Rais Kikwete azuiliwa kuingia Denmark

Rais Kikwete azuiliwa kuingia Denmark

Lusungo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
29,515
Reaction score
42,646
Rais Wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete amezuiliwa kuingia Denmark kutokana na vuguvugu la uchaguzi nchini humo baada ya kubainika kuwepo kwake kungempa nafasi zaidi ya kuonekana waziri mkuu Wa sasa kitendo kilichotafsirika Kama kumpigia kampeni.

RAIS Jakaya Kikwete ambaye amekuwa katika ziara za kuaga washirika wa mandeleo katika nchi za Scandinavia, amekataliwa kuingia Denmark kwa madai kuwa ziara yake itatumika kisiasa kumnufaisha Waziri Mkuu wa sasa wa Denmark.

Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wiki ijayo. Zuio hilo limekuja baada ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kudai kuwa ziara hiyo ingetumika kumnufaisha Waziri Mkuu aliyepo kwa kumpa muda wa ziada mbele ya vyombo hivyo wakati huu wa kampeni.

Vyama vyote vya kisiasa vinapata muda sawa mbele ya vyombo vya habari na kwa hiyo uwepo wa Rais Kikwete nchini Denmark ungesababsha Waziri Mkuu aliyepo madarani kuonekana mara nyingi akimpokea mgeni wake.

Rais Kikwete hivi karibuni amefanya ziara katika nchi za Finland, Sweden, Uholanzi ikiwa ni sehemu ya kuaga kutokana na muda wake wa kuwa madarakani kufikia ukingoni.


MY TAKE:
Vyombo vya habari hapa kwetu vijifunze kutoka kwa Wenzetu viache ushabiki na viweke mizani sawa kwa wagombea na vyama vyote.....
 
Huku watangaza nia wanaleta viongozi wa nchi jirani.

Si unakumbuka pia çcm waliwahi kumleta Mchina jukwaani


Aisee nimevutiwa Sana na demokrasia za Wenzetu zilivyo na usawa....

ingekua hapa waziri mkuu au Rais aliyepo madarakani ambaye naye ni mgombea atafanya manyanga yote kwa kofia ya urais licha ya kwamba inampa favour kuliko wenzie....

Angalia TBC1 inavyotoa airtime kwa CCM kuliko vyama vingine ingawa inaendeshwa kwa kodi zetu sote....
 
Inaelekea hakua nao, labda alimpigia cm akiwa airport kuwa kazuiwa, na akaambiwa ni sawa kabisa. Uswahili hauna mipaka ukikozoea basi utaambatana nao tu.

Mmh haaatariii. . . . (kwa sauti ya tangazo la Ndorrrrrrrooobo)
 
Mkuu Rais Wa nchi halazimiki kuwa na mwaliko pia ziara hii ni yeye ndo kajipeleka ati kuwaaga wahisani wetu....So hakuitwa kaenda mwenyewe kwa mapenzi yake.....

Danh yaweza kuwa. . . . . maswali mengi kuliko majibu
 
Back
Top Bottom