Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Nadhani CCM wakati mwingine hawafikirii "rationally" maana wabunge wa upinzani wametoa pendekezo kuwa ile sitting allowance ya kwenye vikao iondolewe na ibakie posho ya kujikimu. Hii ni hoja inayofikirika na inaingia masikioni. Tatizo la wabunge wengi wa CCM ni kwamba bunge ni sehemu ya kuchuma fedha na siyo kutatua kero za wananchi. Wabunge wakipitisha hivyo katika kanuni zao inakuwa ni rahisi kuwabana pia viongozi wa serikali kuondoa hiyo sitting allowance katika mikutano yao ambayo wamepewa nafasi hizo ili kuweza kukaa katika vikao mbalimbali kuamua au kupanga mamba kwa niaba ya umma wa Watanzania.
Katika hoja za msingi tuache ushabiki wa kisiasa. Kwa Tanzania politics is the highly paying job bila mtu kufanya kazi! No performance review from time to time rather wananchi wenyewe during elections ambayo nayo it is rigged big times!!!!
 
TBC muda huu Kuna mahojiano,

Mh Ndugai Kaulizwa swali kuhusu kupunguziwa posho zao kashindwa kutoa jibu na msimamo wake

Na Mh. Hamad Rashid wa CUF yeye kasema posho analipwa 150,000 analala hotel shiling 80,000 Anamlipa dereva wake sh 30,000/= na kula elf 40,000/= na kumaliza kwa kusema kuwa haoni kama kuna hela inabaki hapo,

Swali langu ni, Hivi dereva wa mmbunge analipwa na Mbunge??,
Hivi wabunge wanalipwa shilingi ngapi kama posho??, coz hiyo figa nanikumbuka na ni ya kitambo, nikosoeni kama nimekosea, nielimisheni inapowezekana!

Fedha za Serikali hutawaliwa kwa mujibu wa Kanuni za fedha za Serikali.Kanuni hizo huelekeza stahili ya kila mtumishi anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi. Stahili ya watumishi wenye hadhi ya mbunge hivi sasa ni Shs 80,000/= tu kwa usiku mmoja anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi.

Katika kanuni za fedha za Serikali hakuna kitu kama posho ya vikao kwa watu ambao waliomba wenyewe kazi ambazo hufanyika maofisini ambapo niia mojawapo ya kutimiza wajibu wao ni kuhudhuria na kushiriki katika vikao k.m vikao vya bunge. Ikumbukwe kuwa wasomi huomba kazi za kutumia akili ambazo nyingi hufanyika maofisini kupitia vikao, mikutano, semina, warsha, kongamano n.k ndio maana husalimika na shuruba za kilimo, kazi ngumu kama vibarua n.k. Iweje wasomi hao leo wageuke na kudai kulipw posho kwa kazi ambazo wanalipwa mishahara na ambazo kwa vigezo vyote ni nyepesi na hufanyika katika amzingira mazuri kuliko kazi wafanyazo wananchi wa kawaida?

Kanuni za Ajira na Fedha za Serikali hutaja aina ya watumishi ambao wanastahili kupata wasaidizi kama vile makatibu wahutasi (Secretaries) madereva n.k. Kwa mujibu wa majibu ya kifisadi ya Mhe Hamda Rashid inaonyesha kuwa Kanuni za Ajira na Fedha za Serikali haziwatambui wabunge kuwa hadhi ya kupatiwa madereva, kama zingekuwa zinatambua hilo madereva wa wabunge wangeajiriwa na Serikali (ofisi ya bunge), na kulipwa mishahara na posho na Serikali kama madereva wa wengine wa Serikali. Toka lini ukasikia Waziri au Katibu Mkuu au Mkurugenzi wa Wizara anagawana Posho yake safari na dereva wake?.

Kinachojitokeza hapa ni kuwa wabunge wetu wanajikweza sana pasipo kutazama umasikini wa wapiga kura wao ndio maana wanakuwa na mahitaji makubwa ya kuhitaji dereva n.k. Ofisi ya bunge inamiliki idadi kubwa ya mabasi kwa ajili ya kuwasafirisha wabunge kwenda na kutoka katika vikao vya bunge kutokea ofisi za bunge; ambapoi kutokea hapo wabunge wanatakiwa kutumia usafiri wa umma kama vile treni, mabasi n.k ili kujua hali halisi ya usafiri wanaotumia wananchi.

