Rais Kikwete azuiliwa kuingia Denmark

Rais Kikwete azuiliwa kuingia Denmark

Mbilikimo wa fikra ni wewe uliyekuja na uzushi na kupindua pindua maneno. Umeulizwa swali na Pasco ukapinduwa pinduwa.

Unajuwa maana ya "kuzuiliwa kuingia"? amezuiliwa airport ipi ya Denmark au mpaka upi wa Denmark?

Hivi unafikiri watu wote humu ni mapunguani kama wewe?

Watakao-kuunga mkono kwenye huu upotoshaji ni mapunguani wenzako tu, wasiojielewa kama wewe.

Wewe ndiyo wale wale "viwanda vya uongo".

Punguani wahed.

Pinduwa=Pindua
Unajuwa=Unajua
Udhaifu wako uko kwenye matumizi ya "w"!
Shuleni ulikuwa mtoro wewe
 
Ifike mahali bunge lihoji matumizi mabaya ya IKULU na safari za mheshimiwa Rais, ni fedheha na aibu sana!!!!

Lihoji wakati wanabembeleza awakubalie yale malipo ya kutisha ya kiinua mgongo?
 
Kikwete anatisha!

Hata uzunguni wamemuogopa? Kuwa anaweza kuwa kichocheo cha wazungu kumpigia kura amtakae yeye.

Kwa hakika hii ni sifa kubwa sana na ni historia kama ni kweli.
HA, wewe wamemuogopa na kweli kawatisha maana ni mwenyekiti wa chama cha mafisadi waliokubuhu na wanaosifika kwa uchakachuaji, jamaa wahataki kuambukizwa ujinga, asijewafunza kuiba hela za kununua kura kuingia ikulu, amefukuzwa ni aibu.
 
Ifike mahali bunge lihoji matumizi mabaya ya IKULU na safari za mheshimiwa Rais, ni fedheha na aibu sana!!!!
Kwani nani kakudanganya kuwa safari za rais ni matumizi mabaya ya Ikulu?
 
Ndiyo maana kila kukicha kila mmoja anataka kuwa Rais, kwa sababu urais hapa Tanzania umefanywa kuwa "RAHISI"
Kwa kawaida wengi wanatamani kuwa Marais. Ila anayejaaliwa na Mungu ni mmoja tu. babu Slaa pamoja na umri wake kwenda anatamani kuwa Mkuu wa nchi. Mbowe pamoja na kutojua kusoma na kuandika anatamani kwenda Ikulu
 
Rais Wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete amezuiliwa kuingia Denmark kutokana na vuguvugu la uchaguzi nchini humo baada ya kubainika kuwepo kwake kungempa nafasi zaidi ya kuonekana waziri mkuu Wa sasa kitendo kilichotafsirika Kama kumpigia kampeni.

RAIS Jakaya Kikwete ambaye amekuwa katika ziara za kuaga washirika wa mandeleo katika nchi za Scandinavia, amekataliwa kuingia Denmark kwa madai kuwa ziara yake itatumika kisiasa kumnufaisha Waziri Mkuu wa sasa wa Denmark.

Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wiki ijayo. Zuio hilo limekuja baada ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kudai kuwa ziara hiyo ingetumika kumnufaisha Waziri Mkuu aliyepo kwa kumpa muda wa ziada mbele ya vyombo hivyo wakati huu wa kampeni.

Vyama vyote vya kisiasa vinapata muda sawa mbele ya vyombo vya habari na kwa hiyo uwepo wa Rais Kikwete nchini Denmark ungesababsha Waziri Mkuu aliyepo madarani kuonekana mara nyingi akimpokea mgeni wake.

Rais Kikwete hivi karibuni amefanya ziara katika nchi za Finland, Sweden, Uholanzi ikiwa ni sehemu ya kuaga kutokana na muda wake wa kuwa madarakani kufikia ukingoni.

MY TAKE:
Vyombo vya habari hapa kwetu vijifunze kutoka kwa Wenzetu viache ushabiki na viweke mizani sawa kwa wagombea na vyama vyote.....
Watanzania wenzangu tujisifu kupata rais makini kiasi hiki.

