Prof. Mohamed Janabi achaguliwa kuongoza WHO AFRO
Kama n hvy mbona unatokwa na mishipa ya kichwa kuuliza manufaa akishinda? Bila kuuliza akishindwa.

Vumilia tuu mkuu, Najua unateseka Ila ndo hvy ameshashinda, kuwa kimya kama haters wenzako wengine wanaoumia taratibu 😂
Mimi sioni faida za kushinda kwake labda nyie makada wenzake mnaweza kuwa na majibu 😅
 
Proffesa Janabi ni tokeo la elimu Bora kutoka Ulaya, ila amelitumikia taifa lake kwa nyadhifa mbalimbali IKIWEMO ya kuwa Dr wa jakaya kikwete
Ni huyo huyo Leo amekulia shavu who ukanda wa Africa angalia aliko soma utagundua yakuwa aliandaliwa kuwa wa nje bhana
Sasa wewe kapuku endelea kutengeneza mabomu kupitia wanao
We ujiulizi kwa Nini watoto wao hawapo uko?
 
Kuna watu walikuwa wanasema hatoshinda kisa uwezo mdogo sijui wako wapi now
 
Hii ni taarifa ya hivi punde.
Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amechaguliwa kuongoza Shirika la Afya Duniani ukanda wa Africa.

Pongezi nyingi kwake na watanzania.
===============
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.

Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:

  • Moustafa Mijiyawa (Togo)
  • Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Mohamed Lamine Dramé (Guinea)

View attachment 3338251
Hii nafasi ilikiwa yetu kabisa hii.
 
Prof. Yupo vizuri. Naamini ataitendea haki hii nafasi.

Ukweli ni kwamba kuna Watanzania Wazuri tuu, kama wangepata support ya taifa wangeipeperusha vyema bendera yetu.

Mpaka sasa sijui kwa nini Tz haikuweka candidate kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.
Wangemuweka Balozi Mulamula, naamini angepata ile nafasi. Sasa imeenda Ghana.

Pia tuwe aggressive UN na AU na hizi nafasi za mashirika ya kikanda.

Waziri wa mambo ya nje, kila mwaka atoe report ya Watanzania waliopata nyadhifa kubwa kimataifa. Mabalozi wetu wapimwe kwa ushawishi katika hili pia.

Mabalozi wetu wengi wamelala. Wawajibike.
Zaidi ya manufaa kwa familia zao hizo nafasi wewe zinakusaidia nini?
 
Kuna watu walikuwa wanasema hatoshinda kisa uwezo mdogo sijui wako wapi now
Yani ashinde Dr Ndugulile ndio ashindwe Profesa Janabi?

Dr Ndugulile ana sifa zipi za kumzidi Janabi na alishinda bila kufanyiwa kampeni nzito kama alizofanyiwa Janabi na Rais.
 
Yani ashinde Dr Ndugulile ndio ashindwe Profesa Janabi?

Dr Ndugulile ana sifa zipi za kumzidi Janabi na alishinda bila kufanyiwa kampeni nzito kama alizofanyiwa Janabi na Rais.
Yani umfananishe Janabi na Ndugulile ? Anyway simsemi vibaya Janabi lakini Ndugulile alikuwa na CV nzuri kuliko huyu wa sasa.
 
Yani umfananishe Janabi na Ndugulile ? Anyway simsemi vibaya Janabi lakini Ndugulile alikuwa na CV nzuri kuliko huyu wa sasa.
Yani Profesa anazidiwa Cv na Dr Ndugulile?

Hebu weka Cv za Ndugulile tuzichakate hapa.
 
Hahakikishe wazazi wa Tanzania wanajifungua bila kulazimishwa kununua gloves

Watoto na wazee wa Tanzania watibiwe bure

Other wise atakuwa hapo kuwatumikia mafisadi waliomuweka ili wapige pesa kupitia miradi ya afya

Ni hayo tu kwa janabi!!
Umepiga panapouma
 
Back
Top Bottom