Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Magamba utayagundud tu siku zote, kama kaingia baada ya kugharamia wapiga kura uoategemea ataacha kuvuna na kurudisha alichotumia? Ukweli unabaki pale pale CDM wanatutetea sisi walala hoi ila basi tu wananchi bado hawajui ndio maana wanayakubali magamba.
 
Nina wasi wasi kama zitapelekwa kWeli huko kwenye mahospitali NA SEHEMU nyingine mlizoshauri ni vema wakasema hizo pesa zipelekwe kwenye halmashauiri Wabunge hao wanapotoka ili zikapangiwe Majukumu huko. Na itakuwa rahisi kuzifuatilia na Wananchi wanaowakilishwa wataambiwa kuwa zimefanya nini katika jimbo lao. MAKAMANDA WA CDM HAWAWEZI KUTUANGUSHA na huo utakuwa ni mwanzo wa ukombiozi wa kweli. Peoplesssssss!!!!!!!!!!
VIVA CDM
 
Tatizo mwenzao anatoa hoja kisha wengine wanaendelea kupokea hizo posho. Inatakiwa CDM wote wasizipokee ili iwe mfano kuwa inawezekana!
 
Watanzania wana maajabu sana, Eti 'Chadema wasusie posho ndo tutaamini'.
Mtaamini nini?
Kwamba kuna matumizi mabaya au?

Na mkishaamini itakuwaje?
Mtafanya nini baada ya CHADEMA kususia posho?

Sijali kama CHADEMA wanachukua au la. Kitu muhimu ni kuwa CHADEMA imeanika uozo, hii nchi siyo ya CHADEMA tu.

Badala tujiulize wananchi tufanye nini baada ya kujua wizi huu wa serikali, tumekaa kando na kung'ang'ania CHADEMA wafanye hiki na kile eti ili tuwaamini. Wengine hapa wabunge wao ni magamba, mbona hamtafuti namna ya kuwashinikiza wateme hizo posho wanazomeza?

CHADEMA wamefanya jambo kubwa sana kuweka hadharani suala hili, suala la kujiuliza sisi raia tunashiriki vipi kuiondoa hali hiyo. Siyo unafiki wa kuwadai CHADEMA wafanye hivi na vile eti ndo muwaamini.

Yaani wabongo kila kitu tufanyiwe tu na fulani... Ndo maana tuliambiwa tule majani.
 
BAADA YA WAZIRI KIVULI WA FEDHA MH. ZITO(CDM) KUTANGAZA VIPAOMBELE VYA BAJETI YA UPINZANI NA KUPENDEKEZA KUPUNGUZWA KWA POSHO ZA SEMINA KWA VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWEMO WABUNGE, IMEPOKELEWA TOFAUTI NA WABUNGE WA CCM HUKU WENGI WAO WAKIDAI KUWA POSHO ZAO HAZITOSHI. JOBU NDUGAI, CHILIGATI NA WENGINE WENGI KUTOKA CCM WAMECHARUKA VIKALI KUPINGA KUPUNGUZWA KWA POSHO ZAO. LEO ASUBUHI KTK KIPINDI CHA JAMBO(TBC) MH. NDUGAI AMBAYE NI NAIBU SPIKA ALIKANA KABISA SWALA HILO NA KUSEMA KUWA CDM WAMEPOTOSHA. SWALI; je, kuna ulaazima gani wa mbunge kulipwa mara mbili kwa kazi hiyo hiyo moja? mimi nadhani posho wanazopewa kwa siku sh.(1750000) zinatosha kuendesha hata shughuli nyingine wanazofanya ikiwemo semina na kamati. vp kuhusu waalimu, madaktari, maafisa kilimo na wananchi wengine?

CCM UDP NCCR watabisha sana juu ya kuondolewa posho ya vikao kwa mazoea tu na sio kwa mantiki.

Utaratibu wa posho ya vikao ni mzuri tu endapo nchi au asasi ina hela nyingi na hakuna njia nyingine ya kugawana zaidi kupitia vikao kama njia tu kuhalalisha matumizi.

Akina Ndugai na Chiligati wenzao wenye mawazo hayo hawatakubali kamwe hiyo idea kwa sababu posho ni moja ya motive za wao kuwania ubunge uspika na vyeo vingine vya kiserikali etc

Nasema kimantiki posho ya vikao ni moja ya matumizi mabaya ya kodi ya wananchi. Yaani mtu analipwa mshahara, posho ya kujikimu safarini na posho ya kikao...yaani unavyoona jitu limelala pale Bungeni.. Anatakiwa kuclaim posho ya kikao. It doesn't make sense kwa economy yetu hata kwa nchi zilizoendelea hazima upuuzi kama huo. Mnaofanya ktk mashirika binafsi nadhani mnaelewa hii dhana.
 
