Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

Is it fair ukatumia milion 50 kwa safari ya kwenda kumsalimia mtu mwenye njaa na ukaishia kumpa mkono na kurudi kwako?
It is not fair na utakuwa uwendawazimu. Lakini mkuu mfano wako na tunachojadili havina uhusiano. Kuna janga pale ambalo limegharimu maisha ya watu sio mtu. Wewe unalinganisha vifo na njaa! kwenda kumpa pole mfiwa ukiwa mikono mitupu nayo ni maajabu mengine.
 
Hongereni wapinzani kwa kazi nzuri na ya wito ambayo mmekuwa mkiendelea kuifanya kwa watanzania wenzetu waliokutwa na tetemeko la ardhi huko bukoba
 
Akiwa mwanza alisema Mwanza sina namna ya kuikwepa madiwan, wabunge na meya ni wa ccm sasa kwa bukoba utajaza mwenyewe......
BK ni UKAWA tu kumbe ndio maana hajaenda ina maana sio rais wa wa watanzania bali ni rais wa CCM ahsante mkuu kwa kunifumbua macho.
 
KWANI AKIENDA MAGUFULI NDO NYUMBA ZITAJIJENGA? KWANI AKIENDA MAGUFULI,WALIOKUFA WATAFUFUKA? WAZIRI MKUU ANATOSHA KWENDA.
RAIS WANGU MAGUFULI PIGA KAZI MZEE HAYA MANENO TUMEYAZOE.
MAGUFULI JUU JUU JUU ZAIDI
Kazi gani hiyo mkuu zaidi ya ubinadamu ??? Hata hii ni sehemu ya kazi yake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hata kapicha kamoja tu kakimuonyesha mungu wa Ikulu akiwa na wahanga wa tetemeko la ardhi au akizuru maeneo yaliyoathirika hakuna. Kuna tatizo, sijui kwanini wanaficha alipo mungu wa Ikulu.

Tuliambiwa kaahirisha shughuli na ziara za kimataifa ili ashighulikie janga la tetemeko la ardhi Bukoba na Mwanza, Lakini huku Bukoba Hatujamwona/Hajafika!!
 
Hajitambui huyu mtu anakula upepo mwanana wa Indian Ocean pale Ikulu, huku wahanga wa tetemeko wakiwa hawajapata msaada wowote ule toka Serkalini.

Sasa kulikuwa na haja gani kuahirisha safari?
 
Tuliambiwa kaahirisha shughuli na ziara za kimataifa ili ashighulikie janga la tetemeko la ardhi Bukoba na Mwanza, Lakini huku Bukoba Hatujamwona/Hajafika!!
Vipaumbele ndugu...!
 
Kazi gani hiyo mkuu zaidi ya ubinadamu ??? Hata hii ni sehemu ya kazi yake.
Ubinadamu upi unaoutaka wewe? Sehemu ya kazi si Waziri Mkuu kamuwakilisha tayari.Madaktari kutoka bugando wameenda kutoa tiba kwa wahanga.Na Serikali bado inatoa mahitaji kwa wahanga.
 
Ujue siku hizi magari yana lala njiani subiri atakuja tu labda kalala tinde atafika kesho
 
Rais John Pombe Magufuli alighairi safari ya zambia ili aende Kagera kwenye maafa ya tetemeko. Lakini sijaona akiongea na taifa wala sijamwona live katika tukio hilo. Je mikakati ya kuwasaidia waathirika inafanywa kimya kimya, kama katuma wawakilishi kulikua na haja gani kuahirisha safari ya Zambia?

Lile tukio kubwa sana halikuwa la kiongozi mkuu kukaa kimya. Zaidi sana aliacha shughuli zingine ili ashughulikie maafa haya, yuko wap? Ikulu sio sehemu ya maafa yampasa afike eneo la tukio. Vingenevyo tutaamini alisitisha safari ya Zambia kwa kazi zingine na sio kuhudumia wahanga. Timu ya kupanga utendaji wa maafa ipo, sijui yeye mikakati ganu inamfanya ajifungie.

Please rais wetu nenda kawahudumie wahanga.

Rais wangu uko wapi Zambia, Magogoni au kagera?
 
Hata kapicha kamoja tu kakimuonyesha mungu wa Ikulu akiwa na wahanga wa tetemeko la ardhi au akizuru maeneo yaliyoathirika hakuna. Kuna tatizo, sijui kwanini wanaficha alipo mungu wa Ikulu.
Mkuu kwani wewe kijijini kwenu yamepita matukio mangapi hujaenda wala hata rambirambi hujatoa?
 
Akienda huko Bukoba na Mwanza mtaanza kumhesabia safari za kwenda kwake. Hamna maana ninyi. Bora aendelee kuratibu maafa akiwa Ikulu kwa vile kule kuna wakuu wa mikoa na wilaya wanaweza kufanya vema
Akienda utakuja na ngonjela gani??
 
Kinachoongelewa hapa ni kuahirisha safari ya kwenda zambia kutokana na janga la tetemeko la ardhi kwa mantiki hiyo tulitegeme kumuona mkuu wa kaya kwenye eneo la tukio
 
Raisi wa Kenya Uhuru keshatuma ndege zenye misaada kwenda bukoba wa kwetu bado amelala.
Balozi wa Kenya amesema msafara wa magari upo njiani kupeleka msaada Kagera. Swali ndege za KDF zimetuwa au zimezuiliwa kwa sababu zisizo eleweka?
 
rais john pombe magufuli alighairi safari ya zambia ili aende kagera kwenye maafa ya tetemeko. Lakn sijaona akiongea na taifa wala sijamwona live katika tukio hilo. Je mikakati ya kuwasaidia waathirika inafanywa kimya kimya, kama katuma wawakilishi kulikua na haja gani kuahirisha safari ya zambia?

Lile tukio kubwa sana halikua la kiongoz mkuu kukaa kimya. Zaid sana aliacha shughuli zingine ili ashughulikie maafa haya, yuko wap?? Ikulu sio sehem ya maafa yampasa afike eneo la tukio. Vingenevyo tutaamini alisitisha safari ya zambia kwa kaz zingine na sio kuhudumia wahanga. Tim ya kupanga utendaji wa maafa ipo, sijui yeye mikakati gan inamfanya ajifungie.pls rais wetu nenda kawahudumie wahanga.

Rais wangu uko wap zambia, magogoni au kagera??
Unahoji kuwa Mkuu Zambia hayupo na Kagera hajafika?

Usije shangaa wale vijana wa Si... roo wakakupa 'title' ya kuwa wewe ni mchochezi..........
 
Back
Top Bottom