Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Hamna aliye serious hapo, hiyo ni domo tu la kisiasa, tulimsikia Dr.Slaa mwaka jana na akapata sana publicity ya kisiasa lakini leo hii hana tena ujasiri wa kuliongelea hilo kwa kuyaramba matapishi yake na hivyo kuonyesha uhalisia wa mtazamo wake halisi aliokuwa ametuficha juu ya hilo.

Sintamuamini mtu yeyote juu ya hizi porojo za kujitafutia cheap popularity,kama mtu yuko serious aanze sasa kwa kuonyesha mfano wa kuzikataa hizo posho na sio vinginevyo.
I swear u will never give any valid argument until when u start to use in THINKING a special organ that is indowed in ur head for that task.
 
Cheap and populist poitics.
We need to push for the overall public policy as far as the issue of allowances is concerned. Populism won't do anything neither can it help much, dear Zitto.:majani7:

This is the push we are talking about, not just words; refusing the allowance will send a very strong message as to how serious we are in confronting corruption disguised as allowance. If you are one of those who like to talk without action, go ahead and attack Zito, but he has set a very good example to all MPs.
 
Hakuna mbunge hata mmoja wa CDM anataka posho ipunguzwe, wote wako pale kwa maslahi yao na si ya wananchi, hizo ni daganya toto tu za kisiasa mkuu

Mkuu, inawezekana unachosema ni kweli lakini kwa vile topic wameshaianzisha kwanini sisi wananchi tusiwashinikize wabunge wote (CDM, CUF, NCCR, CCM, TLP ) watueleze misimamo yao ni nini? Tujue yupi yuko na sisi na yupi ni mbabaishaji ikija kwenye interest za nchi. Sisi wananchi tunauwezo wakuwabana individually; kwani situnajua walipo/wanapopatikana. Vyombo vya habari na vyenyewe vinatakiwa kufanya kazi ya ziada kuwaanika hawa. Together we can do it bila kujali itikadi zetu. Tukiweka presha wataachia tu hizo posho wether wanataka au hawataki; wao ni wachache sana ukilinganisha na umma wa watanzania.
 
Tatizo la Ndugai anajiona yeye ni sehemu ya serikali! Sijui kwa nini anajisahau kijinga hivi!
 
i think ingekuwa beta kama wabunge wa chadema themselves wangelijibu hili...:majani7:
 
Naibu Spika Job Ndugai, amewaambiwa wabunge wa kambi ya upinzani wanaosema posho za wabunge ziondelewe waonyeshe mfano kwa kuiandikia ofisi ya bunge (Spika) kuomba kuondolewa posho zao na wao wataziondoa haraka>

Amesema kitendo cha wabunge hao kuongea kwenye majukwaa ya kisiasa kuhusu kuondolewa kwa posho hizo hakina tija na wanapaswa kuongoza kwa mfano kwa kuandika barua kwa spika ili posho zao zianze kuondolewa kwanza.

Source: TBC 1 asubuhi hii, kipindi cha Jambo Tanzania.

kwa jibu hili ndo mwisho wja Zecomed
 
Wakati siungi mkono wabunge kujichotea mahela bila sababu, NACHUKIZWA na kukerwa kwa mara nyingine na UNAFIKI wa viongozi wa CDM. Issue iko PLAIN kabisa, lead by examples! Tunaona huko YEMEN na kwingineko kama mbunge hapendi regime anajiuzulu. Hawa mazuzuwa CDM kama wanaona uchungu wa kweli wakusanye hizo posho wasaidie kwenye miradi ya maendeleo au wasiojiweza, hapo wananchi tutaamini. HOJA nyingine zozote ni UPUUZI na kupotezeana muda.
 
Nafikiri wewe ni mmoja wa watu ambao hudandia mada bila ya kuzisoma kisawasawa. Alichosema Mhe Zitto ktk bajeti ya kambi ya upinzani ni kuwa wabunge hulipwa posho za aina mbili kwa siku, ya kwanza inayitwa Sitting Allowance ya SHS 80,000/= kwa ajili ya kukaa katika vikao vya bunge; na ya pili ni posho ya kujikimu kwa lugha ya kigeni huitwa "Subsistence Allowance" ya Shs 70,000/= kwa ajili ya chakula, malazi n.k kwa kuwa viako vya bunge hufanyika nje ya vituo vyao vya kazi kwa maana ya maimbo yao ya uchaguzi. Ndipo akahoji uhalali wa mbunge kulipwa posho ya kukaa katika vaikao vya bunge ilihali kazi aliyoomba ni kuwawakilisha wananchi katika bunge na tayari analipwa mshahara kwa kazi hiyo hiyo.