Mafisadi ngoja yatese, mwisho wao wawajia muda si kitambo!
 
We must walk the talk. I have written to the Clerk of Bunge that all sitting allowances I am entittled to should be directed to a charity in my constituency up to when the law is changed and sitting allowances scrapped.
I will advise my fellow CHADEMA MPs to take similar measure.

Silipendi chama lako na wewe pia, lakini kwenye HILI nakupongeza sana mheshimiwa, ni bora uoneshe kwa vitendo kuwa inawezekana. Naomba ushauri huu wape wabunge wote sio wa lichama lako tu kwani hili ni jambo jema kwa linapaswa kufanywa na wabunge wote kwa maslahi ya masikini.
 
Watanzania wana maajabu sana! Eti 'Chadema wasusie posho ndo tutaamini!!' Mtaamini nini? Kwamba kuna matumizi mabaya au? Na mkishaamini itakuwaje? Mtafanya nini baada ya Chadema kususia posho?! Sijali kama Chadema wanachukua au la. Kitu muhimu ni kuwa Chadema imeanika uozo, hii nchi siyo ya Chadema tu, badala tujiulize wananchi tufanye nini baada ya kujua wizi huu wa serikali, tumekaa kando na kung'ang'ania Chadema wafanye hiki na kile eti ili tuwaamini!! Wengine hapa wabunge wao ni magamba, mbona hamtafuti namna ya kuwashinikiza wateme hizo posho wanazomeza??? Chadema wamefanya jambo kubwa sana kuweka hadharani suala hili, suala la kujiuliza sisi raia tunashiriki vipi kuiondoa hali hiyo. Sayo unafiki wa kuwadai Chadema wafanye hivi na vile eti ndo muwaamini!! Yaani wabongo kila kitu tufanyiwe tu na fulani... Ndo maana tuliambiwa tule majani!!!

Kwani wakiacha kuchukua hizo posho wewe utaumia nini? Mbona Zitto kaagiza zake asipewe? Mimi sioni sababu ya wewe kupanic labda uwe ni mbunge wa CDM unaogopa maslahi kuingia kwa mitini.
 
Mbunge aliyetoa Hoja yupo Bungeni kwa kipindi cha pili. Je ni lini alikataa posho hizo? Wazungu wanasema "charity begins at home"
 
Ni aibu kuasikia naibu Ndugai ame-coment hivyo! Shame I am afraid ESAMI center of management excellence haikumsaidia kitu.

Zito anaongelea policy related issue then mtu tena kiongozi wa Bunge anasema waanze wao kwa kuonyesha mfano How is that... Is he suggesting CDM wakileta mswaada wataupitisha... No wonder we never see real development
 
Nilitanguliza kuomba samahani kwa sababu nilijua hili lingeweza kutokea na ni kawaida. Tujiulize kitu kidogo Mery, Mfumo huundwa na nini?

Bila ya shaka mfumo unaundwa vitu kadhaa zikiwemo taratibu, sera, dhamira n.k Tunaweza kuupinga mfumo kama mfumo, lakini pia tunaweza kupinga baadhi ya ellement za mfumo husika.

Tunapoandamana kupinga unyanyaswaji wa wananchi waishio karibu na migodi tunaupinga mfumo, lakini pia ni katika eneo ama aspects kadha wa kadha! Si busara kuona mambo yasiyowatendea haki wananchi tukayafumbia macho kwa kisingizio kuwa tunachopambana nacho ni system... Si sawa! Jiulize hiki:

Serikali ya ccm imewahi kutoa bonus ya migodi kwa viongozi wake (Reffering Kiwira) Sasa, ikiamua ikasema kila mbunge baada ya kustaafu upewa squre meter 40X40 katika eneo la mgodi, should we expect our leaders to accept kwa dhana kuwa "Kususa" si ufumbuzi?

So wachukue? Nakwambia IKO SIKU WATU WENYE UCHUNGU NA NCHI HII WATAWALAZIMISHA KURUDISHA MALI ZOTE WALIZOZICHOTA KUTOKANA NA KODI NA JASHO LA WATANZANIA... When that happens.... sijui, but I wouldnt wish to see the day ambayo viongozi ninaowaamini pia watapaswa kurudisha!

