Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,231
- 6,471
Ktk pitapita zangu viunga vya YouTube nakutana na kisa hiki.
Ikumbukwe South Africa walikuwa na kambi ya wapigania Uhuru eneo la Mazimbu Morogoro.
Aliyewahi kuwa Rais wa South Africa Thabo Mbeki 1999 Hadi 2008 alikuwa na Mtoto mmoja tu wa pekee aitwaye Kwanda Mbeki. Alimzaa na Mwanafunzi wa secondary akiwa na miaka 16 tu. Alitozwa adhabu ya ng'ombe watano Kama adhabu ya kumbebesha Mwanafunzi mwenzie tena Mtoto mimba, ikaisha kimila hivyo japo hawakuoana.
Thabo Mbeki aliendelea na shule hadi elimu ya juu pasipo kumuona Mtoto wake Kwanda kutokana na kuikimbia Africa ya kusini kimasomo na kiusalama. Mbeki alipata elimu yake ktk nchi mbalimbali huku mtoto akikulia kwa Mama yake Mbeki au Bibi yake Mtoto huyu mwanaume.
Sasa bwana mtoto huyu baada ya kukua alianza kuandamwa na mikosi ya kutekwa Mara tatu na watu wasiojulikana bila kufanikiwa.
Bibi hakuwa akijua babaye mtoto yupo wapi na yupo hai au laah. Akaamua kumtorosha mtoto Kwanda kumpeleka Zambia kwa msaada wa chama cha ANC na baadae tena Swaziland baada ya kuona watekaji wanamfuatilia. Baadye baada ya miaka mitatu alitoroshwa Swaziland na kuletwa Morogoro Tanzania.
Mtoto aliishi ktk kambi ya Mazimbu Morogoro kuanzia 1983 hadi 1989 alipochukuliwa na watu waliokuwa wakizungumza Kiswahili kizuri Sana na Kingereza chenye lafudhi ya waswahili. Iko hivi, watu hao waliripoti kambini na kuongea na uongozi wa kambi na kuomba ofisi ya muda na kuomba kuitiwa Kijana huyo wa Mbeki. Walimhoji kwa Siri mtu huyu ambaye sio Mtoto tena kwa masaa matatu na kuondoka naye kwa gari walilokujanalo.
Tangu siku hiyo hakuonekana tena. Alikuwa mtoto wa pekee wa Rais wa baadae wa South Africa Thabo Mbeki. Kisa hiki kinamtesa Rais huyu mstaafu hadi leo.
Kisa hiki kilikuja kujulikana na kupelelezwa bila kupata majibu baada ya Mandela kuwa Rais 1994 na Kuunda tume ya ukweli na Maridhiano yaani Truth and Reconciliation Commission. Mambo Mengi majibu na muafaka ulipatikana isipokuwa hili la kijana wa Mbeki. Rais Mbeki alikuja kuoa lakini maskini ya Mungu hakuwahi kumpata Mtoto ktk ndoa yake. Dunia ina Mengi na Mengi hayo ni yetu binadamu pia.
Kina na nani na walitumwa na nani kumteka na kumtowesha Mtoto huyu wa Rais ajaye ktk Taifa lilojaa ulinzi na inteligensia kali?