Hivyo bajeti ya upinzani inapendekeza posho ya kujikumu iendelee na posho ya kukaa katika vikao vya bunge iondolewe. Vivyo hivyo kwa kwa watumishi wa serikalini hususan wakubwa wakikaa katika vikao mwisho hupitishwa bahasha zenye posho ilihali waliomba wenyewe kazi za kutumia akili katika vikao ndio maana hawafanyi kazi za shuruba kama vile kilimo, vibarua n.k. Kiutendo cha watumishi wa serikali tena wa kada ya juu tu, kulipwa posho ya kutimiza wajibu wao ambao tayari wanalipwa mishahara kuutimiza ni ufujaji mkubwa wa fedha za walipa kodi. Ndio maana vikao serikalini haviishi. Kinachotokea wanapanga vikao kufanyika katika mikoa nje ya vituo vya kazi na kupata posho mbili kama wabunge yaani posho ya vikao na posho ya kujikimu.

Je hiyo ndio siasa kwako?

Mkuu umeeleza vyema! Kulipwa posho wakati muda unaotumia ni ule unaolipwa mshahara ni wizi wa pesa za mlipa kodi!!
 
Hoja ya Mh. Zito inaeleweka vizuri kwa mtu mwenye akili ya kawaida na hakuna sababu ya mtu anayewaza vizuri kuipinga.
Wanaoweza kuipinga ni;
1. Wabunge wenye tamaa, wanaojifikiria wenyewe na familia zao. Hawa hawaoni tatizo hata kama wananchi wengine wakifa kwa njaa ilimradi tu wao wajilimbikizie.

2. Jamaa na ndugu wa karibu wa waliotajwa hapo juu ambao wana tabia kama zao na wanafaidi posho hizo.

3.Watu wengine wasiojua lolote, wanaoshabikia tu kama mazuzu.

Ni muhimu kupunguza tofauti kati ya walionacho na wasionacho na kwa hili Mh Zito anastahili pongezi na amelitoa wakati muafaka yaani wakati wa makadirio ya mapato na matumizi ya serikali.
Ili kupunguza rushwa katika uchaguzi, posho za wabunge zipunguzwe na fedha hizo ziingizwe kwenye matumizi ya maendeleo au kuongeza mishahara ya watumishi wa kima cha chini.
 
Hoja ya kwamba wabunge wengine wakatae kizipokea posho hizo si sahihi, kwani zimesha ingizwa kwenye budget,sasa nini kinafuata ni suala la kuzungumza ili zipunguzwe, kama kweli wanalipwa 175,000/= ni pesa nyingi fikiria mtumishi kama Katibu mkuu analipwa 80,000/]= na dreva analipwa 45,000/= kwenye majiji, manispaa na miji. Kwanini MBUNGE ambaye ni mwakilishi wa mwananchi alipwe mara mbili ya KM huu ni ufisadi na nilazima zipunguzwe. Naunga mikono na miguu hoja
 
M nafikiri ni wakati mzuri kwa wabunge wa UPINZANI wa kweli kuuthibitishia uma kwamba wapo pamoja nao kwa kuzikataa hizo posho kwa nguvu nzote. Asilimia 99 ya wananchi wote wanaunga mkono hoja hiyo isije ikawa walikuwa wanatafuta umaarufu bila kujitoa mhanga. Kwa mfano idadi ya wabunge wote wa upinzani au watakaokubaliana na hoja hiyo hela zao zikajumulishwa na kufanya kitu cha maana kama kujenga vyoo au kununua madawati tutaona wamefanya la maaana sana ili hata watakapokuwa wankuja kwetu kututambishia waseme tuliokoa kiasi fulani cha hela zikafanya kazi fulani:smiling: Cha kushangaza unaweza kuona hoja hiyo imeishia mdomoni mwa Zitto.

Sio wapinzani tu ni wote. Sisi wananchi tunauwezo wakuwataka wafanye hivyo. Sisi ndio tumewaajiri na sisi ndio tutawaachisha ajira. Asiyetaka ajulikane wazi huyo si mwenzetu. Tumewatuma kule si kwa makundi (upinzani vs CCM) tumewatuma wakatuwakilishe kwahiyo it is not what they want it is what people of Tanzania wants. Hamna hata haja yakupindisha pindisha hii hoja.
 
