Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,622
Mtu ukiwa hujui kitu fulani, ni mjinga!, mtu kuwa mjinga sio kosa, kwasababu kutokujua kitu fulani sio kosa, ukiisha julishwa, ujinga unakutoka unakuwa mwerevu.Acha kuchekesha mkuu!
Zanzibar siyo nchi wakati ina raia wake, Bunge lake na mawaziri wake?
Zanzibar siyo nchi wakati ina wimbo wake wa Taifa?
Zanzibar siyo nchi wakati ina bendera yake?
Zanzibar siyo nchi wakati hata plate namba za magari ya huko ni tofauti na ya magari ya Tanganyika?
Zanzibar siyo nchi Mtanganyika hawezi kuvusha mzigo bila kutozwa Kodi "mpakani"?
Zanzibar siyo nchi wakati Mtanganyika hawezi kuendesha gari huko bila kibali maalum?
Zanzibar siyo nchi wakati Sheria zozote zitakazotungwa Tanganyika hazina mamlaka Zanzibar mpaka zitakaporidhiwa na Bunge la Zanzibar?
Zanzibar siyo nchi? How?
Wewe unaijua Zanzibar kuwazidi Wazanzibar ambao kote waendako wamekuwa wakijitambilisha kuwa nchi yao ni Zanzibar?
Ili nchi kuwa taifa, sio eneo, sio rais, sio bendera, sio wimbo wa taifa, nchi kuwa taifa ni kitu kinachoitwa sovereignty, dola!, Zanzibar haina sovereignty, sio dola!. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndio yenye sovereignty, yenye dola, yenye vyombo vya dola, yenye sarafu, Zanzibar ni jina tuu, la nchi lakini sio nchi, na rais wa Zanzibar ni rais jina tuu wa sehemu inayoitwa Zanzibar lakini kimataifa sio rais, rais ni mmoja tuu, rais wa JMT na nchi ni moja tuu, JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT!.
P