We una matatizo, ulipoleta mada haraka nlikimbilia store kuangalia mchango wako wakati CHADEMA walipotoka bungeni, sikuona popote ulipowasapoti.

Hivi leo unasema utapeli huu usifanyike CHADEMA but uendelee CCM? Huwezi ukawa unserious kiasi iki. Hivi wanasema kugoma au wanaongelea sheria na kanuni?

Hivi kuna vikao vya CHADEMA au vikao vya bunge zima?

Ok wakienda vikao vya CHADEMA wagomee ila si kwa vikao vya wote, kwa iyo kuna siku tutapitisha sheria kuwa atakayeiba afungwe jela. Halafu useme waanze kufungwa wa CHADEMA? We vipi?
 
Wakuu zangu,
Tafadhalini! mnasikitisha sana mnapoandika vitu ili mradi fikra zenu zinafikiria hivyo basi lazima iwe hivyo..
Kumbukeni kwamba hoja zote za kambi ya Upinzani ni kulitaka bunge la nchi yetu lipitishe na iwe sheria. Na ndio maana tunawaona wakiwasiliosha bajeti yao ambayo sidhani kama mnataka Chadema au kambi ya Upinzani waitumie wao dhidi ile ilopitishwa...

Na ikumbukwe tu bunge linapopitisha sheria iwe hata Posho ni wajibu wa kila mmoja wetu kuheshimu maagizo hayo hata kama hatukubaliani nayo. Kuna maamuzi mengi yamepitishwa kisheria ambayo Chadema hawakubaliani nayo lakini hawana hila isipokuwa kufuata kwa sababu ni sheria tayari..

Tena basi yapo maswala ambayo Chadema hwakubaliani nayo lakini wakifuata mfano huu hapa mtawaona vichaa. Kwa mfano Chadema hawakubaliani na mambo mengi sana ndani ya katiba iliyopo lakini leo wakichukua hatua ya kususia baadhi ya sheria zilizopo kweli bado mtawapenda hivyo ama kuwaita waasi na wanaotaka kuleta vurugu nchini..

CCM ndio kinara wa maamuzi ni wao wenye wabunge wengi na wao ndio wameshika mpini hivyo kitakachopita bungeni kitaheshimiwa na kupokewa..
Mimi binafsi sipendi wala sikubalianina Wabunge wanaoishi nje ya majimbo wanayowakilisha kwani hawana uchungu wala muda kabisa wa kuyatembelea hali vyama vinapewa mamlaka ya kuchagua majina ya wagombea bila kujali wanaishi wapi na wananchi hawakupewa nafasi ya wao kuchagua wanamtaka kiongozi wa aina gani..
Mfano mwingine siwezi kumsusia Dr.Shein kama rais halali wa Zanzibar ingawa kisheria hakuwa mkazi wa Zanzibar, ni mkazi wa bara na kajiandikisha bara na kapita uchaguzi kinyume cha sheria za uchaguzi Zanzibar..Again, hivi kweli itakuwa busara kwa CUF na wabunge wake kutomtambua kwanza Shein kama ni rais ikiwa wataiwasilisha hoja hii bunge la Zanzibar?
 
We must walk the talk. I have written to the Clerk of Bunge that all sitting allowances I am entittled to should be directed to a charity in my constituency up to when the law is changed and sitting allowances scrapped.
I will advise my fellow CHADEMA MPs to take similar measure.

with honour I beg to stand away your decision my MP,hon.Zitto! Should this mean that you have rejected the allowance or you have channel it somewhere you are interested. Should this mean that you have cut down govt.cost/expenditure on allowance or changed its direction? This is much like when Prime Minister refused the very expensive V8 and it was given to someone else in need. Did he save anything in that? What was need here is to push the Speaker to have the idea of raising the discussion and not to do it own your own. We should build laws and regulation of rule of order and not rule of who decides! I heard my Ndugai morning suggesting the same, for sure that is not what we citizens desire whether it will work in long run or not. Mr Zitto,you mean next time you suggest a regulation or lets say a law that whoever refuses to attend govt.hospital whenever he/she feels sick should be hanged in public and the Parliament refuses,should you suggest that you inform the govt.that it should work on you and to you family ??then if you don't find health health attendant at govt.hosp and switch to private ,then we should hung you? Yes,my example isn't torelable,but in reality it can't work on individuals but to the public or all Mps. We are not there to show examples,we should suggest our Parliament prepure laws and orders and not else! In this I beg you to draw your letter back and still insist the govt.to 'eradicate'such abnoxious allowances,we will,and continue respecting you even being with that allowance until order to remove such allowance in general is in place. Otherwise wish you all indelible and remarkable success in your entire life and politics!
 
watu kuachia za posho kwa hiyari siyo hoja tunataka iandikwe kwenye sheria ili kila mbunge aondolewe na siyo kwa kujitolea kama anavyotaka mheshimiwa ndugai ambaye anaonekana kufikiria kwa kutumia tumbo kuliko ubongo wake.
 