Its time for action, Mh Waziri Zitto umetoa hoja, kama wabunge hawataki waacheni, lakini kama hili liko ndani ya uwezo wenu CDM litekelezeni ili ukweli wake uonekane.

Kwanini waachwe na sisi wananchi ndio tumewaajiri? Mimi nashindwa kuelewa hii mantiki. Hili ni suala la kupunguza spending hata makazini utasema tupunguze marupurupu ya matarishi alafu madereva tuwaache? Sisi wananchi tuna-demand wafanye hivyo, sisi ndio tumewaajiri na sisi ndio tunawalipa. Hivi bosi akija kazini akasema sasa tunaondoa overtime pay inakuaje. Ni either unakubali au unaacha kazi; huwezi kujadili eti ondoa kwa fulani lakini mimi hivi na hivi.
 
Kwanini waachwe na sisi wananchi ndio tumewaajiri? Mimi nashindwa kuelewa hii mantiki. Hili ni suala la kupunguza spending hata makazini utasema tupunguze marupurupu ya matarishi alafu madereva tuwaache? Sisi wananchi tuna-demand wafanye hivyo, sisi ndio tumewaajiri na sisi ndio tunawalipa. Hivi bosi akija kazini akasema sasa tunaondoa overtime pay inakuaje. Ni either unakubali au unaacha kazi; huwezi kujadili eti ondoa kwa fulani lakini mimi hivi na hivi.

Hoja za hao jamaa ni so cheap, argument ni kwamba kuna huge budget deficit na njia kuu mbili za kudeal na hiyo ni aidha kubana matumizi au kuongeza mapato. Sasa kama wanaona kubana matumizi is not an option wasuggest basi namna gani ya kuongeza mapato ya serikali.
 
This is the push we are talking about, not just words; refusing the allowance will send a very strong message as to how serious we are in confronting corruption disguised as allowance. If you are one of those who like to talk without action, go ahead and attack Zito, but he has set a very good example to all MPs.

Public policy and political management require expanding horizons, otherwise expect no broader achievement but ever grumbling.
 
We must walk the talk. I have written to the Clerk of Bunge that all sitting allowances I am entittled to should be directed to a charity in my constituency up to when the law is changed and sitting allowances scrapped.
I will advise my fellow CHADEMA MPs to take similar measure.

Kwa nini msikusanye hizi hela kama Chadema na kufanya kitu cha maendeleo kama Chama. Kwa mfano, kujenga shule, kununua madawati kwa shule moja, au kitu kingine kinachoendana na sera zenu. Pia mnaweza kuziwekeza kwa kusudi la uchaguzi ujao ili muweze kupata wawakilishi katika vituo vingi zaidi vya kura, ambao wataweza ku-relay information moja moja kwa central command. Kwa mfano mkiwapa simu au vocha za kutuma matokeo immediately, basi mtaweza kuhakiki jinsi uchaguzi unavyoenda kwa undani. Charities hazina mipango na mara nyingi pesa zinaishia administrative work. Charity ni njia rahisi ya kutoa hela yako, kama vile benki ilivyo njia rahisi ya kuwekeza pesa. Lakini kama utakuwa tayari kutafuta njia bora zaidi na zenye return ni sharti ufanye research kidogo.
 
Jana nilifuatilia kwa makini hotuba ya Mh. Mustafa Mkullo wakati akiwasilisha bajeti ya Tanzania kwa mwaka 2011/2012. Kama ilivyo kawaida ya bajeti za miaka yote kodi katika vinywaji na sigara ilipandiswa. Vile vile ada ya leseni iliyoondolea na Mramba wakati wa utawala wa Mh. Mkapa ilirejeshwa tena. Mabadiliko hayo ya kwenye vinywaji, sigara na leseni za biashara nakubaliana nayo kwa 100% kwani yanalenga kuongeza mapato ya serikali.

Badiliko pekee lililonivunja nguvu ni lile la kutotoza kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa watumishi wa serikali na taasisi nyingine zinazopokea ruzuku ya serikali kwani hii inapingana na Ibara ya 81 ya Sheria ya Mapato ya 2004 na inapunguza mapato ya serikali.

