Rais Samia Aizawadia Timu ya Taifa (Zanzibar) ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) Shilingi Milioni 50

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys), Ikulu Tunguu visiwani Zanzibar leo tarehe 25 Novemba, 2023 ameizawadia timu hiyo Shilingi Milioni 50

Rais Samia Ameunga mkono zoezi la kuchangia timu hiyo lililoanzishwa na ZBC ambapo mpaka sasa kuna ahadi ya Shilingi Milioni 90 huku Milioni 40 zikiwa zimeshakusanywa
 
Ni sawa pia wala hatuna neno, hongera zao vijana kwa kupata zawadi nono! Iwe motisha nzuri kwa basi!
 
Nadhani ifike wakati sisi tunaomlipa huyo Rais mtoa Hisani, Tupate Mkeka mzima wa Matumizi, Tunamlipa ngapi na anazifanyia nini kama ni sawa afanye anachofanya (opportunity cost)...,

Unless kama anatumia kwenye mshahara wake (na hapo itakuwa huenda tunamlipa nyingi) au anatoa kwenye urithi (Hapo I have nothing to say na aendelee na moyo wa kutoa)
 
Katiba katiba katiba

Kuanzia kipindi cha magu Hawa Marais wanatoa fedha tu kama wanatoa mifukoni kwao....

Kuna shule juzi tumeonyeshwa watoto wanaandika chini hawana hata ubao, yaani Kuna vitu ukiwaza sana unaweza kufuru
Usiwe MBUMBUMBU sio kila hela inajenga shule.

Wakati wa COVID hela zilipoenda kujenga madarasa mlipinga sasa hivi unainua kidomodomo kudai madarasa
 
Nadhani ifike wakati sisi tunaomlipa huyo Rais mtoa Hisani, Tupate Mkeka mzima wa Matumizi, Tunamlipa ngapi na anazifanyia nini kama ni sawa afanye anachofanya (opportunity cost)...,

Unless kama anatumia kwenye mshahara wake (na hapo itakuwa huenda tunamlipa nyingi) au anatoa kwenye urithi (Hapo I have nothing to say na aendelee na moyo wa kutoa)
Jielimishe kidogo
Kuna Bajeti ya Ofisi ya Rais Ikulu
Na kuna Bajeti ya Ofisi Binafsi ya Rais (OBR)
Na katika hizi zote bajeti ya CSR ipo, so kitulize
 
Jielimishe kidogo
Kuna Bajeti ya Ofisi ya Rais Ikulu
Na kuna Bajeti ya Ofisi Binafsi ya Rais (OBR)
Na katika hizi zote bajeti ya CSR ipo, so kitulize
Rudia nilichosema hapo Juu au hata kusoma haujui ?!!!!! Narudi tena sentensi itakayokujibu uliyosema hapo juu...

Kama Bajeti hizo zipo na zinaweza kutumika zinavyotumika basi sisi kama walipo Kodi tunalipa nyingi na zipunguzwe.... (kuna ugumu wa kuelewa hilo suala)?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys), Ikulu Tunguu visiwani Zanzibar leo tarehe 25 Novemba, 2023 ameizawadia timu hiyo Shilingi Milioni 50

Rais Samia Ameunga mkono zoezi la kuchangia timu hiyo lililoanzishwa na ZBC ambapo mpaka sasa kuna ahadi ya Shilingi Milioni 90 huku Milioni 40 zikiwa zimeshakusanywa
Zimetoka kwenye mfuko upi ?
 
Wakati huo huo timu ya Netbol ya Taifa imeshindwa kwenda kam sikosei Zambia sijui Msumbiji kwa kukosa tiketi za milion 20. Hawa viongozi mbona hawajui kupriotize vitu ?

Ajabu sana ile taarifa ilinisikitisha sana team kukosa hela na kwa sasa Tanzania mpira ndo unaitambulisha nchi kuliko vingine!
 
Back
Top Bottom