Prof. Mussa Assad atoa maoni yake kuhusu Ripoti ya CAG, asikitishwa na yanayoendelea

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,720
218,271
Profesa Mussa Assad ameonyesha masikitiko yake kuhusiana na wezi wa mali ya umma wanaochekewa.

Mussa Assad aliyewahi kuhudumu kwenye nafasi ya CAG kwa mafanikio , na baadaye kuondolewa kinyume cha Katiba na John Magufuli aliyekasirishwa na kufichuliwa ubadhirifu wa kutisha wa Serikali yake, ni miongoni mwa Watanzania wachache makini sana.

Akihojiwa na Azam TV, hasa kwenye hatua za kuchukua ili kudhibiti wizi kwenye Taasisi za serikali, amesema kwamba, ziko njia mbili za haraka ambazo zaweza kuchukuliwa, mosi ametaja ni ya kuwajibisha mtu binafsi, kwamba mkurugenzi wa shirika akatwe mshahara kwa kiasi fulani kila mwezi na iwe kwa kuongezeka kila mwezi ili baada ya miezi kadhaa awe hana mshahara kabisa, anadai kwa adhabu ya namna hii viongozi wa mashirika watawajibika ili kulinda mishahara yao.

Jambo la pili alilolitaja ni kwa serikali kuwajibisha moja kwa moja wajumbe wa bodi za mashirika kwa njia itakayooneka inafaa ili wasizembee kwenye usimamizi.

Prof. Assad amesema mengi sana mazuri ambayo si rahisi kuyaweka yote hapa.

Chanzo: Azam TV
 
Ila hatujiulizi hao viongozi wa mashirika ya umma wanapatikanaje.

Nawafaham watoto wa viongozi wengi ni wafanyakaz kwenye hayo mashirika, walipataje kazi only God knows.

Lingine ni compliancy ya wafanyakazi wa hiz taasis.. so relaxed and dumbs you can't belive....
Hasara iwe ya wizi au utendaji mbovu haitokaa iondoke serikalini... sio leo wala kesho wala keshokutwa...

Hapa hata kujadili ni kupoteza tu muda.
 
Jana Tundu Lissu alirejea nchini kimya kimya bila mapokezi wala maandamano ya misafara!

Na hapo nikajiuliza,ilikuwa na tija gani pale chama chake kilipompokea awali kwa kuandaa kampeni na maandalizi ya mapokezi kwa kutumia pesa za walipa kodi wa nchi hii.

Kwa jambo lisilo na tija kwa hao wananchi?
 
Nawafaham watoto wa viongozi wengi ni wafanyakaz kwenye hayo mashirika, walipataje kazi only God knows...
Hapa tunajifunza jambo moja, kumbe chanzo cha wizi na uzembe huko serikalini ni "connection", watu wanapewa kazi kwa kuangaliana sura, matokeo yake hata kama mhusika akija kuharibu, hakuna wakumshughulikia, wanaoneana aibu na kufichiana maovu.

Pamoja na yote, kama Rais [mamlaka ya uteuzi] akiamua kuwa serious, ana uwezo mkubwa wa kuondoa huu ujinga, anatakiwa kuwashughulikia personally wote wanaoharibu kwenye mashirika yao, ili nao wasiwaonee aibu wale wasaidizi wao watakaowaharibia kazi.

Lakini kama Rais akiamua kuyakalia kimya haya maovu, nae anakuwa ni sehemu ya tatizo, anakuwa amekubali kuingizwa kwenye kapu la kulindana ili kuwafichia waovu maovu yao, huyu hafai kuwepo ikulu.
 
Profesa Mussa Assad ameonyesha masikitiko yake kuhusiana na wezi wa mali ya umma wanaochekewa.

Mussa Assad aliyewahi kuhudumu kwenye nafasi ya CAG kwa mafanikio , na baadaye kuondolewa kinyume cha Katiba na John Magufuli aliyekasirishwa na kufichuliwa ubadhirifu wa kutisha wa Serikali yake, ni miongoni mwa Watanzania wachache makini sana....
Professor Assad muda wake wa uteuzi ulikwisha Isham. CAG huteuliwa na Rais kwa kipindi cha miaka 5 na anaweza kuongezewa kipindi kingine kisichozidi kimoja.

Hakuongezewa. Hayo mapendekezo yake kwa nini hakuyatoa alipokuwa CAG, kayajua leo? Basi hafai, no wonder hakuongezewa muda tena.
 
Profesa Mussa Assad ameonyesha masikitiko yake kuhusiana na wezi wa mali ya umma wanaochekewa.

Mussa Assad aliyewahi kuhudumu kwenye nafasi ya CAG kwa mafanikio , na baadaye kuondolewa kinyume cha Katiba na John Magufuli aliyekasirishwa na kufichuliwa ubadhirifu wa kutisha wa Serikali yake...
Tatizo kubwa la nchi hii ni uongozi mbovu kuanzia ikulu
 
Professor Assad muda wake wa uteuzi ulikwisha Isham. CAG huteuliwa na Rais kwa kipindi cha miaka 5 na anaweza kuongezewa kipindi kingine kisichozidi kimoja. Hakuongezewa. Hayo mapendekezo yake kwa nini hakuyatoa alipokuwa CAG, kayajua leo? Basi hafai, no wonder hakuongezewa muda tena.
Alisimamia misingi ya taaluma yake na uzalendo wa kweli lkn wapiga dili wakamuondoa!!
 
