Prof. Mohamed Janabi achaguliwa kuongoza WHO AFRO
Nguvu imetumika kubwa sana tofauti na ile ya Ndungulile
Ndungulile was pure janabi kabebwa sana na mzee wa msoga pamoja na Dr Mpanju
 
Nguvu imetumika kubwa sana tofauti na ile ya Ndungulile
Ndungulile was pure janabi kabebwa sana na mzee wa msoga pamoja na Dr Mpanju
[/QUOTE

Na wewe kabebwe umalaya tu unawasumbua kila kitu kinawawashabhameni nchi basi na siasa zenu za maji taka
 
Yani Profesa anazidiwa Cv na Dr Ndugulile?

Hebu weka Cv za Ndugulile tuzichakate hapa.
Akikujibu nitagi.....
Ushabiki maadazi ni mwingi humu...
Hizi hapa kuna ya page 10 na ya page 6.........
 

Attachments

Hongera kwake Prof,
Ila sasa ile shule yake ya misosi tutaikosa au namna gani?😄
 
Whooooh🥰 afadhali maana kuna waTanzania mlimnafkia huyu baba jamani looh🚮
Hasa wanaojiita Madaktari. Ndio walioleta mambo ya hovyo humu.

Nafasi ya janabi inabeba nafasi kadhaa za watanzania wengine kwenda kula mema ya dunia. Tena mojawapo ya wanufaika ni hao walioleta maandiko ya kitaaluma utafikiri huko anaenda kupasua mioyo ya watu.
 
Hii ni taarifa ya hivi punde.
Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amechaguliwa kuongoza Shirika la Afya Duniani ukanda wa Africa.

Pongezi nyingi kwake na watanzania.
===============
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.

Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:

  • Moustafa Mijiyawa (Togo)
  • Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Mohamed Lamine Dramé (Guinea)

View attachment 3338251
Tusubiri hayers wake waje kutukana
 
Back
Top Bottom