Kwani wakiacha kuchukua hizo posho wewe utaumia nini? Mbona Zitto kaagiza zake asipewe? Mimi sioni sababu ya wewe kupanic labda uwe ni mbunge wa CDM unaogopa maslahi kuingia kwa mitini.

ndugu kinachotafuta ni public policy si chadema policy wala Zitto policy. We need to build a new order and not one or two citizens wishes. In this it will be passed like this,then citizen should be given option to reject or accept rules they want. Then some shall opt to spare all rules to be kept behind bars,what is next?it means every citizen to decide what one wants and reject the other! We are preparing a self ruled nation then!
 
We must walk the talk. I have written to the Clerk of Bunge that all sitting allowances I am entittled to should be directed to a charity in my constituency up to when the law is changed and sitting allowances scrapped.
I will advise my fellow CHADEMA MPs to take similar measure.

Huu ni mfano mzuri na umeonesha ukomavu wa kisiasa na kiuongozi thanks again Hon. Zitto!
Wabunge kadhaa wa chadema wamekuwa wakifanya hili la kutumia posho zao katika charity activities katika majimbo yao nao nawashukuru sana. Hoja ni nzuri japo tayari naibu wa spika ameipinga pamoja na Mh. Hamad Rashid katka mazungumzo yao ya asb ya leo katika Jambo TBC. Imagine ni mabilion mangapi yataokolewa kwenye pesa za alllowance za wabunge peke yao. Hii itaambatana na kufuta posho za kijinga mfano za chai na vikao vya kiselikali then zikitumika katika shughuli za kuleta maendeleo basi nadhani sekta kama afya na elimu pamoja na kilimo basi zitaboreshwa na kusaidia kukuza uchumi wa nchi hii.

Swala hapa siyo kususia posho ni harakati za kufumua mfumo wote na kuanza upya kwa kila kitu.
 
Huyu Hamad Rashid kichaa tupu kwa sababu Mbunge analipwa mshahara ambao una cover hadi mikutano ya kamati ambazo pia ni kazi ya Bunge..Kama vikao hivi vingekuwa nje ya Bunge tuseme mathlan yupo ktk board of directors ya shirika fulani posho hiyo inaeleweka, lakini tunazungumzia kuondoa posho hizi kwa wabunge wanapokuwa wakifanya kazi za bunge.

Kifupi Wabunge wanalipwa mara mbili kama vile ni overtime hali majukumu haya wameyaomba wenyewe ku volunteer ktk kuonyesha uzalendo wao ktk kulitumikia taifa.

Tunachosema wananchi mishahara yao ni mikubwa sana ukilinganisha na hali ya uchumi wa nchi yetu hivyo sii swala la kipimo cha maisha yao wao bali kipimo kinaanzia ktk uwezo wa nchi yetu.

Leo hii mimi siwezi kuzungumzia maswala ya kulala Hotel ya five star kutokana na uwezo wangu na sii kutazama gharama hizo nastahili au laa...Swala hapa ni fedha hizo zinaweza kabisa kutumika ktk kujenga au kuimarisha miradi mingine ambayo imesimama kutokana na ukosefu wa fedha..
 
mpuuzi mkubwa huyu Ndugai
anatumia makalio kuanalyse

Hapa wapinzani wanataka mfumo urekebishwe ili kujaribu kuleta usawa na si kugomea posho.

Wapinzani wanazungumzia MFUMO kugomea posho/mishahara hakutasaidia chochote.

Hawa viongozi sijui Ndugai ni zero kabisa. Hii sio kukomoana ni kujaribu kupunguza spending. Too much spending, tuna-spend zaidi ya tunavyo-gain lazima tubadilishe huu mfumo mzima. Nategemea viongozi wa upinzani watawaelewesha wasioelewa huko bungeni. Kweli hawa viongozi ni mzigo sana kwetu .
 
Back
Top Bottom