Nilimsikiliza na kumwona laivu pale C10 Mh Zitto akiliongelea suala hili la posho Bungeni na kwenye ajira za serikali na taasisi zake. Na kama kawaida yake alikuwa na takwimu pia. Kwa kweli inasikitisha kuona jinsi watu wanavyojilipa mara mbili au zaidi kwa kazi wlioajiriwa kuifanya kwa mshahara mzuri tu. Haya masuala ya posho yalishakuwa ni utamaduni, ni sehemu ya maisha ya viongozi wetu. Posho hizi ndizo zinazoendesha nyumba ndogo na anasa nyingine. Kwa aina ya Wabunge tulionao sasa sio rahisi kukubali kuziondoa posho hizi lakini ngoja angalau Mh Zitto aziseme Bungeni wananchi wajue nchi inavyotafunwa na wachache.