Kwanini raia wa tanganyika hagombei urais wa zanzibar kama ilivyo kwa raia wa zanzibar kugombea urais wa tanzania?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau nawasabahi.Baada ya TANGANYIKA na ZANZIBAR kuungana Nchi ya TANZANIA ikapatikana na Nchi ya ZANZIBAR ikaendelea kuwepo ikiwa na Bendera na RAIS WAKE lakini Nchi ya TANGANYIKA IKAFA .
Katika UCHAGUZI MKUU wa kumpata RAIS wa TANZANIA tumewahi kuwashuhudia Mzee Mwinyi akiwa Mzanzibari akawa Rais wa Tanzania vile vile Rais Samia akiwa mzanzibari akawa Rais wa Tanzania
Ili KUIMARISHA Muungano wetu kwanini Watanganyika nao WASIGOMBEE URAIS wa ZANZIBAR kama ilivyo kwa URAIS wa TANZANIA?
Kufanya hivi kutaimarisha Muungano wetu kinyume Chake NCHI ya TANGANYIKA IRUDISHWE ili TANGANYIKA iwe na RAIS WAKE kama ilivyo ZANZIBAR na RAIS wa TANZANIA apatikane kutoka Nchi ya ZANZIBAR au Nchi ya TANGANYIKA ili awe RAIS wa TANZANIA
 
Back
Top Bottom