Butola
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 2,290
- 765
Butola ndugu yangu, kinachopiganiwa sio posho ya wabunge pekee,hapo ni pakuanzia tuu. Posho za vikao zitolewazo kwa watumishi wa serikali na mashirika ya umma kwa mwaka ukipata idadi yake utashtuka. Huijui CCM na watu wake wasivyo na haya? Wabunge wa CHADEMA wakisusa wao bila aibu watakuambia ok na mfumo utabaki hivyohivyo. Hauta gusa sekta nyingine na hizo fedha za posho ya Wachadema haziwezi kuleta mabadiliko yeyote.
Upo sahihi mkuu lakini bado haitoshi kwa CDM kuongea tu ilhali wanajua hoja yao haitapita, wanachopaswa kufanya ni kwenda hatua moja mbele na kuzipinga posho hizo kwa vitendo, kukataliwa kwa hoja na kisha wao kuendelea kupokea hizo posho kutauonyesha umma tofauti gani kati yao na wale wanaofurahia malipo yasiyo sawa?
Suala ni kuwa ili kuonyesha userious wao na kwa ajili ya kuuonyesha umma jinsi CDM ilivyo serious kujinyima kwa ajili ya kulinda maslahi ya umma, wabunge wao watapaswa wao sasa waanze kuonyesha mfano kwa kuzikataa posho hizi, na kitendo hiki kitaonyesha tofauti ya dhahiri kabisa kati ya wanaoumizwa na mgawanyo dhalimu wa keki ya taifa na wale ambao maslahi yao binafsi ni muhimu zaidi, kati ya walio kwa ajili ya wananchi na wale walio kwa ajili ya matumbo yao, hii ya kuongeaongea tu bila vitendo haitoshi, tunataka vitendo sasa.