Kama Tume ya Uchaguzi ya Denmark imehofia kuwa rais wetu Kikwete akiingia Denmark kipindi hiki cha uchaguzi basi anaweza kusababisha raia wa Denmark wampigie kura mgombea ambaye atakuwa na rais Kikwete.

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Kikwete.
 
Nashangaa amewaambia watanganyika waishio Finland kuwa kutakua na kura ya maoni na uchaguzi mkuu wakati hapa nyumbani hawatuambii hayo hasa kuhusu katiba mpya iliyotafuna mabilioni ya shilingi!!!!

Wewe inaonesha umelala usingizi. Mambo ya kila siku hayajuwi?

Hivi ni Mtanzania yupi zaidi ya alie usingizini asiyeelewa zoezi la BVR linaloendelea nchi nzima hivi sasa? Ulifikiri ni la nini lile?

Amma kwa hakika kwa watu kama wewe, Tanzania tu safari ndefu ya kwenda.

Punguani wahed.
 
vyombo vya habari venyewe haviwezi kubeba jambo hili kwani vyombo vyote vinaendeshwa kwa maslahi fulani.

wapo wafanya biashara sasa mgombea mmoja akilipia mda arushwe na mwingine hajalipia je ufanyeje? ukatae fedha ya aliyelipia au umpe mda bure ambaye hajalipia.

lakini vipo vyombo vya umma ambavyo kimsingi vilitakiwa kufanya hivyo lakini sisi wenyewe tunasapoti makundi katika kutafuta uraisi na baada ya kundi kupata uraisi wanagawana nyadhifa za umma. sasa mtu huyu aliyewekwa na kundi fulani na kundi hilo ndilo linaloweza kumbakiza na likiingia kundi jingine anatolewa afanyeje?

hivyo jambo hili haliwezi kubebwa na vyombo vya habari bali jamii nzima ndiyo inatakiwa kubeba jambo hili kwa maana linagusa maslahi ya jamii moja kwa moja.

kwa nini linagusa maslahi ya jamiii ni kutokana na ukweli kwamba jamii inahitaji viongozi bora na wananchi wanatakiwa kuwapa wanaojitokeza uwanja sawa kuwasikiliza na kubaini viongozi wanaowafaa ni kina nani?

mfano kabla ya wale waliotangaza nia kufanya hivyo watu walikuwa na majina yao wakitaja nifulani ni fulani na haya yalitokana na popularity zao huko nyuma. yaani mtu aliyewahi kushika nyadhifa fulani au mzazi wake ilimpa jina la kudhaniwa anafaa kuwa raisi.

na wale ambao hawakuwahi kupata kutokea kwenye vyombo vya habari mara kwa mara walidhauriwa

lakini baada ya kupata nafasi za kuongea kwenye vyombo vya habari mtizamo wa wananchi kwa wagombea umebadilika kwa maana wapo waliojiweka juu kwa kuonekana kutambua lile viongozi wanatakiwa kufanya huku baadhi ya wale waliokuwa wakipewa nafasi kubwa kuonekana wanategemea umaarufu wao au wazazi wao lakini hawana mipango yoyote ya uongozi.

kwa uzoefu huo unaweza kuona kuwa kama wagombea hawa wasingepata kuonekana kupitia vyombo vya habari bado tungewatathmini kwa kutumia mazoea na uwezekano wa kupata pumba badala ya kupata mchele.

upo uwezekano wa watu wasio na sifa kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kupitia vyombo vya habari na watu wenye sifa kukosa nafasi na sikuzote huwezi kumlinganisha uliyemsikiliza na usiyemsikiliza kwa maana usiyemsikia utamtathmini kwa background yake tu.

dawa hapa ni tuwe na sheria za uchaguzi zinatoa uwanja sawa kwa wagombea .

