Prof. Mohamed Janabi achaguliwa kuongoza WHO AFRO
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.

Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:

  • Moustafa Mijiyawa (Togo)
  • Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Mohamed Lamine Dramé (Guinea)
 
Hahakikishe wazazi wa Tanzania wanajifungua bila kulazimishwa kununua gloves

Watoto na wazee wa Tanzania watibiwe bure

Other wise atakuwa hapo kuwatumikia mafisadi waliomuweka ili wapige pesa kupitia miradi ya afya

Ni hayo tu kwa janabi!!
 
Nadhani ilikuwa ni zamu ya Tanzania tu kwenye hii nafasi.Huu uchaguzi ni kukamilisha ratiba tu.
 
Back
Top Bottom