Zanzibar yatwaa ubingwa wa CECAFA U15. Hongera Karume Boys

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akifurahia bao la nne la mkwaju wa penalti lililoipa ubingwa Zanzibar Karume Boys wa CECAFA kwa vijana chini ya umri wa miaka 15.

Uganda ndio walikuwa mabingwa watetezi wa Kombe hilo.

Rais Dk. Mwinyi alikuwa akifuatilia fainali hiyo ofisini kwake Ikulu Mnazi Mmoja.

Ikulu Zanzibar.

20231116_183424.jpg


#####

ZANZIBAR YATWAA UBINGWA WA CECAFA U15 KWA PENATI

Timu ya Taifa ya Vijana ya Zanzibar 'Karume Boys' imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa CECAFA U15 2023, ambayo ilihusisha Timu za Vijana chini ya umri wa miaka 15.

Karume Boys umebeba Ubingwa Kwa njia ya matuta 4-3 dhidi ya Uganda baada ya sare ya 1-1.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akifurahia bao la nne la mkwaju wa penalti lililoipa ubingwa Zanzibar Karume Boys wa CECAFA kwa vijana chini ya umri wa miaka 15....
Hongera sana Zanzibar katika Soka
 
Hongera sana kwa Karume Boys, Dr.Mwinyi na Wazanzibari wote. Ila ofisi yake haina tofauti sana na chumba changu maalumu cha kujisomea.
 
Haya majina wana yatoa wapi? Bora ingekuwa Dolphin fc 🐬 Au Mnazi mmoja fc au ata mchamba wima fc

Tuna takiwa kubadilika tuachane na zama zile...
 
Hao wachezaji usikute walikuwa ni vijeba, ndiyo maana walifanikiwa kuokota dodo chini ya mti wa mwarobaini.
 
Back
Top Bottom