Rais Samia Suluhu alitaka Bunge kujadili Bajeti badala ya kumfananisha yeye na Hayati Magufuli

Rais mama Samia Suluhu Hassan, amewachana tena bunge la mheshimiwa Ndugai binge lake halina Afya ikimaanisha ni dhaifu, sasa hii inaonesha ni kiasi ganii mhashimiwa Ndugai ameshindwa kusimamia uhai wa bunge ukilinganisha na wenzake waliopita akina mama ANNA mzee wetu marehemu Sitta na wengineo.

Sasa tunachotaka kuwaambia Mataga acheni kutoa kejeli kwa watu wanaposema ukweli kama Prof. Assad aliposema ukweli tena aliongeza juzi kwa kusema hata watendaji wa serikali baadhi ni dhaifuu kwenye kutoa na kusimamia maamuzi, tujadili hili wadau.
 
Kwenye hotuba yako jana ulipiga tofari, Kuna mashabiki wako a.ka Mashabiki uchwara wanaotaka kuonesha kwamba JPM ni tofauti sana na wewe na kwamba uyaache yote aloyafanya uanze yako tu.

Kwa lughwa nyingine ufute legacy ya Hayati Mapema sana, yaani bila kujali jambo hilo ni jema ama lah. Nia yao ilikuwa ni kuwagawa watanzania walio kuwa karibu na JPM na ikiwzekana uwatenge kabisa. Wewe ndie unaujua ukweli, hatukuchagulii lakini hotuba zako zinaendelea kutibu taratibu.

Mama ni Mama, tofari lako la jana limefanya watu wanune huku mtaani na nikwambie tu wameanza kukugeuka mapema sana. Watu wa kujpendekeza na kujina wao ndio wao.


Mda ni hakimu mkuu sana na mda si mrefu tutajuana tunaokuunga mkono kwa matendo na si kwa maneno.
 
Kwa tume huru ya uchaguzi au hii hii iliyojazwa makada na wanazi wake?
Ukitaka kujua Power ya JPM, fanya jaribu moja tu, utapata jibu.
Jambo lenyewe ni hili:

Chukua picha ya JEMBE(JPM), halafu muweke mtu mwingine yeyote pembeni ya picha ya JPM.

Alika watu wapige kura kuchagua ama picha ya JPM au huyo mtu mwingine. Zoezi hilo lifanyike mchana kutwa. Kisha hesabia kura za kila mmoja. Hapo ndipo utajua JPM ni nani.
 
Mheshimiwa mama Samia ana nafasi kubwa ya kurekebisha yote mabaya yaliyofanywa katika uongozi wa Magufuli, ila anakosea kusema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Mheshimiwa Mbowe ameandika vizuri kwamba, “...kivuli cha Magufuli bado kinamtesa mama Samia...”. Je mama Samia atawezaje kurekebisha makosa ya utawala uliopita ilhali yeye ni kitu kimoja na utawala uliopita? Maneno haya yanamfunga mama Samia kiutendaji.
 
Nadhani kauli alitakiwa kusema ni kwamba JPM na yeye wote ni CCM, na wote wanaongozwa na ilani ya chama waliyoipigia na kuinadi pamoja katika uchaguzi.
 
Ndani ya ccm kuna mtifuano wa wazi kuhusu kuenziwa kwa Magufuli, timu Magufuli wanaona kama Mwendazake haenziwi ipasavyo.

Timu Magufuli wananguvu na mihemiko balaa, wanatamani kila saa na kila dakika atajwe Magufuli, wanatamani wapinzani wasisikilizwe kabisa, wanatamani kila msimamo wa Magufuli uahudiwe na Kila mtu.

Hawaamini kama Mama Samia yuko pamoja nao, hawataki Kundi la Nappe,Makamba, Ridhiwani na wengine wa kufanana hao kuongea maana wanaona kama wanamsiliba mwenda zake.
 
Mama amenifurahisha sana aliposema mradi wa daraja la busisi utaendelea kama kawaida
 
Watanzania ni watu wa ajabu kabisa sijui aliyewaroga nani sasa ulitaka aseme yeye ni kitu kimoja na Mbowe?

Samia si Rais wa kuchaguliwa ni Rais kwa mujibu wa katiba ibara ya 37/5
Article 37, subsection 5 states:
"Where the office of President becomes vacant by reason of death, resignation, loss of electoral qualifications or inability to perform his functions due to physical infirmity…then the Vice-President shall be sworn in and become the President for un expired period."

yupo pale kumalizia kipindi cha miaka 4 kilichobaki utamtenganisha vipi na JPM ? Leo hakuna mradi atakaosema ambao umeanza kuanzia tarehe 19 mwezi 3 siku anaapishwa atataja miradi ambayo alishiriki kuianzisha kama makamu wa Rais na Rais alikuwa JPM

Huwezi kumtengenisha Samia na JPM hata kidogo Samia amekuwa na JPM miaka 6 na majukumu yake kama Makamu wa Rais yanajulikana kikatiba 50,48 vifungu hvyo vinazungumzia Vice-President, his duties and powers

Kama mnaona JPM hafai kukumbukwa kwenye nchii hii subirini Lissu akiwa Rais mpleke marekebisho ya katiba kufuta Urais wa JPM japo Dunia nzima itawaona watu wa ajabu kuwai kuishi kwenye Dunia lakini kusema Samia hasijiushishe na JPM mnachekesha sana tena sana na kuonekana mlivyo mbumbumbu kiakili.
 
Tatizo sio Mama ila tatizo ni mihemuko ya watu waliyokurupuka kwa kuanza kumshobokea Mama kwa sababu ya hasira zao kwa Magufuli, ilikuwa ni akili mbovu kufikiri watamtumia Mama kwenye huo ugomvi wao dhidi ya marehemu au kwamba Mama nae ana hasira na utawala wa Magufuli kama walivyo wao na kusahau kuwa Mama nae alikuwa kwenye utawala huo huo.
 
Mheshimiwa mama Samia ana nafasi kubwa ya kurekebisha yote mabaya yaliyofanywa katika uongozi wa Magufuli, ila anakosea kusema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Mheshimiwa Mbowe ameandika vizuri kwamba, “...kivuli cha Magufuli bado kinamtesa mama Samia...”. Je mama Samia atawezaje kurekebisha makosa ya utawala uliopita ilhali yeye ni kitu kimoja na utawala uliopita? Maneno haya yanamfunga mama Samia kiutendaji.
Maana yake chupa mpya mvinyo uleule
 
Back
Top Bottom