Pongezi kwenu Single Mothers
Hammer11

Maisha kwa sasa ni magumu kea mfano sio rahisi eti mzazi mwenzie atoke arusha aje mara kwa mara kumtafuta mkeo labda tabora ili amtafune...mostly wanakuwaga wamegombana so ni wanawake wachache wenye hulka za umalaya huo

Hint

1.mbadilishie line wasiwe na mawasiliano
2.akitaka kuja kumuona mtoto basi mtoto apelekwe kwa ndugu zake wemgine akamuonee hukohuko
 
Inategemea, kuna wanawake hata ex akiwa jaribu hawarudi tena kwake. Mara nyingi akiwa aliumizwa sana nae basi huyo hatamrudia, ila ikiwa mengine kusali tu.
 
UMEZALISHWA, UKATELEKEZWA. SASA UNAITWA SINGLE MOTHER. FANYA HAYA:

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwèñye Maisha mambo meñgi usiyoyatarajia Wala kuyajua huweza kukutokea. Hata usiamini kwamba kweli yamekutokea. Wala usijali. Hayo ndîo Maisha.

Ikiwa ikatokea umezalishwa kibahati mbaya, au kimakusudi ukaamua kubeba Mimba, au uliolewa ukazaa m/Watoto lakini ikatokea mkaachana na huyo Mwanaume akakuacha au ukamuacha au mkaachana.

Íwe Kwa uzembe na Makosa yako au íwe Kwa uzembe na Makosa Yake. Sasa unaitwa Single mother. Mwanamke mwenye m/Watoto na Kwa Bahati mbaya zaidi Mwanaume akawa hawajibiki kuangalia m/Watoto wake mliozaa pàmoja. Íwe haangalii Kwa sababu yoyote Ile íwe ni Kwa sababu umemuudhi Kwa ukorofi na tàbia zako mbaya au ukorofi au tàbia Zake Mbaya.

Yaani Kwa lugha nyepesi umekuwa single mother aliyetelekezwa.
Basi Mimi Baba yako, ndiye Mtibeli nakuambia haya na unisikilize Binti yàngu;

Fanya haya ukiwa katika Hali hiyo:

1. Kubali ukweli;
kuwa wewe siô kama Wanawake Wengine àmbao Hawana Watoto Kabisa.
Hivyo ni ngumu Kwa Wanaume wengi kukubali kuwa na wéwe, kukuoa.
Huo ni ukweli na ni Haki Yao kukuona hivyo. Hivyo usijisikie vibaya.
Ukweli utakusaidia kutokujidanganya na kudanganywa na Wanaume Wengine hasa waovu àmbao watatumia Hali yako kukufanya ujione upo Sawa na Wanawake Wengine Wakati huo ni Uongo. Lengo Lao ni Kukutumia

2. Usimlaumu yeyote Wala kujilaumu.
Íwe ulikosea au ulikosewa. Huna haja ya kujilaumu Wala kulaumu Wengine.
Jisamehe Kisha jikubali vile ulivyo. Msamehe aliyekutelekeza au kaombe Msamaha kwa aliyekutelekeza.

3. Jitegemee. Beba Majukumu yako mwenyewe.
Tafuta Kazi kama ulikuwa hauna. Punguza mahitaji na matumizi yasiyo ya lazima yaendane na Hali yako.
Usimpe yeyote mzigo wako. Beba Msalaba wako mwenyewe. Jitunze na tunza Watoto wako.

Jinsi ya kujitegemea ukiwa Kama single mother;
a) Fanya Kazi Kwa bidii.
Kazi yoyote halali inayokufanya uishi.
b) Kula Vizuri.
Ukifanya Kazi utapata pesa, hiyo Pesa hata íwe ndogo vipi hakikisha unakula unashiba wewe na Watoto wako.
Kula Vizuri siô gharama Sana. Kula ni Sanaa na uwezo wa kubajeti Pesa utakayopata.
Kula Vizuri itakusaidia kuwa na Afya Njema na mvuto. MVUTO utalinda utukufu wako kama Mwanamke. Usikubali kuchoka.
Usitumie Pesa nyingi Saluni. Bora hizo pesa za Saluni uziingize kwèñye bajeti ya msosi weñye lishe Bora. Lishw bora itakusaidia kuwa na Mwili mzuri na urembo utazidi kuchomoza.

c) Toa zaka na sadaka
Saidia Watu waliochini yako. Kama huamini katika Dini. Tenga fungu la Kumi kwaajili ya wahitaji kama wajane wasiojiweza, mayatima, chokoraa na mtaani, au wafungwa.

d) ongeza ujuzi na maarifa.
Hakikisha unaongeza maarifa na kukuza Fikra zako, uwezo wako WA Kazi unaoifanya, ujuzi Mwingine kama kusuka, Kushona, Kupika, Kwa namna ya biashara.

e) jiunge na jumuiya Zenye maadili hapo mtaani.
Jiunge na vikundi vya Wanawake vyenye maadili. Kama ni Mkristo jiunge na vikundi vya Wanawake vya Kanisani vyenye maadili.
Kama ni muislam halikadhalika.

