Prof. Mohamed Janabi achaguliwa kuongoza WHO AFRO
Hivi kushinda kwa Janabi kunaisaidia nini Tanzania?

Maana hii habari imekuwa gumzo kubwa sana Tanzania
Imekuwa gumzo kwa sababu kuna watu walikuwa wanaombea ashindwe, na wakawa wanaapiza kwamba hawezi kushinda! Kwahiyo, kabla ya kuhoji kwani TZ itanufaika na nini tulitakiwa kwanza tuhoji wale waliokuwa wanaombea ashindwe kwani walihofia Tanzania ingedhurika na nini kwa ushindi wake?
 
Nadhani wa kufurahia ilitakiwa iwe mkewe na watoto maana fungu la baba limeongezeka. Atakinga maokoto Muhimbili, WHO pamoja na Ikulu.
 
Ndugu zangu hii ni dalili tosha hata no reforms no elections tutaangukia pua 🐼
Hapana mkuu msikate tamaa kiwepesi hvy 😂 naskia hata Uswisi napo hakuna tume huru ya uchaguzi ndo mana jamaa Kashinda.
 
Kwani zile nyuz zenu za kumuombea asishinde hiyo nafasi mlifikiri zingeleta manufaa au hasara gani? Prof Janabi ameshinda!! Pole kwa maumivu ya kiroho mbaya unayopitia. Jali afya yako zaidi chuki zitakupunguzia umri wa kuishi duniani hapa!!! Pumbav!!!
Maelezo marefu kama gazeti ila hakuna sehemu yoyote uliyojibu swali nililouliza.

Kati ya mimi na wewe nani mpumbavu?
 
Ushindi wake ungekuwa hauisadii chochote Tanzania baadhi yetu tusingepandisha uzi jukwaani kupinga CV yake, tena aibu yenyewe ni ukweli kwamba wale jamaa walikuwa ni madaktari wenzake!.

Riziki ni masuala ya msimu, huu muda ni wa waislam hivyo kelele zinazojificha nyuma ya udini ni upotezaji wa nguvu binafsi. Utakuja tena muda wetu wakristo kula bata.
Watanzania ni watu wenye vichwa vigumu sana

Ushindi wa Janabi una faida kwa taifa la Tanzania?

Niliomba jibu la hilo swali wewe umeenda OP
 
Hii ni taarifa ya hivi punde.
Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amechaguliwa kuongoza Shirika la Afya Duniani ukanda wa Africa.

Pongezi nyingi kwake na watanzania.
===============
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.

Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:

  • Moustafa Mijiyawa (Togo)
  • Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Mohamed Lamine Dramé (Guinea)

View attachment 3338251
Waafrika tutakunywa supu ya matembele miaka hii mpaka tuwe kama ngongoti.
 
Hongera ,Prof yaani ninefurahi mpka basi machozi ya furaha Siina tu uwezo wa kumwona ana kwa ana ila tunakuombea kwa Mungu.Sasa ule ushauri wa afya utaendelea kutoa eee
 
Back
Top Bottom