Ni kwanini kila mbunge apige gari moto kuelekea Dodoma? kama sio ufujaji wa fedha za walipa kodi. Ndio maana wabunge wanajiingiza katika ufisadi wa posho mbili mbili ili kumudu maisha haya ya anasa.

Ndio maana wabunge waroho kama Mhe Hamad Rashid na wenzake wote wanaotetea utaratibu huu wa kifisadi wanalazimika kutetea wizi wa fedha za serikali kwa njia ya posho za vikao ili kufidia masiha ya anasa ya wabunge wetu.
 
Kweli kabisa,anakula elf40 anaona ni poa kabisa,wanafunzi wanasema elf5 haitoshi wabunge
wana washangaa,....wapuuzi kabisa!===Tunaitaga ujinga wa nyani kuona nini... ya mwenzie!!!

Devera analipwa elf30 kwa siku kweli?=== Ndo hivo jamaa kasema sasa
so dereva anakula nini?=====hakufafanua!
ana lala wapi kwa hiyo hiyo elf30 kwa siku? -------Labda atalala kwenye Gari

Kweli,PATA HELA TUJUE TABIA YAKO!!!!!
Hela yake ya chakula ni kubwa kuliko hela ya matumizi yote ya binadamu mwenzie hii inaonyesha tumbo lake ni muhimu kuliko maisha bora kwa mtu aliyeshikilia uhai wake!
Na Mh. Hamad Rashid wa CUF yeye kasema posho analipwa 150,000 analala hotel shiling 80,000 Anamlipa dereva wake sh 30,000/= na kula elf 40,000/= na kumaliza kwa kusema kuwa haoni kama kuna hela inabaki hapo,

Jameni, mbona Mh. Hamad hakutoa mchanganuo wa dereva wake? Posho anayomlipa ni ndogo kulinganisha na pesa anayotumia kwa chakula tu. Yeye anatumia ngapi kwenye kulala, kula na kuitumia familia yake huko kwao? Nadhani viongoz wetu wanadhan wao ndo wana haki ya kupata hivyo wanavyopata.

Hata hivyo, upinzani umetoa mawazo yao tu. Kama wangekuwa wao wanaandaa bajeti kwa ajili ya watanzania wangewafanyia nini. Sasa kuanza kuona mjadala ya kupinga mawazo yao na mapendekezo mimi nashangaa kabisa. Kwa kweli mimi sioni hata maana ya wabunge kulipwa mishahara, kwangu mimi ubunge sio fani ya mtu kujivunia hadi kustahili kupata mshahara. Ndo mana rushwa kwenye uchaguzi zinazidi kuongezeka kwani watu hufuata maslahi badala ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Its good because we now begin to know true colours of our leaders. Hawako tayari kupunguziwa maslahi yao kwa ajili ya kuwaletea wananchi ustawi ambao walijinadi kuwa wataupigania. Kiama chao kinakuja kwani 2015 sio mbali kama wanavyodhani.

2015 tutashuhudia vihoja na Mahoka ya wanasiasa wetu, mungu niweke hai nisikose vimbwanga!

siku tukipata wabunge wa CCM ambao wapo kwa ajili ya wananchi hoja kama hizi hawatozipuuza, lakini wale wapo kwa ajili ya mitumbo yao ndio maana utayaona hayo. Katika Hili mimi ningeomba media zote zitangaze hoja moja tu ya Posho kuondolewa na hoja ya chiligati abakie nayo mwenyewe na ndugai wake, naamini ikitangazwa kama vile alivotangazwa Babu wa loliondo mpaka wagonjwa wakakimbia mahospitali na kwenda kufia kule loliondo basi tutafanikiwa. Kwa vile jamaa wamejifanya vichwa ngumu ktk hili basi wabunge wa upinzani wote msirudi nyuma litekelezeni hili kwa vitendo halafu media zote ziitangaze sana tena sana kwa wananchi juu ya kinachofanywa na wabunge wa ccm ambao watang'ang'ania kuchukua posho hiyo na wawe wanatajwa majina uone kama hawaachii wenyewe, nakwambia wataanza kusutana kwahili na watakuwa wamejitengenezea picha mbovu sana kwa wapiga kura wao.