Tafsiri yangu kutokana na kutotoza kodi kwenye posho za watumishi wa serikali na taasisi nyingine zinazopata ruzuku ya serikali ni kuwa "watawala wameungana na wafanyakazi wao na wanasiasa" kutekeleza sheria ya mapato ya mwaka 2004 kibaguzi. Nasema hivi kwa sababu mabadiliko hayo yatawahusu:
(i) Viongozi wakuu wa serikali ambao mbali na mishahara yao wana posho mbalimbali zinazozidi hata mishahara ambazo kwa mujibu wa sheria ya mapato ya mwaka 2004 zinatakia kulipiwa kodi lakini kwa kuwa wao ndio walioshika mpini wameamua kutokulipa kodi;

(ii) Wafanyakazi wa serikali na taasisi zake nao wanaungana na watawala kutokulipa kodi. Kwa tafsiri hii watajipangia mishahara midogo na sehemu nyingine kujilipa kama posho na hivyo kutokulipa kodi;

(iii) Wanasiasa - kutokana na vyama vya siasa kupata ruzuku ya serikali watawalipa watumishi wao posho badala ya mishahara na hivyo kutokulipa kodi kabisa.

Matokeo hasi ya mabadiliko haya ni kuwa

(a) Utendaji wa TRA kwenye kuhimiza ulipaji wa kodi za mishahara kwenye sekta binafsi hasa kwenye posho utapata upinzani, ilitakiwa wadai kodi wakionyesha mfano wa wao kulipa hizo kodi kinyume chake wao hawatalipa bali watawataka wafanyakazi wa sekta binafsi walipe. Wakati wa utawala wa Mh. Mwinyi, serikali ilifuta kodi kwenye posho na matokeo yake Mh. Mustafa anafahamu kwani Serikali ilikuwa na hali mbaya sana kifedha na

(b) Nia ya serikali kukuza sekta binafsi itafifishwa na rekebisho hili kwani nguvu kazi kubwa itapendelea kufanya kazi kule ambako watalipa kodi kidogo

(c) Kutakuwepo tofauti ya mapato kwa watu wa kada moja mfano nesi anayefanya kazi serikalini posho zake za night allowance hazitatozwa kodi lakini nesi ambaye yuko hospitali binafsi posho zake za night allowance zitatozwa kodi.

Mtazamo wangu ni kuwa rekebisho hili ni mtego mkubwa kwa wabunge wetu. Endapo watapitisha rekebisho hili, ina maana wako bungeni kwa maslahi binafsi kwani wao na vyama vyao ni sehemu ya watu watakaofaidika na rekebisho hili. Kwa upande mwingine, chama cha waajiri Tanzania na vyama vya wafanyakazi ambao si wa sekta ya umma ni wakati mwafaka kujitokeza na kupinga rekebisho hili kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
"Hatuwezi kuwaachia nguruwe wale mihogo shamani peke yao"___Hamad Rashid Mohamed (Mp)
Kwa kuwa hao nguruwe wa kijani wanaiba mihogo ya wananchi, ni bora na sisi tuibe pia??? Mh! Jamani!

Natamani kuiona siku ambayo wabunge wa CDM watamwambia spika "posho yetu tunaiweka na kufanya ABC ili kuonesha kuwa kama wote tungefanya hivyo nchi hii ingepiga hatua... Najaribu kufikiria km baada ya kikao cha bunge wakanunua ambulance kwa ajajili ya wananchi wa Tandahimba au Namtumbo na hiyo amburance(s) zikawa/ikawa na chata la CHADEMA kwa nyuma. Duh,... From there hatutahitaji nguvu kubwa kuwaelewesha wananchi wa tandahimba au namtumbo kuwa laiti pangekuwa na mgawanyo sawa wa keki ya nchi hii, kina mama wasingejifungulia majumbani na chini ya miembe wakiwa njiani kwenda hospitali kama ilivyo sasa!!
 
Vincent,

Mabadiliko haya kimsingi yanalenga kuhalalisha kile ambacho kinaendelea. Kama utakumbuka tuliwahi kukijadili katika mada iliyokuwa inahusiana na Mh mbowe kusema kuwa Dr Slaa analipwa posho na sio mshahara na hivyo hakuna kodi. Kama tulivyosema kwenye mjadala ule, in practice vyama vya siasa, taasisi za serikali na naamini pengine hata bunge lenyewe kwa muda mrefu zimekuwa hazilipi kodi kwenye posho mbalimbali zinazowapa watumishi wake (pamoja na kwamba ilikuwa ni kinyume cha sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004).

Inatia mashaka sana kuanza kubaguana katika namna hii na kimsingi inafanya sheria hiyo kuwa kinyume na katiba. kila mtanzania anapaswa kulipa kodi ya mapato kutokana na kipato chake, iwe ni biashara, ajira au uwekezaji bila kujali source ya kipato hicho. Na kama ulivyosema hatua hii inatoa ishara mbaya juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom