata tu Waziri Mkuu hawezi kuchukua hatua bila ya kumuuliza raisi, Mkuu wa Mkoa/Wilaya wote hawa ni raisi anaamua hata Wakuu wa mashirika kama ttcl, nssf wote Bosi wao ni raisi, sasa ulitaka nani afanye ?

Ndo maana nasema kama imemzidi aende kwingine anakoweza, Magu alipiga mzigo miaka 6 na nchi ilikwenda, Samia amekuta nchi ina deni dogo sana, yeye (Samia) ndani ya mwaka 1 kaongeza kwa > 50% ya deni lote alilokuta, …
 
Kwa sasa Rais Samia huwezi kumkwepa kwa lolote linalotokea au litakalotokea hapa nchini, Ni Rais na kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa yeye ni kila kitu...ni Mfalme.

Na ndiyo maana sisi wenye akili tunataka kuandika katiba nyingine ila CCM hawataki.
 
Tatizo Kubwa la nchi hii ya Tanzania ambalo nalirudia tena na tena, na sitaacha kuwakumbusha kila niandikapo makala kama hizi ni swala la KUKOSA KATIBA MPYA. Katiba hii ya sasa ndio inayompa Rais wa nchi mamlaka kubwa ya Kifalme na ya Kimungu kwamba kila hitaji lolote la nchi lazima tuliombe kwa Rais na ndiye anayepaswa kutuamulia kuwa tupate au tukose!
Bravo !!
 
Sawa, Kwa lugha ya kwetu fuso Ni Aliye Data,

Na Hakuna aliyeitwaa kwa Jina la Fuso akasalimika
usijitoe ufahamu, nakwambia hivi kwa katiba hii Rais wa Tanzania ni mfalme, hawezi kushindwa kufanya lolote alakalo; ndiyo maana tunaopopa sana kama nchi kupata Rais mwengine chizi tena tutakwishaaa. Tuungane kubadilisha katiba mapema !!
 
Back
Top Bottom