GE2025 Rais Samia, hii ahadi ya kuondoa tatizo la umeme mpaka lini?

GE2025 Rais Samia, hii ahadi ya kuondoa tatizo la umeme mpaka lini?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
580
Moja kati ya mambo yanayokera katika nchi hii ni changamoto ya kukatika kwa umeme.

Nakumbuka nikiwa kule kusini mwaka jana, nikiwa kwenye hotel Moja, umeme ukikatika ghafla. Pembe yangu kulikuwa na wazungu wanne wakipata vinywaji. Mara umeme ulipokatika walisikika wakisema, " welcome to Tanzania".

Wenye kuelewa wanaelewa wazungu hao walimaanisha Nini lakini kwa kifupi ni kauli ya kejeli, kwamba, tatizo la kukatika kwa umeme hapa nchini ni la kawaida ni sawa na utambulisho wa nchi yetu.

Ja ajabu, kushangaza na kusikitisha, kila baada ya miaka mitano, CCM ambao wameshindwa kutatua tatizo hili kwa miaka 60 baada ya Uhuru, husimama kwenye majukumu ya Kampeni wakiomba kura Kwa ahadi ya kumaliza tatizo Hilo.

Nimemsikia Samia Suluhu Hassan akisema eti akichaguliwa atamaliza tatizo la umeme na kwamba ziada itauzwa nchini Zambia.

Ahadi zile zile kila baada ya miaka mitano huku kwetu tumechoka!

Kwa Nini hamkumaliza changamoto hii ndani ya miaka mitano iliyopita ili.mwaka huu mje na jipya kuhusu umeme?

Ifike mahali mseme tu kwamba changamoto ya umeme ni mfupa uliomshinda fisi!
 
Kwani si tunasema mama hatumdai mbona yeye anasema tunamdai mbona mwanichanganya ine
 
Sarakasi za walioshindwa hata ukiwa na kiwango kiduchu sana cha uelewa, hutopata shida kujua ccm ni waongo na matapeli
 
Back
Top Bottom