Waziri Tabia Mwita: Tuna 80% ya Karume Boys Kutwaa Ubingwa CECAFA U15

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Waziri Tabia Mwita: Tuna 80% ya Karume Boys Kutwaa Ubingwa CECAFA U15

"Mimi ni timu zote, ukiona siku inacheza Simba na Yanga utaona nimevaa jezi huku ina Yanga huku ina Simba mimi ni timu zote kwa mujibu wa itifaki, ikitokea nimebadilishwa wizara nikiwa sipo wizara ya michezo nitachagua niko wapi lakini kwa sasa hivi mimi ni timu zote" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri wa Habaari, Vijana, Utamaduni Na Michezo Zanzibar (SMZ)

"Kama mzazi niseme furaha yangu bado haijatulia kwasababu kesho tuna jambo kubwa kidogo la fainali na tuna 75% hadi 80% ya kupata ushindi kiukweli niseme nimefurahi sana" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri wa Habaari, Vijana, Utamaduni Na Michezo Zanzibar (SMZ)

"Karume Boys ni timu ya Taifa na sisi wizara yenye dhamana tunalijua hilo na ndio maana kuna mkono wetu tangu safari ya kuondoka kwao, huko walipo hadi kurudi tena hapa nyumbani, kwahiyo tumeguswa kwasababu moja ya majukumu tuliyopewa ni kusimamia hizi timu za Taifa" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri wa Habaari, Vijana, Utamaduni Na Michezo Zanzibar (SMZ)

"Tunamshukuru Mhe.Rais Dkt Hussein Mwinyi kwa kuahidi kununua kila goli litakalofungwa na vijana wa Karume Boys kwa shilingi milioni 1 kwasababu hatukutegemea. Tumefarijika sana kwasababu inahitaji moyo kufanya haya kwasababu tunajua Mhe.Rais ana mambo mengi lakini ameona pia sekta ya michezo inahitaji sapoti" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri wa Habaari, Vijana, Utamaduni Na Michezo Zanzibar (SMZ)

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Tabia Mwita ameeleza kuwa wao kama wizara wametoa zaidi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya safari na maandalizi ya timu ya vijana ya Zanzibar U15 nchini Uganda kwenye michuano ya CECAFA U15 Boys Championship.

"Marais wetu wote wawili wapo serious kwenye sekta ya michezo jitihada zao wote tunazishuhudia, lakini pia tunachoshukuru hii CECAFA U15 ya mwaka huu imezaa matunda na imezaa matunda kwasababu makocha wetu waliochagua timu wamefanya vizuri" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri wa Habaari, Vijana, Utamaduni Na Michezo Zanzibar (SMZ)
 

Attachments

  • F--_3pKaMAA-B-C.jpg
    F--_3pKaMAA-B-C.jpg
    93.3 KB · Views: 3
  • F-_CtNqaMAAtnMU.jpg
    F-_CtNqaMAAtnMU.jpg
    99.9 KB · Views: 3
  • F-_Ehc-XIAAsCWK.jpg
    F-_Ehc-XIAAsCWK.jpg
    99.7 KB · Views: 3
  • F-_OlOHWIAEc6MK.jpg
    F-_OlOHWIAEc6MK.jpg
    98.4 KB · Views: 3
Tatizo langu lipo sehemu moja tu. Je, umri umezingatiwa kweli kwenye hayo mashindano?
 
Back
Top Bottom