SI KWELI Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki Afariki Dunia

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
IMG_9519.jpeg


Inasemekana kuwa Rais wa awamu ya Pili wa Afrika Kusini Thabo Mbeki amefariki dunia. Hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi.
 
Tunachokijua
Thabo Mvuyelwa Mbeki alizaliwa Juni 18, 1942, Mbewuleni, kijiji kidogo huko Idutywa, Transkei, Afrika Kusini.

Wazazi wake wote wawili walikuwa walimu, wanaharakati na wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini (CPSA baadaye ikaitwa SACP) na baadae ANC.

Mnamo Desemba 1997, Mkutano Mkuu wa 50 wa ANC ulimchagua Mbeki bila kupingwa kumrithi Nelson Mandela kama Rais wa ANC.

Kufuatia uchaguzi wa kitaifa wa 1999, ambao ANC ilishinda kwa kura nyingi, Mbeki alichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya Pili wa Afrika Kusini. Alichaguliwa tena kwa muhula wa pili mnamo 2004 hadi 2008.

Miongoni mwa mambo yanayomtambulisha zaidi duniani ni msimamo wake wa Kutokuafikiana na wanasayansi pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa VVU ndio chanzo cha Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI) pamoja na kumfuta unaibu Waziri na kumnyima stahiki zake zote Mke wa Hayati Nelson Mandela, Winnie Mandela kwa kutokufuata maelekezo ya chama kwenye utendaji wake wa kazi.

Aliwahi pia kuwa ni Makamu wa Rais, chini uongozi wa Hayati Rais Nelson Mandela kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1999, pia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2003.

Taarifa za kifo chake
Habari zinazohusu kifo cha Rais huyo wa Pili wa Jamhuri ya watu wa Afrika Kusini ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na Blog tofauti Januari 3, 2024.

Kwenye Mtandao wa Kijamii wa X, ukurasa wenye jina la TNG Breaking uliandika taarifa hii ikisema:

“Thabo Mbeki, Rais wa zamani wa Afrika Kusini amefariki dunia. Akiwa na miaka 74, Mbeki alikimbizwa hospitalini, Jumanne ya Januari 2, 2024 akikabiliwa na maradhi, kisha akatangazwa kufariki Dunia na Madaktari”

Aidha, ukurasa wa mwandishi wa Habari wa Nigeria, President Eniola Daniel ulichapisha pia taarifa ya kifo hili.

JamiiCheck ilibaini pia uwepo wa taarifa hii kwenye blog ya Vatican News, BNN Breaking, Daily Brief, The Nigerian Voice pamoja na ukurasa wa gazeti la Mwananchi kwenye mtandao wa Instagram.

Ukweli upoje?

JamiiCheck imefuatilia taarifa hii kutoka kwenye vyanzo vyake vya kuaminika vilivyopo nchini Afrika Kusini na kubaini kuwa haina ukweli.

Aidha, hakuna chombo chochote cha habari nchini Afrika Kusini, pamoja na vyombo vya habari vya kimataifa vilivyoripoti kuhusiana na kifo cha Mbeki.

Aidha, taarifa ya Taasisi ya Thabo Mbeki, iliyotolewa baadae ilikanusha madai hayo na kuwataka watu kuyapuuza kwani Mbeki ni mzima wa Afya.

img_9521-jpeg.2861031

Taarifa inayokanusha kifo cha Thabo Mbeki
Ushahidi mwingine wa habari hii kutokuwa na ukweli ni baadhi ya vyombo vya habari vilivyoichapisha kuiondoa hewani (kuifuta) ili isiendelee kuonekana kwa umma. Mathalani, ukurasa wa Instagram wa Kampuni ya Mwananchi.
Hii taarifa nimeitoa Mwananchi , kama si sahihi nachukua nafasi hii kuomba radhi , na ninaomba uzi ule ufutwe mara moja
 
No research no right to speak/write here . Kudos Jamii check kwa ufafanuzi wa taarifa hii
 
Kwanini mtu anapenda kuwa mjumbe wa shetani, kusambaza habari za kifo? Madhara yake ndiyo haya.. Watu wajizuie kutangaza habari za kifo, kama kipo kila mtu atajua ...haina haja ya kiherehere
 
Kwanini mtu anapenda kuwa mjumbe wa shetani, kusambaza habari za kifo? Madhara yake ndiyo haya.. Watu wajizuie kutangaza habari za kifo, kama kipo kila mtu atajua ...haina haja ya kiherehere

Ni maumbile, genetics matters a lot.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom