benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi wameipongeza timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya miaka 15 (Karume Boys) kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya CECAFA-U15 yaliyofanyika nchini Uganda.
Karume Boys waliwafunga wenyeji Uganda ambao pia walikuwa mabingwa watetezi kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya mchezo kuisha kwa sare ya goli 1-1
Rais Samia ameandika kupitia mitandao ya kijamii
"Hongereni sana Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 (Karume Boys), kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA U15 2023. Mmetupa heshima kubwa. Nawatakia kila la kheri katika ndoto na safari yenu kwenye mchezo wa soka siku za usoni."
Ukurasa rasmi wa Ikulu ya Zanzibar ulimuonesha Rais Mwinyi akishangilia ushindi huo wakati akifuatilia mchezo
huo ofisini kwake Ikulu ya Mnazi Mmoja-Zanzibar