Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la kushuhudia ufungaji wa lango la handaki mchepuko (diversion tunnel) ili kuruhusu maji kuanza kujaa katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere litakalofanyika siku ya Alhamis, 22 Disemba 2022.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika eneo la mradi wa umeme wa Mto Rufiji, Waziri wa Nishati, January Makamba amesema mradi huo una hatua kubwa mbili ambazo zina hadhi ya kushuhudiwa, hatua ya kwanza ni kufunga lango la njia ya mchepusho wa maji na ya pili ni kuwasha mitambo ya kufua umeme.
"Kwa jumla hadi leo (Disemba 18, 2022) mradi huu umefikia hatua ya 78%, ni hatua kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
“Tumemaliza kujenga tuta, barabara, tumemaliza kujenga nyumba za wafanyakazi kwa hiyo kuna mafanikio katika kipindi chote, sasa tumefikia kwenye mafanikio makubwa tangu tuanze ujenzi wa mradi huu na yenyewe ni kujaza maji kwenye bwawa, kazi ya kujenga handaki la kuchepusha maji ilifanyika miaka mitatu iliyopita na handaki hilo lina urefu wa mita 700 na ujenzi uligharimu Tsh. Bilioni 235.”
Waziri Makamba amesema kutokana na umuhimu wa hatua hiyo ya mradi ulipofikia wakati wa uzinduzi Rais atabonyeza kitufe ambacho kitashusha geti la kuziba handaki lilikuwa linachepusha maji na rasmi maji yataanza kujaa kwenye bwawa.
Ameongeza kuwa Shughuli hiyo itauzuliwa na watu takribani 2,000 wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na viongozi wengine kama Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mawaziri, Makatibu Wakuu, wakuu wa Mikoa na Wilaya zinazozunguka Bonde la Mto Rufiji, viongozi wa dini, Viongozi wa Chama na Wananchi
Pia Serikali ya Misri ambapo ndipo wanatoka wakandarasi wanaojenga mradi huo, mawaziri, viongozi wa Serikali pamoja na Vyombo vya Habari vya nchi hiyo watahudhuria wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Nchini Misri.
Akizungumzia faida za mradi huo Makamba amesema ndani ya Serikali mradi huu ni mpana zaidi na utasaidia pia katika masuala ya Kilimo chini ya Mto Rufiji, uvuvi, kuondoa mafuriko, Upatikanaji wa huduma za maji wa uhakika kwa Jiji la Dar es Salaam, Utalii, miundombinu na usafirishaji pamoja na kupata umeme wa uhakika.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande ameeleza kuwa inakadiriwa kwamba misimu miwili ya mvua itaweza kufanya bwawa Hilo la Julius Nyerere kujaa maji, hivyo zinatazamiwa mvua za masika Machi 2023 na 2024 kuweza kujaza Bwawa hilo.
Mradi wa kufua umeme kwa njia ya maji wa Julius Nyerere unakadiriwa kuzalisha Megawati 2115, ulianza kujengwa mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika Juni 2024 na umegharimu kiasi cha Shilingi Trilioni 6.5 ukiwa umebakisha 22% kukamilika.
Chanzo: Beatrice Sanga-MAELEZO