mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
612
1,045
Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

👉🏾 Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu. (Sikiliza zaidi)

👉🏾 Ukomo hauwekwi kwenye IGA, bali kwenye mikataba ya chini (Projects Agreements). (Sikiliza Zaidi)

Profesa Assad ametoa majibu mazuri kabisa, na huyu ndio Profesa wa kweli sasa, sio wale wengine akina Tibaijuka na Shivji, wachumia tumbo tu, Sikilizeni nondo kutoka kwa Prof.

a1ee29f0-f118-43c5-b807-6eb666a4c66a.jpg

c761bb55-10a9-454a-92b1-ad2883ee9cbf.jpg

718c30d8-9568-44b1-b8dd-5a1d5fb39c54.jpg

03a803aa-d4cc-43de-9197-eb9f43633652.jpg



Prof. Assad: Kuongeza kodi hakusaidii pato la Nchi
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema Nchi zilizofanikiwa sio ambazo zilifanikiwa kuongeza kodi.

Akizungumza katika mahojiano na Channel Ten, Profesa Assad amesema “Kwa mfano kiwango cha Kodi ya Kampuni Nchini ni 30%, hicho ni kiwango kikubwa sana, Taifa kama Ireland ni moja ya Nchi zilizovutia wawekezaji wengi Ulaya, kiwango chao cha Kodi ni 18%.”

Ameongeza kuwa haungi mkono kupanda kwa kodi kwa kuwa ikishushwa makusanyo yake yatapanda na kusaidia Nchi.


Prof. Assad: Mamlaka zishiriki kukuza wafanyabiashara wadogo sio kusubiri mpaka wakue
“Tuwafundishe watu umuhimu wa uwekaji wa hesabu za fedha, si kwa sababu ya kukusanya kodi, akiweka hesabu zake vizuri miaka mitano sita atahitaji mkopo wa benki, baada ya hapo atakata leseni na tutatoa kodi kidogokidogo,” - Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Profesa Mussa Assad.

PROF. ASSAD: MKATABA WA BANDARI UNAHUSU HAKI ZA ARDHI SIO UMILIKI
Akitoa maoni kuhusu uwekezaji wa DP World katika Bandari, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Profesa Mussa Assad amesema tatizo ni dhana ambazo si nzuri kufikiri kuwa wawekezaji watafanya vitu ambavyo havifai pamoja na watu ambao sio wataalam husika kulisemea jambo hilo.

Akizungumza katika mahojiano na Channel Ten, amesema “Kuna wataalam wa uwekezaji wakiwemo Wanasheria wa Uwekezaji japo ni wachache lakini sisi tunawasikiliza Wanasheria wa Kodi, Wanasheria za Familia, Wanasheria wa mambo ya kampuni ambao ndio wameingia katika maeneo ambayo hayana tija na kusababisha dhana mbaya.”

Ameongeza “Watu wengi si wataalam wa uwekezaji, kipengele kinachozungumziwa katika mkataba ni Haki za Ardhi, sio umiliki, wanachomaanisha ni haki ya utumiaji lakini mmiliki ataendelea kubaki Shirika la Bandari, kuhusu suala la ukomo wanaweza kuweka hata miaka 25 au 30 basi ili watu wakafurahi.”

 
Kwahiyo tulipata uhuru tukiwa hatuwezi kujiendesha wenyewe sasa tumewapata watu wenye akili watulee!

Huu ni ujinga, miaka yote tumeshindwa kusomesha watu wetu leo tuwe vibarua wa wageni na tunalichekelea jambo hilo!

Tutakuja ingia mkataba na waarabu watuendeshee bunge letu maana nalo limetushinda tunaliendesha kama wafugaji wako mnadani.
 
Ni kweli kabisa hakuna palipoandikwa inauzwa lakini pia hakuna palipoandikwa inakodishwa wala kupangishwa hivyo basi.

Kama haiuzwi
Kama haikodishwi
Kama haipangishwi

Maana yake ni moja tu inatolewa bure...

Zaidi Assad naye anataka kugeuka mchumia tumbo.

Maana yeye anazungumzia bandari moja tu wakati IGA inasema bandari zote Tanzania na miundombinu yake.

Mwambie kachelewa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabisa hakuna palipoandikwa inauzwa lakini pia hakuna palipoandikwa inakodishwa wala kupangishwa hivyo basi
Kama haiuzwi
Kama haikodishwi
Kama haipangishwi
Maana yake ni moja tuu inatolewa bure... Zaidi Assad naye anataka kugeuka mcbumbia tumbo.. Maana yeye anazungumzia bandari moja tuu wakati IGA inasema bandari zote Tanzania na miundombinu yake..
Mwambie kachelewa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
ACHA UNAFIKI...humkubali kwakuwa alikuwa anasema kitu usichotaka kukisikia...ila kwasasa AMESEMA UNACHOPENDA SIKIO LAKO KUKISIKIA NDIO UNAJIFANYA KUMBARIKI...AISEE UNAFIKI MBAYA SANA...
Kitu gani ambacho sikupenda kusikia? Taja nikudadafulie
 
Back
Top Bottom