Prof. Mohamed Janabi achaguliwa kuongoza WHO AFRO
Hongera sana kwake na kwa serikali ya mama Samia kwa jinsi walivyompambania. Akaiwakilishe vyema nchi
 
Hii ni taarifa ya hivi punde.
Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amechaguliwa kuongoza Shirika la Afya Duniani ukanda wa Africa.

Pongezi nyingi kwake na watanzania.
===============
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.

Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:

  • Moustafa Mijiyawa (Togo)
  • Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Mohamed Lamine Dramé (Guinea)

View attachment 3338251
 
Hongera Tanzania, Hongera Africa.
 
Hii tabia ya kuteka na kupoteza watu inayofanywa na watu wasiojulikana isipokomeshwa inaweza kutuharibia.
Swala la watu kutekwa na kupotea ni moja ya aina za uhalifu wa kawaida unaotokana na mmomonyoko wa maadili baina ya watanzania.
Ukiingia kwenye magereza kumejaa aina mbalimbali za wahalifu kama wauaji wa albino , wabakaji, majambazi , magaidi na wahalifu wengine.
Miezi michache iliyopita kuna katibu wa CCM huko mkoani Iringa aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake na watu waliohusika na mauaji hayo hadi leo HAWAJAJULIKANA!.
Huku Moshi kuna kada wa CCM alimwagiwa tindikali hadi leo wahusika wa uhalifu huo HAWAJAJULIKANA.
Huko Kagera mwanaume kashirikiana na kiongozi wa kanisa kumuua mwanae albino.
Majuzi tumesikia mtu kamuua mwanae kwa kumkatakata vipandevipande kisha kimflashi ndani ya sinki la choo!
Kuna watu wanaua wake zao, waume zao nk, kwahiyo utekaji ni moja ya aina za uhalifu unaoendelea katika jamii na sisi tunatakiwa kuvisaidia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa wahalifu wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria kwakuwa wahalifu hawatoki nje ya nchi bali ni ndugu na jamaa zetu ambao tunashinda nao tukila na kucheza pamoja.
Yatakiwa mtu unapoona viashiria vya uhalifu mahala popote bila kujali kuwa ni uhalifu wa kisiasa, kijamii au kiuchumi uwe wa mwanzo kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa mapema!
ASANTE SANA.
 
Tanzania inajulikana kimataifa kwamba ni Moja ya nchi zenye wasomi wabobevu wenye sifa za kusimamia mambo ya kimataifa.
Kama kuna watu walikuwa hawaijui Tanzania wataanza kufatilia habari za Tanzania kijiografia, kisiasa, kitaaluma, kitalii , kiuchumi na mengine mengi yatakayoboresha ushirikiano kati ya Tanzania na mataifa mengine ya Africa na dunia kwa ujumla wake.
Kuaminiwa kwa pro.Janabi kwa nafasi hiyo ni moja ya misingi ya kuaminiwa watanzania wengine katika nafasi mbalimbali za uongozi wa kimataifa na hilo ni jambo zuri sana.
Kwa hiyo hizi ndio faida? 😅😅😅
 
Kushinda na kutoshindwa kwake sioni kama kuna manufaa yoyote
Kama n hvy mbona unatokwa na mishipa ya kichwa kuuliza manufaa akishinda? Bila kuuliza akishindwa.

Vumilia tuu mkuu, Najua unateseka Ila ndo hvy ameshashinda, kuwa kimya kama haters wenzako wengine wanaoumia taratibu 😂
 
Hongera nyingi kwake na timu yake ya kumuombea kura, hakika walifanya kila lililowezekana na kufamikiwa , tuna kila sababu ya kujivunia na kujipongeza na kuwashury walio wezesha na kumtakia majukumu mema na mazuri prof janabi .
 
Back
Top Bottom