Media zimenunuliwa ndugu, na ukitangaza sana utapigwa kitu cha BAN
 
Ila katika hali ya kawaida, inawezekana kweli kwa mbunge au mfanyakazi yeyote wa serikali au wa makampuni binafsi kutoka nje ya kituo chake cha kazi for official duties bila ya kulipwa posho??? Kuwa muwazi weka siasa kando
Hatuzungumzia posho ya kuwa nje ya kituo cha kazi (perdiem), tunazungumzia posho ya vikao, hapo kuna double payment, amelipwa kwenda dodoma kuhudhuria kikao cha bunge na amelipwa kwa kukaa mjengoni, wapinzani wanachotaka iondolewa ya kukaa mjengoni maana tayari washalipwa hela ya kuhudhuria vikao vya bunge.
 
ANAKULA 40,000/= KWA SIKU DU??HUYU MUISLAM NI SOO,HII SI NI BEI YA MBUZI MKUBWA BEBERU NA KRET MBILI ZA KILIMANJARO,NA MAJI KATON MOJA KWELI JAMAA YUKO JUU

ANAMPA DEREVA WAKE 30,000/= PER DAY MAANA YAKE JAMAA ANATENGENEZA

30,000 X 30=900,000/=
SASA BUNGE HILI N LA MIEZI MITATU
900,000 X 3=2,700,000/=
MSHAHARA WA DEREVA SH 900,000/= KWA MWEZI HAIWEZEKANI

SI KWELI HUYU MPEMBA ANADANGANYA UMMA

mnafki tuu hana lolote

Hapo kwenye red hakikisheni mnapeleka wakristo kwa wingi unguja na pemba ili 2015 wasirudi hawa maana ni hatari sana.
 
Hatuzungumzia posho ya kuwa nje ya kituo cha kazi (perdiem), tunazungumzia posho ya vikao, hapo kuna double payment, amelipwa kwenda dodoma kuhudhuria kikao cha bunge na amelipwa kwa kukaa mjengoni, wapinzani wanachotaka iondolewa ya kukaa mjengoni maana tayari washalipwa hela ya kuhudhuria vikao vya bunge.

Sasa kama wameshapewa per diem zao ni busara kwa wapiga kelele kwenye majukwaa wakaandika barua ya kusudio la kuondolewa hizo posho bila ya hivyo itakuwa ni unafiki tu.
 
Fedha za Serikali hutawaliwa kwa mujibu wa Kanuni za fedha za Serikali.Kanuni hizo huelekeza stahili ya kila mtumishi anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi. Stahili ya watumishi wenye hadhi ya mbunge hivi sasa ni Shs 80,000/= tu kwa usiku mmoja anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi.

Katika kanuni za fedha za Serikali hakuna kitu kama posho ya vikao kwa watu ambao waliomba wenyewe kazi ambazo hufanyika maofisini ambapo niia mojawapo ya kutimiza wajibu wao ni kuhudhuria na kushiriki katika vikao k.m vikao vya bunge. Ikumbukwe kuwa wasomi huomba kazi za kutumia akili ambazo nyingi hufanyika maofisini kupitia vikao, mikutano, semina, warsha, kongamano n.k ndio maana husalimika na shuruba za kilimo, kazi ngumu kama vibarua n.k. Iweje wasomi hao leo wageuke na kudai kulipw posho kwa kazi ambazo wanalipwa mishahara na ambazo kwa vigezo vyote ni nyepesi na hufanyika katika amzingira mazuri kuliko kazi wafanyazo wananchi wa kawaida?

Kanuni za Ajira na Fedha za Serikali hutaja aina ya watumishi ambao wanastahili kupata wasaidizi kama vile makatibu wahutasi (Secretaries) madereva n.k. Kwa mujibu wa majibu ya kifisadi ya Mhe Hamda Rashid inaonyesha kuwa Kanuni za Ajira na Fedha za Serikali haziwatambui wabunge kuwa hadhi ya kupatiwa madereva, kama zingekuwa zinatambua hilo madereva wa wabunge wangeajiriwa na Serikali (ofisi ya bunge), na kulipwa mishahara na posho na Serikali kama madereva wa wengine wa Serikali. Toka lini ukasikia Waziri au Katibu Mkuu au Mkurugenzi wa Wizara anagawana Posho yake safari na dereva wake?.

Kinachojitokeza hapa ni kuwa wabunge wetu wanajikweza sana pasipo kutazama umasikini wa wapiga kura wao ndio maana wanakuwa na mahitaji makubwa ya kuhitaji dereva n.k. Ofisi ya bunge inamiliki idadi kubwa ya mabasi kwa ajili ya kuwasafirisha wabunge kwenda na kutoka katika vikao vya bunge kutokea ofisi za bunge; ambapoi kutokea hapo wabunge wanatakiwa kutumia usafiri wa umma kama vile treni, mabasi n.k ili kujua hali halisi ya usafiri wanaotumia wananchi.

Ni kwanini kila mbunge apige gari moto kuelekea Dodoma? kama sio ufujaji wa fedha za walipa kodi. Ndio maana wabunge wanajiingiza katika ufisadi wa posho mbili mbili ili kumudu maisha haya ya anasa.

Ndio maana wabunge waroho kama Mhe Hamad Rashid na wenzake wote wanaotetea utaratibu huu wa kifisadi wanalazimika kutetea wizi wa fedha za serikali kwa njia ya posho za vikao ili kufidia masiha ya anasa ya wabunge wetu.

Nimekuelewa saaaaana!, Na hivo ningeomba kama kuna mtu amabae anaweza kutupatia hizo kanunu tafadhali afanye hivo coz huenda hata hiyo 150000 wanayopata wameingiza na mambo yao wenyewe kama bwana rashidi anavosema!,

Au kama mdau unaweza kutuwekea hapa hizo sheria weka! nitafurahi sana!
 
Wakuu natanguliza samahani kwa nitakayemkwaza lakini ukweli katika hili siwaelewi viongozi wa vyama vya upinzani including CHADEMA kama wako serious! Hivi wanashindwa nini kususia posho hizo za wabunge??? Je kisingizio ni kwa sababu wakiacha CCM wanachukua?? If yes, Je inaleta mantiki yoyote??

Kama CCM wanaziiba, (na of course ndivyo ilivyo) je wao wanaona wakiziacha watakuwa wamewasusia CCM na hivyo bora na wao waziibe??? Jamani, hili linanikoseha raha na kunipa wasiwasi kama kweli dhamira yetu ya kuikomboa nchi hii inadhihirshwa hasa na tunachokisema na kukikariri kila siku.

Najua CCM hawataruhusu kuziondoa hizo posho ambazo sisi tunaamini kuwa ni kuwaibia wananchi wanyonge wa nchi hii!! Sasa je, kwa sababu CCM watakataa basi na wabunge wa CHADEMA wazichukue!!! Gosh!! Why?

Hoping that two blacks will eventually make white??? TUACHE UZEMBE!!! NA TUMAANISHE KWA DHATI TUNAPOSEMA TUNA DHAMIRA YA KUMKOMBOA MWANANCHI ALIYEKATA TAMAA KUTOKANA NA UONEVU WA SERIKALI YA KIKWETE!!!! Viongozi wetu tunaomba mtutoe mashaka na kulifanunua hili!

Naanguliza shukurani kwa viongozi watakaochukua hatua kulifafanua kwa makini suala hili.
 
Mbona Ndugai kakurupuka, ameongea kama mbunge au kama naibu spiker. Maana kama naibu spiker hawezi kuanza kuponda hoja ya mbunge kwa kuwa ni haki ya mbunge kupeleka hoja binafsi,na yeye kama naibu spiker hatakiwi kuelemea upande wowote.
 
Hapo kwenye red hakikisheni mnapeleka wakristo kwa wingi unguja na pemba ili 2015 wasirudi hawa maana ni hatari sana.

Post ya huyo jamaa haijatulia na wala sijaipenda kuingiza udini ila sometimes unaweza kuignore tu itakusaidia, sasa pia ulichoandika sio sahihi mkuu, na machonkwangu havinipendezi, Especially udini
 
Sasa kama wameshapewa per diem zao ni busara kwa wapiga kelele kwenye majukwaa wakaandika barua ya kusudio la kuondolewa hizo posho bila ya hivyo itakuwa ni unafiki tu.