Rais Wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete amezuiliwa kuingia Denmark kutokana na vuguvugu la uchaguzi nchini humo baada ya kubainika kuwepo kwake kungempa nafasi zaidi ya kuonekana waziri mkuu Wa sasa kitendo kilichotafsirika Kama kumpigia kampeni.

RAIS Jakaya Kikwete ambaye amekuwa katika ziara za kuaga washirika wa mandeleo katika nchi za Scandinavia, amekataliwa kuingia Denmark kwa madai kuwa ziara yake itatumika kisiasa kumnufaisha Waziri Mkuu wa sasa wa Denmark.

Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wiki ijayo. Zuio hilo limekuja baada ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kudai kuwa ziara hiyo ingetumika kumnufaisha Waziri Mkuu aliyepo kwa kumpa muda wa ziada mbele ya vyombo hivyo wakati huu wa kampeni.

Vyama vyote vya kisiasa vinapata muda sawa mbele ya vyombo vya habari na kwa hiyo uwepo wa Rais Kikwete nchini Denmark ungesababsha Waziri Mkuu aliyepo madarani kuonekana mara nyingi akimpokea mgeni wake.

Rais Kikwete hivi karibuni amefanya ziara katika nchi za Finland, Sweden, Uholanzi ikiwa ni sehemu ya kuaga kutokana na muda wake wa kuwa madarakani kufikia ukingoni.

MY TAKE:
Vyombo vya habari hapa kwetu vijifunze kutoka kwa Wenzetu viache ushabiki na viweke mizani sawa kwa wagombea na vyama vyote.....
 
Kwani nani kakudanganya kuwa safari za rais ni matumizi mabaya ya Ikulu?
Umesoma kilichoandikwa au umekurupushwa usingizini?
Matumizi mabaya ya ikulu NA safari za rais, kutumia ikulu vibaya ni pamoja na kufanya matumizi yasiyo na lazima, mfano ni hizo safari zake.
 
Nadhani wewe ndiye uliyesomea ujinga!!!
JK kama mwenyekiti atakayeongoza vikao vya maamuzi lazima apitie hayo mafaili ile awe na uelewa mkubwa kabla maamuzi kutolewa!! Haiwezekani mambo yaliyomo katika mafaili yamchukuwe by surprise!!!!!

Mafaili gani wewe? na hao watangaza kura wote wanajulikana na wengi kama si wote yeye ndiyo bosi wao kwa sasa, labda atokee asiyejulikana.

Hata iwe kuna mafaili, hivi mnafikiri siku hizi bado watu wanakimbizana na mafaili ya makaratasi? Ofisi sasa hivi ni popote.

Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
 
MY TAKE:
Vyombo vya habari hapa kwetu vijifunze kutoka kwa Wenzetu viache ushabiki na viweke mizani sawa kwa wagombea na vyama vyote.....
Waandishi wa Bongo ni famba for the most part, mimi nimeshangaa kumuona Ephraim Kibonde eti mshereheshaji wa tafrija ya Lowassa ya kutangaza nia akichombeza "safari ya matumani oyeee!" sikuamini. Nikajiuliza hivi waandishi wa Bongo wana wazimu?

Nchi za watu huyo Kibonde kesho yake angepoteza half of his audience ambao hawamfagilii Lowassa. Lakini Tanzania hakuna ratings, vipindi vinajiendea endea tu, waandishi wanafanya lolote. Huwezi kumlipa mwandishi wa BBC, hata mamilioni ya dola, aje kuwa mshereheshaji wa vi shughuli vyako binafsi vya kisiasa, ni mwiko wa maadili ya uandishi, never!

Pinduwa=Pindua
Unajuwa=Unajua
Udhaifu wako uko kwenye matumizi ya "w"!
Shuleni ulikuwa mtoro wewe

Kwi kwi kwi teh teh teh.

Sasa hayo maneno yaandike kama ulivyoandika wewe halafu tamka mara tatu kwa sauti huku unajisikiliza, jibu utalopata. Ucheke tu wewe mweyewe, huna haja ya kunielezea, nnalijuwa.
 
Back
Top Bottom