Prof. Mohamed Janabi achaguliwa kuongoza WHO AFRO
Wanaume wenye kiuno zaidi ya inches 40 Janabi anawaambia wapo nje ya vigezo vinavyotakiwa kiafya
Janabi ni mgodi wa madini unaotembea
 
Ila watanzania bana...acheni watu wapate kile walichopangiwa na Mungu...
Mweee
Uccm na uchadema
Usimba na Uyangaa
Baadae tutabondana wenyewe kwa wenyewe
 
Watanzania ni watu wenye vichwa vigumu sana

Ushindi wa Janabi una faida kwa taifa la Tanzania?

Niliomba jibu la hilo swali wewe umeenda OP
Heshima kwa tabaka la wasomi, unadhani kwanini wanigeria wanaheshimika kimataifa, wameshazoea kuona wasomi wao wakizoea kupewa hizi posts za kidunia.

Ushawishi haswa wa kielimu ni kitu kikubwa mahali popote.
 
Hii ni taarifa ya hivi punde.
Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amechaguliwa kuongoza Shirika la Afya Duniani ukanda wa Africa.

Pongezi nyingi kwake na watanzania.
===============
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.

Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:

  • Moustafa Mijiyawa (Togo)
  • Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Mohamed Lamine Dramé (Guinea)

View attachment 3338251
Mm nipo hapa kama ataendelea na ile tabia yake
 
Hongera Prof
 
Wakenya wameanza kuangazia jinsi watakavyonufaika na uwepo wa Janabi ambaye ni mwanaafrika mashariki mwenzao kuhakikisha mpango wa WHO kuendelea kuitumia Kenya kama moja ya eneo la kufanyia tafiti za dawa na tiba na mengine mengi.

Kenyans wanaona Janabi ni fursa kwao kumtumia wakati sisi bongo baadhi yetu wanaona haina faida. Rais sio mjinga kumpigia kampeni mtanzania aipate hiyo nafasi. Ukitaka kuelewa faida Regional Director wa who elewa duties and responsibilities zake then elewa malengo ya who kwa ujumla. Leo mtu akisema haina faida ni kukosa akili kabisa. Kuna faida za moja kwa moja na faida mtambuka. Sera kuhusu Africa kwenye maswala ya kiafya ni shida sana.
Chadema ni wapumbavu tuu hawawezi kuelewa.
 
Msoga anakwenda kupiga madili ya pesa za afya sasa....mwenye nacho daima atazidi kuongezewa.
 
Back
Top Bottom