Wapiga kelele ni akina nani mkuu!??
 
Pale walimdunga swali, infact nilichoona hakulipenda swali na kusema tunasubiri walete hoja bungeni!
 
Hapo kwenye red hakikisheni mnapeleka wakristo kwa wingi unguja na pemba ili 2015 wasirudi hawa maana ni hatari sana.
Mkuu Shossi huyo jamaa aliyeingiza udini msamehe bure tu, sie tuzungumzie je ni haki hawa watu kupata posho mbili kwa kazi moja?
 
Wakuu natanguliza samahani kwa nitakayemkwaza lakini ukweli katika hili siwaelewi viongozi wa vyama vya upinzani including CHADEMA kama wako serious! Hivi wanashindwa nini kususia posho hizo za wabunge??? Je kisingizio ni kwa sababu wakiacha CCM wanachukua?? If yes, Je inaleta mantiki yoyote?? Kama CCM wanaziiba, (na of course ndivyo ilivyo) je wao wanaona wakiziacha watakuwa wamewasusia CCM na hivyo bora na wao waziibe??? Jamani, hili linanikoseha raha na kunipa wasiwasi kama kweli dhamira yetu ya kuikomboa nchi hii inadhihirshwa hasa na tunachokisema na kukikariri kila siku.

Najua CCM hawataruhusu kuziondoa hizo posho ambazo sisi tunaamini kuwa ni kuwaibia wananchi wanyonge wa nchi hii!! Sasa je, kwa sababu CCM watakataa basi na wabunge wa CHADEMA wazichukue!!! Gosh!! Why? Hoping that two blacks will eventually make white??? TUACHE UZEMBE!!! NA TUMAANISHE KWA DHATI TUNAPOSEMA TUNA DHAMIRA YA KUMKOMBOA MWANANCHI ALIYEKATA TAMAA KUTOKANA NA UONEVU WA SERIKALI YA KIKWETE!!!! Viongozi wetu tunaomba mtutoe mashaka na kulifanunua hili!

Naanguliza shukurani kwa viongozi watakaochukua hatua kulifafanua kwa makini suala hili!
una analyse kwa kutumia makalio
kinachoongelewa ni mfumo.Mfumo ambao utajaribu kuleta usawa na sio kususiwa kwa posho
 
Wabunge wa CHADEMA sio kuwa wao hawazitaki hizo posho, hapo ndio watu mnaposhindwa kuwaelewa. Hakuna asiye taka pesa. Ila wao wanapigania mfumo mpya utakao ondoa hizo sitting allowance ili fedha hizo ziweze kufanya majukumu mengine ya manufaa.
Ukiliangalia hili kwa pupa utaona ni jambo la mzaha,ila kama Bunge litajiondolea posho za aina hiyo ina maana hakuna idara au wizara ambayo fedha za aina hiyo zitapitishwa na Bunge tena. Tutaokoa ngapi kama taifa? NYINGI. Kususia sio ufumbuzi wa tatizo
 
Post ya huyo jamaa haijatulia na wala sijaipenda kuingiza udini ila sometimes unaweza kuignore tu itakusaidia, sasa pia ulichoandika sio sahihi mkuu, na machonkwangu havinipendezi, Especially udini

Hapa hakuna udini ukitajwa ukristo wala uislam, ni dalili ya kukimbia hoja waelewe.
 
Sasa kama wameshapewa per diem zao ni busara kwa wapiga kelele kwenye majukwaa wakaandika barua ya kusudio la kuondolewa hizo posho bila ya hivyo itakuwa ni unafiki tu.
Mimi nadhan tungekuwa wa kweli tu, ofisi kubwa ya mwanasiasa makini ni jukwaani, sidhan kama kuna dhambi kuyasemea mambo hayo jukwaani, kama hoja ni kuandika barua tu basi hakuna haja ya kukaa bungeni waandikiane barua tu mambo yote yajadiliwe kwa barua.

Hata kama mnawapenda wabunge hawa wengi wao ni watu ambao hawajali wananchi wao, Mtu kama Rashid Mohamed ambaye mimi namheshim na kumkubali kama mbunge makini ila kwa hili alilosema lazima nimpunguzie credit naona kama amekurupuka pengine ni hasira za kukosa ukuu wa kambi ya upinzani.
 
