Miili ya Watanzania waliofariki Septemba 2023 kurejeshwa nchini kesho Januari 25, 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
MIILI ya Watanzania watatu waliofariki dunia Septemba mwaka jana, kwenye ajali ya moto Afrika Kusini, inatarajiwa kurejeshwa kesho nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana, Watanzania hao waliopoteza maisha ni Said Mohames Kisarazo, Ibrahim Mohamed Kisarazo na Mohames Ismail Amiri.

“Ubalozi unawaarifu kuwa Januari 20, mwaka huu, miili ya Diaspora watatu waliofariki (dunia) kwa ajali ya moto Agosti 31, 2023 jijini Johannesburg, Afrika Kusini, ilifikishwa kwa kampuni itakayosafirisha kwenda Tanzania kwa mazishi,” alisema Balozi Bwana.

Kwa mujibu wa Balozi Bwana, miili ya Watanzania hao itasafirishwa kwa awamu mbili. Leo itasafirisha miili miwili ya Said Mohames Kisarazo na Ibrahim Mohamed Kisarazo kwa ndege ya AIRLINK Flight itakayoondoka Afrika Kusini saa 4:00 usiku na kuwasili Tanzania kesho saa 8:30 usiku.
 
Mungu awasitiri marehemu na adhabu ya kaburi.

Jambo jema Ubalozi kushungulikia hili
 
Back
Top Bottom