Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,308
Mimi nadhan tungekuwa wa kweli tu, ofisi kubwa ya mwanasiasa makini ni jukwaani, sidhan kama kuna dhambi kuyasemea mambo hayo jukwaani, kama hoja ni kuandika barua tu basi hakuna haja ya kukaa bungeni waandikiane barua tu mambo yote yajadiliwe kwa barua.
Hata kama mnawapenda wabunge hawa wengi wao ni watu ambao hawajali wananchi wao, Mtu kama Rashid Mohamed ambaye mimi namheshim na kumkubali kama mbunge makini ila kwa hili alilosema lazima nimpunguzie credit naona kama amekurupuka pengine ni hasira za kukosa ukuu wa kambi ya upinzani.
Na ukweli wa wanasiasa wanakuwa na hotuba mbili pale jukwaani ya kuwaelezea mafala mfano hii ya kupinga posho na ya kweke mwenyewe kwa kuikumbatia na kuipenda ilhali akijua anaweza kupeleka kusudio kwa spika la kufuta posho lakini asifanye hivyo.
Kwahiyo wanasiasa hawana lolote zaidi ya kuangalia maslahi yao usibabaike sana na maneno yao matamu kikubwa tuangalie yetu yanatendeka? tumewachagua majimbo je wapo pamoja na sisi kwenye kuleta maendeleo ya jimbo? wamesaidia nini uwepo wao bungeni kuleta tija kwenye majimbo yanayotoka?