Profesa Mussa Assad ameonyesha masikitiko yake kuhusiana na wezi wa mali ya umma wanaochekewa.

Mussa Assad aliyewahi kuhudumu kwenye nafasi ya CAG kwa mafanikio , na baadaye kuondolewa kinyume cha Katiba na John Magufuli aliyekasirishwa na kufichuliwa ubadhirifu wa kutisha wa Serikali yake...
Nadhan tatizo ni chama tawala ndicho kina bless haya yote, kwann? Kwasababu hakijawah onyesha nia ya kweli ya kupambana na ufisadi!!
 
Jana Tundu Lissu alirejea nchini kimya kimya bila mapokezi wala maandamano ya misafara!

Na hapo nikajiuliza,ilikuwa na tija gani pale chama chake kilipompokea awali kwa kuandaa kampeni na maandalizi ya mapokezi kwa kutumia pesa za walipa kodi wa nchi hii.

Kwa jambo lisilo na tija kwa hao wananchi?
Jikite kwenye HOJA.

Lisu Si mmoja wa STUPID na PUMBAVU aliowaita mkubwa wakati anaipokea Ripoti.
 
Jana Tundu Lissu alirejea nchini kimya kimya bila mapokezi wala maandamano ya misafara!

Na hapo nikajiuliza,ilikuwa na tija gani pale chama chake kilipompokea awali kwa kuandaa kampeni na maandalizi ya mapokezi kwa kutumia pesa za walipa kodi wa nchi hii.

Kwa jambo lisilo na tija kwa hao wananchi?
Tuna upinzani wenye mambo ya kitoto hasa hao chadema.
 
Hapa tunajifunza jambo moja, kumbe chanzo cha wizi na uzembe huko serikalini ni "connection", watu wanapewa kazi kwa kuangaliana sura, matokeo yake hata kama mhusika akija kuharibu, hakuna wakumshughulikia, wanaoneana aibu na kufichiana maovu.

Pamoja na yote, kama Rais [mamlaka ya uteuzi] akiamua kuwa serious, ana uwezo mkubwa wa kuondoa huu ujinga, anatakiwa kuwashughulikia personally wote wanaoharibu kwenye mashirika yao, ili nao wasiwaonee aibu wale wasaidizi wao watakaowaharibia kazi.

Lakini kama Rais akiamua kuyakalia kimya haya maovu, nae anakuwa ni sehemu ya tatizo, anakuwa amekubali kuingizwa kwenye kapu la kulindana ili kuwafichia waovu maovu yao, huyu hafai kuwepo ikulu.
Wazuri hawafi, yani hivyo tu.
 
Profesa Mussa Assad ameonyesha masikitiko yake kuhusiana na wezi wa mali ya umma wanaochekewa.

Mussa Assad aliyewahi kuhudumu kwenye nafasi ya CAG kwa mafanikio , na baadaye kuondolewa kinyume cha Katiba na John Magufuli aliyekasirishwa na kufichuliwa ubadhirifu wa kutisha wa Serikali yake, ni miongoni mwa Watanzania wachache makini sana.

Akihojiwa na Azam TV, hasa kwenye hatua za kuchukua ili kudhibiti wizi kwenye Taasisi za serikali, amesema kwamba, ziko njia mbili za haraka ambazo zaweza kuchukuliwa, mosi ametaja ni ya kuwajibisha mtu binafsi, kwamba mkurugenzi wa shirika akatwe mshahara kwa kiasi fulani kila mwezi na iwe kwa kuongezeka kila mwezi ili baada ya miezi kadhaa awe hana mshahara kabisa, anadai kwa adhabu ya namna hii viongozi wa mashirika watawajibika ili kulinda mishahara yao.

Jambo la pili alilolitaja ni kwa serikali kuwajibisha moja kwa moja wajumbe wa bodi za mashirika kwa njia itakayooneka inafaa ili wasizembee kwenye usimamizi.

Prof. Assad amesema mengi sana mazuri ambayo si rahisi kuyaweka yote hapa.

Chanzo: Azam TV
Prof. Assad the genius! Adui mkubwa wa walinda legacy!!
 
Hapo hakuna njia hasa ya kwanza ni ya kijinga sana, mfano nimeiba 2B nikafungua biashara na bado ofisini nina posho za kutosha na safari kibao + rushwa, kunikata mshahara kutanipunguzia nini? watu wafungwe na kufilisiwa
 
Ila hatujiulizi hao viongozi wa mashirika ya umma wanapatikanaje.

Nawafaham watoto wa viongozi wengi ni wafanyakaz kwenye hayo mashirika, walipataje kazi only God knows.

Lingine ni compliancy ya wafanyakazi wa hiz taasis.. so relaxed and dumbs you can't belive....
Hasara iwe ya wizi au utendaji mbovu haitokaa iondoke serikalini... sio leo wala kesho wala keshokutwa...

Hapa hata kujadili ni kupoteza tu muda.
Thread closed
 
Back
Top Bottom