SI KWELI Rais samia: Natamani muda wangu uishe

SI KWELI Rais samia: Natamani muda wangu uishe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #2
View Source #2
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la usambazaji wa nukuu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zinazodaiwa kutolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Mojawapo ya nukuu hizo, iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook, inamdai Rais Samia amesema: "Natamani muda wangu uishe."

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa kupitia vyanzo mbalimbali vya mtandaoni umebaini kuwa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuwa Rais Samia aliwahi kutoa kauli hiyo, iwe katika hotuba, mahojiano, taarifa rasmi au kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Aidha, ukaguzi wa hotuba na taarifa rasmi zinazochapishwa kupitia kurasa za mawasiliano za Ikulu ya Tanzania haukubaini sehemu yoyote ambayo Rais Samia amesema anatamani muda wake wa uongozi uishe.

Kutokana na matokeo hayo, hakuna ushahidi unaothibitisha uhalali wa nukuu hiyo. Hivyo, nukuu hiyo imebuniwa na kusambazwa na wapotoshaji kwa lengo la kupotosha umma.
SAMIA JPG.jpg
 
Tunachokijua
Julai 20, 2026 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alikuwa Kigoma akiweka jiwe la ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme mkoani humo pamoja na uzinduzi wa meli za mizigo.

Madai

Kupitia mitandao ya kijamii kumeibuka nukuu inayodaiwa kuwa imetolewa na kiongozi huyo akisema kuwa "Natamani muda wangu uishe"

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatila na kujiridhisha kuwa nukuu hiyo si ya kweli na haijatolewa na Rais Samia. Hakuna kumbukumbu zozote kuonesha kuwa Rais Samia alitoa nukuu hiyo.

Katika hotuba yake aliyoitoa Kigoma, Rais Samia alizungumzia umuhimu wa reli hiyo kwa taifa na kuwataka wananchi watunze amani na kudumisha umoja na mshikamano. Rejelea hotuba hiyo hapa. Sambamba na hilo ufuatiliaji zaidi
Back
Top Bottom