SI KWELI Rais Samia kukaa mapumziko ya Eda siku 90

SI KWELI Rais Samia kukaa mapumziko ya Eda siku 90

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo na picha inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa ni taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi. Picha hiyo inadai kuwa, kufuatia msiba wa mume wake, Mzee Hafidh Ameir Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahirisha mapumziko ya kifamilia na shughuli nyingine kwa muda wa siku 90 kuanzia Septemba 7, 2026.

Taarifa hiyo pia inadai kuwa shughuli zote za Serikali zitasimamiwa na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba na sheria, huku ikieleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka husika endapo zitahitajika.
JAMIICHECK MEI 2026.jpg
 
Tunachokijua
Ufuatiliaji kupitia ukurasa rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali umebaini kuwa taarifa hiyo potoshi . Kupitia ukurasa huo, wananchi wametakiwa kuipuuzia taarifa hiyo, ambayo imeelezwa kuwa ni ya uzushi na imetengenezwa kwa lengo la kupotosha.

Aidha, wananchi wamesisitizwa kuendelea kufuatilia taarifa sahihi kupitia vyanzo rasmi, ikiwemo tovuti ya Idara ya Habari – MAELEZO, www.maelezo.go.tz, pamoja na akaunti rasmi za Idara hiyo kwenye mitandao ya kijamii, zikiwemo Msemaji Mkuu wa Serikali na Maelezo News.

Mbali na kukanushwa kwa taarifa hiyo na mamlaka husika, uchunguzi wa picha hiyo umebaini pia kuwa ina makosa ya kiuandishi na haifuati kikamilifu muundo na mtiririko unaotarajiwa katika taarifa rasmi za Serikali nchini Tanzania

Similar Discussions

Back
Top Bottom