Profesa Mussa Assad: Kuhusu Ripoti ya CAG hakuna uwajibikaji, Mifumo ilivyo si namna nzuri ya kuendesha Nchi

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa zamani, Profesa Mussa Assad amechambua kwa ufupi mazingira ya Ripoti ya CAG iliyotolewa hivi karibuni Mwaka 2023.

Hili jambo la kuwasilisha Ripoti ndio taarifa pekee, mhutasari wa Ripoti ya CAG ni jambo ambalo anatakiwa kukabidhiwa Rais na linamhusu Rais pekee, yeye pia hatakiwi kusema jambo lolote kuhusu ripoti hiyo hadi itakapokwenda Bungeni.

Unadhani kuna uwajibikaji?
Kwa mawazo yangu naona hakuna uwajibikaji wa kutosha, kama mapendekezo yametekelezwa ni jambo zuri lakini kama hayakutekelezwa si sawa, mpaka sasa sijaona chochote kimefanywa.

Njia gani zifanywe na Serikali kuhusu Ripoti ya CAG?
Kwanza ni maumivu binafsi, kama Mkuu wa shirika haujatekeleza mapendekezo basi unatakiwa kuwajibika, Nchi nyingine zinafanya hivyo.

Mfano usipotekeleza mapendekezo ya CAG basi mshahara wako utapunguzwa kwa 5% hadi 10% kila mwezi, hiyo inamaanisha ikimalizika miezi 10 hautakuwa na mshahara kabisa.

Pia watu hao (wasiotekeleza ripoti) wanaweza kuingizwa katika ‘blacklist’, yaani wanakuwa katika orodha ya watu ambao wanaonekana hawafai, hivyo wanakuwa hawapati nafasi nyingine Serikalini.

Pili ni taasisi zenyewe kuwajibika, mfano Bodi za Taasisi, nyingi zinakuwa haziguswi ndio maana hazifuatilii mapendekezo ya CAG, hapa pia hata Wizara inayosimamia taasisi yenye shida katika Ripoti ya CAG nayo inatakiwa kupata maumivu.

Licha ya kauli ya Mamlaka lakini hakuna utekelezaji, unashauri nini?
Rais anapozungumza kwa utaratibu jambo hilo linatakiwa kuandikwa na lianze kutekelezwa, mfano Katibu Mkuu anatakiwa kuandika anachopendekeza Rais na kusimamamia au kufuatilia kile kilichopo katika maandishi, lakini wakichukulia anachozungumza Rais kuwa ni kama mazungumzo ya kawaida hapo ndipo inakuwa ngumu kufuatilia jambo aambalo lipo tu kwenye mazungumzo.

Unadhani kuna shida kwenye mfumo?
Ndio, zipo mbili, kwanza ni Ripoti yenyewe, mfano Ripoti ya Mwaka 2022, inaeleza kuwa kulikuwa na mapendekezo 205 ambayo yalitolewa kwa Mwaka 2020, kati ya hayo 60% yamejibiwa, 40% hayakujibiwa, inamaanisha kulikuwa na mapendekezo 82 hakujibiwa na hatupewi taarifa yoyote kuhusu hayo mengine yaliishiaje.

Pili ni clarity ya utekelezaji, mfano kuna ufafanuzi kuhusu mapendekezo kuwa: Yalitelekezwa kamili, Linaendelea kutekelezwa, Halikutekelezwa na Overtaken by events.

Mfano hili suala la ‘Linaendelea kutekelezwa’ lina ukakasi kidogo kwani Ripoti inapotoka kunakuwa na miaka miwili nyuma ya ukaguzi, hivyo kunakuwa kama kuna miaka mitatu hapo kati, sasa inakuwaje jambo linaendelea kutekelezwa kwa miaka mitatu?

Mifumo mingi ya Taasisi nyeti haisomani, kitu gani kinatokea?
Nchi nyingi wenzetu wanakuwa na Database moja tu ya Serikali, mfano nilienda Peru nikaona taasisi yao moja inarekodi Vizazi na Vifo, Leseni za Udereva, Umiliki wa magari n.k hivyo watu wote wanakuwa wanaingia na kupata taarifa zao.

Hapa kwetu TRA wana Database yao, Wizara, RITA na wengine wanazo za kwao, kila mmoja analinda ya kwake isiibiwe, hiyo si namna nzuri ya kuendesha Nchi.

