Rais Samia Suluhu alitaka Bunge kujadili Bajeti badala ya kumfananisha yeye na Hayati Magufuli

Mheshimiwa mama Samia ana nafasi kubwa ya kurekebisha yote mabaya yaliyofanywa katika uongozi wa Magufuli, ila anakosea kusema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Mheshimiwa Mbowe ameandika vizuri kwamba, “...kivuli cha Magufuli bado kinamtesa mama Samia...”. Je mama Samia atawezaje kurekebisha makosa ya utawala uliopita ilhali yeye ni kitu kimoja na utawala uliopita? Maneno haya yanamfunga mama Samia kiutendaji.
Watu mnakosea sana, mnategemea aseme yuko kinyume naye aamshe mjadala mkubwa na asiungwe mkono na wafuasi wa Magu?
Kuna wakati ukiwa KIONGOZI unapaswa kuwa mnafiki kidogo.
Ki matendo mama na Magu ni vitu viwili tofauti
 
Hapana. JPM bila haya wala soni aliwaambia wastaafu kila zama zina kitabu chak, wanyamaze nao wakatii. Ikiwa hii ni awamu ya sita kwa nini tuendelee kusomeshwa kitabu cha awamu ya tano kilichojaa mashairi ya huzuni, mateso, vilio na mustakabali wa maisha ya watu usioeleweka?

Aseme yuko ccm tu kama jpm, inatosha, siyo yeye na jpm ni kitu kimoja.

Ni kweli kimatendo wanaweza kuwa tofauti. Lakini uelewe kuwa siasa is about perception, what you perceive baada ya kusikia. Kinachosikika kutoka kwake ndicho watu wanaperceive na kuamini.
 
Mama alisema kwamba ataendeleza yale mema yote aliyoyafanya mwendazake, kwa hiyo yale mabaya ya Magufuli Mama ameshayazika.
 
Watanzania ni watu wa ajabu kabisa sijui aliyewaroga nani sasa ulitaka aseme yeye ni kitu kimoja na Mbowe?

Samia si Rais wa kuchaguliwa ni Rais kwa mujibu wa katiba ibara ya 37/5
Article 37, subsection 5 states:
"Where the office of President becomes vacant by reason of death, resignation, loss of electoral qualifications or inability to perform his functions due to physical infirmity…then the Vice-President shall be sworn in and become the President for un expired period."

yupo pale kumalizia kipindi cha miaka 4 kilichobaki utamtenganisha vipi na JPM ? Leo hakuna mradi atakaosema ambao umeanza kuanzia tarehe 19 mwezi 3 siku anaapishwa atataja miradi ambayo alishiriki kuianzisha kama makamu wa Rais na Rais alikuwa JPM

Huwezi kumtengenisha Samia na JPM hata kidogo Samia amekuwa na JPM miaka 6 na majukumu yake kama Makamu wa Rais yanajulikana kikatiba 50,48 vifungu hvyo vinazungumzia Vice-President, his duties and powers

Kama mnaona JPM hafai kukumbukwa kwenye nchii hii subirini Lissu akiwa Rais mpleke marekebisho ya katiba kufuta Urais wa JPM japo Dunia nzima itawaona watu wa ajabu kuwai kuishi kwenye Dunia lakini kusema Samia hasijiushishe na JPM mnachekesha sana tena sana na kuonekana mlivyo mbumbumbu kiakili.
Wanataka wampotoshe mama,hii nchi kwa sasa jinsi wananchi wengi wanajua kazi alizofanya Magufuli kujitenga naye tena walikuwa naye ni kujimaliza.Mama aendelee hivyohivyo.
 
Hapana. JPM bila haya wala soni aliwaambia wastaafu kila zama zina kitabu chak, wanyamaze nao wakatii. Ikiwa hii ni awamu ya sita kwa nini tuendelee kusomeshwa kitabu cha awamu ya tano kilichojaa mashairi ya huzuni, mateso, vilio na mustakabali wa maisha ya watu usioeleweka?

Aseme yuko ccm tu kama jpm, inatosha, siyo yeye na jpm ni kitu kimoja.

Ni kweli kimatendo wanaweza kuwa tofauti. Lakini uelewe kuwa siasa is about perception, what you perceive baada ya kusikia. Kinachosikika kutoka kwake ndicho watu wanaperceive na kuamini.
Mpeni nafasi aongoze kwa namna yake
 
Uko sahihi sana, kuna watu wanatamani amponde Magu, akifanya hivyo ataharibu kila kitu, anajua vyema anategwa
Hata mm simpendi Magu kupita kiasi lakini siwezi kumponda hadharani itakuwa ni upumbavu mkubwa sn, kiongozi lazima uwe na hekima na busara
 
ccm watagombana kwa sabbau mbalimbali lakini linapokuja swala la kutawala nchi, WATAUNGANA SANA!
 
Mpeni nafasi aongoze kwa namna yake
Ndicho tunataka. Anaposema yeye na mshikaji ni kitu kimoja. Kinachokuja katika fikra za wengi ni kuwa pengine tutaona wimbi jipya la wasiojulikana wakiumiza watu kwa kasi kubwa zaidi.....hata slogani ya kazi iendelee angeipadilisha hata aseme "mwelekeo mpya"
 
Alichelewa kukemea. Tungemsifu ang
Rais Samia amesema siyo afya kwa bunge kuacha kujadili bajeti na kuanza kumlinganisha yeye na hayati Magufuli .

--+
Inasikitisha sana kuona wanapiga ngoma mitandaoni lakini ngoma ile inachezwa Bungeni na mnademka vizuri sana. Mnafanya kazi ya kulinganisha watu badala ya kulinganisha ajenda za Taifa, mnalinganisha Magufuli na Samia nawaambia Magufuli na Samia ni kitu kimoja.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala yenu Bungeni, mijadala yenu haina afya kwa Taifa. Naomba tufanye kazi kama Bunge linavyotakiwa kufanya kazi.

Alichelewa kukemea. Tungemsifu tangu wabunge wachache sijui walitumwa na nani walipoanza kumkashim Hayati Nabii Mfalme JPM ndio tungemuelewa.
 
Rais Samia amesema siyo afya kwa bunge kuacha kujadili bajeti na kuanza kumlinganisha yeye na hayati Magufuli .

--+
Inasikitisha sana kuona wanapiga ngoma mitandaoni lakini ngoma ile inachezwa Bungeni na mnademka vizuri sana. Mnafanya kazi ya kulinganisha watu badala ya kulinganisha ajenda za Taifa, mnalinganisha Magufuli na Samia nawaambia Magufuli na Samia ni kitu kimoja.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala yenu Bungeni, mijadala yenu haina afya kwa Taifa. Naomba tufanye kazi kama Bunge linavyotakiwa kufanya kazi.

Koh! Koh!
 
Back
Top Bottom