Rais Samia Suluhu alitaka Bunge kujadili Bajeti badala ya kumfananisha yeye na Hayati Magufuli

Njia ya mnafiki utaiona tu
Unapewa za uso halafu unaamka kwa zile zile ngoma unaanza kucheza tena bila soni

Hivi kweli wanashindwa kutofautishwa lugha au wanajua mtu mpaka akufokee na kukutukana ndio ukae kimya?
 
Njia ya mnafiki utaiona tu
Unapewa za uso halafu unaamka kwa zile zile ngoma unaanza kucheza tena bila soni

Hivi kweli wanashindwa kutofautishwa lugha au wanajua mtu mpaka akufokee na kukutukana ndio ukae kimya?

Waache tu wakate viuno huko bungeni ndio washaambiwa sasa
 
Mama anawapoza wafuasi kindakindaki wa Magufuli maana bado wana uchungu sana—She is just being polite hasa ukizingatia 40 ya marehemu bado!
Mtu akikuambia hivi ndivyo nilivyo, muamini.

Mara zote amesema hamna tofauti kati yake na aliyemtangulia. Na ameonyesha kwa vitendo. Mawaziri ni walewale. Watendaji karibu wote ni walewale. Ndege nyingine zinanunuliwa.

Watu wamekamatwa kwa kunywa ulanzi wakati wa msiba. Wengi wa waliobambikiwa kesi bado wako ndani na hamna aliyechukuliwa hatua kwa kuwambakia kesi.

Magazeti bado yamefungiwa. Vyama vya upinzani bado vinazuiwa kufanya mikutano. Mradi wa umeme wa Stieglers ni full steam ahead. Anasema watu wachukue tahadhari dhidi ya Corona lakini mwenyewe na viongozi wenzake hawachukui tahadhari wakiwa nchini.

Awaambiaje kuwa yeye ni kama aliyemtangulia? Inaelekea ni Mbowe peke yake ndie aliyemuamini na bado anamuamini. Awamu ya sita ni muendelezo wa yote ya awamu ya tano. Hamna tofauti. Rais ametuambia na tunatakiwa kumuamini.

Amandla...
 
Haha Bavicha walifikiri wameshinda Uchaguzi.

Hapo wamekumbushwa kuwa awamu hii haitayaacha yale mazuri ya awamu iliyopita,

Kinachofanyika ni uboreshaji tu.

Chama kinachoongoza nchi ni CCM na wala sio Chadema mitandaoni.
 
Ukitaka kujua Power ya JPM, fanya jaribu moja tu, utapata jibu.
Jambo lenyewe ni hili:-
Chukua picha ya JEMBE(JPM), halafu muweke mtu mwingine yeyote pembeni ya picha ya JPM.
Alika watu wapige kura kuchagua ama picha ya JPM au huyo mtu mwingine. Zoezi hilo lifanyike mchana kutwa. Kisha hesabia kura za kila mmoja. Hapo ndipo utajua JPM ni nani.
Tayari anajulikana ni nani, bila kura, ni Mwendazake! Na harudi tena!
 
Japo mama Kuna kipindi alikuwa kama anataka kuyumba naona wamemshika sikio kuwa hawezi kujitenga na JPM hata siku moja watu wanaona na kura za kanda ya ziwa zinaitajika sana mwaka 2025
Kile kikundi kilikuwa kinatest wananchi watareact VP na hiyo move yao? Kazi ilianzia bungeni, wakaanza kugawanyika, comments za wananchi walio wengi, zinaonyesha kupendwa kwa Magu.

Uzuri ni kwamba, legacy ya Magu siyo hivi kitambo, imejengwa kwa miaka mingi, watu tunamjua tangu akiwa waziri mpaka raisi, utawezaje kutudanganya kuhusu Magu? Walikurupuka sana team Msoga.
 
Kwa hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan naye ataisigina Katiba kama alivyokuwa akifanya mwendazake?

Kwa hiyo na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan nayo itakuwa sheria hata kama inapingana na Katiba?
Ameapa kulinda na kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ndio nguzo kuu atakayofuata,lakini kawa Raisi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kupitia chama cha Mapinduzi hivyo hivyo atatekeleza irani ya chama chake.

Lakini kwa kuwa anahitaji pia kuwa kiongozi mkuu wa chama yaani Mwenyekiti, anahitaji ummoja na mshikamano wa wanachama wa CCM.

Raisi SSH anajua anafanya nini,na kwa wakati gani.
 
Ameapa kulinda na kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ndio nguzo kuu atakayofuata,lakini kawa Raisi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kupitia chama cha Mapinduzi hivyo hivyo atatekeleza irani ya chama chake...
Time will tell. Ila kwangu mimi bora nijitayarishe kuwa dissapointed halafu nijikute nilikosea kuliko kujitayarisha kwa furaha halafu nikakuta nilikosea.

Amandla...
 
Hapo simply wabunge wameambiwa waache mipasho, yaani Rais haupendi utoto wanaofanya wakiwa bungeni, au zaidi ni kwamba Rais hataki mbunge yeyote awaye ajipendekeze kwake, yeye anataka wafanye kilichowapeleka bungeni na hili agizo zaidi linamhusu Spika na Naibu wake kama viongozi wa hiyo mipasho.

Mlimuona Ndugai na Makamu wake? Ndugai lazima aone aibu na utani wake wa kijinga kuhusu simba na yanga ndani ya bunge!!
 
Back
Top Bottom