Chanzo: Azam TV
 
Kwa kuanzia, Mh. Rais alisema, wale waliohusika na kuiba fedha za ndege wajiuzulu, yaani wapishe nafasi zao, hata hili agizo la Mh. Rais bado hawajatekeleza, yaani Mkuu wa nchi, anasema wapishe kwa sauti ya ukali na hasira sana, bado iko mijitu ofisini haitoki, ujue hawa watu wezi ni sugu sana aisee, hata Mkuu wa nchi anatoa amri, hayasikiiii, aaarrgghh..

Mh. Rais, tunakuomba urudie tena, waambie ukiwakuta ofisini wale uliowaambia waondoke, kama bado wako ukiwakuta, unawakamata, unawanyonga haraka, yaani utaona msururu wa watu wanakimbia ofisi na kuachia ngazi, sababu tunavyowajua wezi si watu wa kupisha positions zao kirahisi, ila wakisikia watanyongwa, leo leo wanaondoka, utasikia wakisema, hii sasa imekuwa serious case.
 
Ni lazima kuwepo na "collective responsibility" viongozi ambao idara zao zimeguswa lazima wajiuzulu au waondolewe, ofisi au Idara zilizoguswa ni;

1. BANDARI
2. TRA
3. AG
4.tamisemi
5. Air Tanzania

n.k n.k n.k
 
Hiyo haijawah kutokea na kamwe haiwezi tokea Tanzania, 🤣 mambo ya wazungu na ngozi nyeusi wapi na wapi🤣🤣
 
Mifumo mingi ya Taasisi nyeti haisomani, kitu gani kinatokea?
Nchi nyingi wenzetu wanakuwa na Database moja tu ya Serikali, mfano nilienda Peru nikaona taasisi yao moja inarekodi Vizazi na Vifo, Leseni za Udereva, Umiliki wa magari n.k hivyo watu wote wanakuwa wanaingia na kupata taarifa zao.

Hapa kwetu TRA wana Database yao, Wizara, RITA na wengine wanazo za kwao, kila mmoja analinda ya kwake isiibiwe, hiyo si namna nzuri ya kuendesha Nchi.
Hii ndio kitun inatakiwa Tanzania.
Labda iwe na Zanzibar kama hivi pia
AuSMT na SMZ wote wakubaliane ili wawe na Data base Moja tuu.
 
Licha ya kauli ya Mamlaka lakini hakuna utekelezaji, unashauri nini?
Rais anapozungumza kwa utaratibu jambo hilo linatakiwa kuandikwa na lianze kutekelezwa, mfano Katibu Mkuu anatakiwa kuandika anachopendekeza Rais na kusimamamia au kufuatilia kile kilichopo katika maandishi, lakini wakichukulia anachozungumza Rais kuwa ni kama mazungumzo ya kawaida hapo ndipo inakuwa ngumu kufuatilia jambo aambalo lipo tu kwenye mazungumzo
Weee! Waliozifuja hizo hela Wana nguvu kuliko mtu yeyote serikalini. Naomba nirudie. Wana nguvu kuliko mtu yeyote serikalini..... Nadhani mmenielewa.
 
Kwa kuanzia, Mh. Rais alisema, wale waliohusika na kuiba fedha za ndege wajiuzulu, yaani wapishe nafasi zao, hata hili agizo la Mh. Rais bado hawajatekeleza, yaani Mkuu wa nchi, anasema wapishe kwa sauti ya ukali na hasira sana, bado iko mijitu ofisini haitoki, ujue hawa watu wezi ni sugu sana aisee, hata Mkuu wa nchi anatoa amri, hayasikiiii, aaarrgghh..

Mh. Rais, tunakuomba urudie tena, waambie ukiwakuta ofisini wale uliowaambia waondoke, kama bado wako ukiwakuta, unawakamata, unawanyonga haraka, yaani utaona msururu wa watu wanakimbia ofisi na kuachia ngazi, sababu tunavyowajua wezi si watu wa kupisha positions zao kirahisi, ila wakisikia watanyongwa, leo leo wanaondoka, utasikia wakisema, hii sasa imekuwa serious case.
Watapisha wangapi sasa kwa mfano ..yaani kila unapoharibu ww unapusha tu ... kirahisi hivyo unaenda kula mabilioni yako huko mbele
 
Ni lazima kuwepo na "collective responsibility" viongozi ambao idara zao zimeguswa lazima wajiuzulu au waondolewe, ofisi au Idara zilizoguswa ni;

1. BANDARI
2. TRA
3. AG
4.tamisemi
5. Air Tanzania

n.k n.k n.k
AG kaguswa wapi na kwa swala lipi?
 
Back
Top Bottom