Nafikiri wewe ni mmoja wa watu ambao hudandia mada bila ya kuzisoma kisawasawa. Alichosema Mhe Zitto ktk bajeti ya kambi ya upinzani ni kuwa wabunge hulipwa posho za aina mbili kwa siku, ya kwanza inayitwa Sitting Allowance ya SHS 80,000/= kwa ajili ya kukaa katika vikao vya bunge; na ya pili ni posho ya kujikimu kwa lugha ya kigeni huitwa "Subsistence Allowance" ya Shs 70,000/= kwa ajili ya chakula, malazi n.k kwa kuwa viako vya bunge hufanyika nje ya vituo vyao vya kazi kwa maana ya maimbo yao ya uchaguzi. Ndipo akahoji uhalali wa mbunge kulipwa posho ya kukaa katika vaikao vya bunge ilihali kazi aliyoomba ni kuwawakilisha wananchi katika bunge na tayari analipwa mshahara kwa kazi hiyo hiyo.

Hivyo bajeti ya upinzani inapendekeza posho ya kujikumu iendelee na posho ya kukaa katika vikao vya bunge iondolewe. Vivyo hivyo kwa kwa watumishi wa serikalini hususan wakubwa wakikaa katika vikao mwisho hupitishwa bahasha zenye posho ilihali waliomba wenyewe kazi za kutumia akili katika vikao ndio maana hawafanyi kazi za shuruba kama vile kilimo, vibarua n.k. Kiutendo cha watumishi wa serikali tena wa kada ya juu tu, kulipwa posho ya kutimiza wajibu wao ambao tayari wanalipwa mishahara kuutimiza ni ufujaji mkubwa wa fedha za walipa kodi. Ndio maana vikao serikalini haviishi. Kinachotokea wanapanga vikao kufanyika katika mikoa nje ya vituo vya kazi na kupata posho mbili kama wabunge yaani posho ya vikao na posho ya kujikimu.

Je hiyo ndio siasa kwako?

You said it all!

Unajua humuhumu JF na sisi wengine tunakuwa tunajadili hoja tusiyoielewa. Kwa mtu aliyeilewa hoja ya ZItto na kama ilivyofafanuliwa hapa na Mheshimiwa Watanabe ataona kuna point ya wazi kabisa kwamba wabunge na watumishi wa umma wanatuibia!

Hawa wabunge wanaopinga hoja hii wanajaribu kujifanya hawajaielewa na kuchukulia kwamba Zitto anaongelea habari ya posho zote ili kuwalaghai wananchi. It is very clear that the MPs and public servants are extravagant.

Hii posho ndiyo inayofanya kazi haziendi mofisini watu wako bize na vikao na semina zisizo na kichwa la miguu, simply kwa ajili ya bahasha.
Lazima tuupinge huu mfumo sisi tunaofanya kazi private hakuna kitu kama hiki na kazi zinafanyika kwa ufanisi zaidi na mikutano ni mingi tu lakini ni ya manufaa.
Watumishi walipwe mishahara stahili na wafanye kazi siyo kukalia semina na mikutano isiyo na tija. Mbaya zaidi ni kwmba wakubwa ambao ndo wenye mishahara mizuri ndo pekee wanafaidika na hii posho maana ndo wahudhuriaji wa vikao na semina. Watumishi wa chini wenye mshahara kiduchu hakuna cha semina wala kikao na matokeo yake wanakuwa hawana molari wanaanza kuchukua rushwa za kijinga tu.
Tumesikia mabosi wengi wanajipangia kwenda training ambazo hazimo kwenye job description zao badala ya subordinates wao ili tu wapate poshoi!

Shame on you Magamba MPs and your rotten Government !
 
Wapiga kelele ni akina nani mkuu!??

Wale wabunge wanaozungumzia posho za ubunge kwenye vyombo vya habari wakati wanaendelea kila siku kuzipokea au wakikosa ubunge wanalazimisha wapewe mishahara minono ya kibunge. Tumekwisha lisikia hili kwa muda mrefu tunataka waanze utekelezaji wake mara moja. Wazipokee kisha watoe kiwango kinachozidi wachangie hazina au hata vyama visvyopata ruzuku.
 
Back
Top Bottom