Usikubali ukatumika nguvu zako, Akili zako, Pesa yako sehemu àmbayo haina tija. Usikubali Mtu yeyote akakutumia Kwa maslahi yake Bila wewe kunufaika. Kwèñye hizô jumuiya íwe NI mtaani, Kanisani, msikitini au vyovyote.
Ndîo maana nikakuambia ongeza MAARIFA na hakikisha Akili yako inachaji.

Ujuzi usiouhitaji usiulipie. Jambo lolote ambalo halikufurahishi usilitolee Pesa yako hata Kama ni Kanisani au msikitini.
Usikubali kuambiwa wewe toa tuu Pesa utabarikiwa. Nop!
Toa Pesa pale unapoguswa Moyoni.
Sadaka ya kulazimishwa hainaga Baraka, sadaka ya kushawishiwa hainaga Baraka.
Toa sadaka Ikiwa Moyoni unaguswa kufanya hivyo.

4. Usigombane na Mzazi mwenzako Kwa maslahi ya Watoto wako.
Mmeshaachana, Haitakusaidia kitu kugombana naye.
Mtoto au Watoto wako kûna kitu kikubwa watakihitaji Kwa Baba Yao. Na mwenye uwezo wa kukifanya kitu hicho Watoto wako wakipate ni wewe mwenyewe.

Watoto watahitaji Baraka za Baba Yao àmbaye wewe ulikuwa mwenza wake au ulizaa naye kibahatibahati.
Tumia Akili.
Huenda ni kweli haupendezwi na tàbia ya Mzazi mwenzako au huenda wewe mwenyewe ndîo unamatatizo lakini vyovyote iwavyo hakikisha watoto wako Wapate Baraka za Baba Yao.

Namaanisha, Baba yao asiwe na kinyongo na Watoto uliowazaa wewe. Wala Mtoto asiwe na kinyongo na Baba yake. Hapo Maisha ya Mtoto yatakuwa salama. Hata kama Baba asimpomtamkia Baraka Mtoto.
Mwambie Mzazi mwenzako Watoto wake wanampenda na wanatamani sana kumwona.

Mwambie, unaamini kuwa Hata yeye anawapenda Watoto wake semà mambo yake hayajakaa Sawa. Mwambie asijali kwani Mungu ndiye anayejua.

5. Usiwaabudu WATOTO.
Binti yàngu, Kwanza usimuabudu yeyote isipokuwa Mungu. Ninaposema usiabudu namaanisha usimtegemee yeyote. Wala usimtumainiye yeyote kuwa ndiye tegemeo Lako.

Usiwakuze Watoto wako ili waje wakusaidie baadaye. Unawapa Laana Bila ya wewe Kujua.
Wewe ni Mama. Jukumu Lako ni kuzaa na kulea Watoto àmbao tayari umetelekezewa.

Kulea Watoto ukiwa unawategemea kuwa watakuwa msaada kwako baadaye ni kupanda Mche wa maumivu àmbao Miaka mingi ijayo utakuja kuyala matunda Yake wewe na haohao Watoto.

Mtegemee Mungu, Kisha Fanya wajibu wako. Mungu yeye ndiye anayejua na ndiye anayeandaa msaada wako pindi utakapopatwa na shida. Kumuandaa mtoto kama sehemu ya KUKUSAIDIA Huko baadaye ni kuongeza tatizo zaidi.

6. Ongeza na Linda Thamani na heshima yako
Kuwa Mtu pekee haitoshi kuwa na heshima na thamani. Kûna wajibu unatakiwa ufanye ili uzidi kuheshimiwa na kuongeza thamani yako.

Usilale lale hovyo na kîla Mwanaume kama Mbwa.
Epuka Kulala na Vijana wadogo uliowazidi umri zaidi miaka 10 unajitia aibu na kudhalilisha Watoto wako.

Epuka kuombaomba Pesa na kupewa misaada.
Epuka kujihusisha na Watu wa hovyo yàani kuwaweka Karibu ila haimaanishi uwatenge.

Epuka kufanya Kazi za aibu na kudhalilisha Ûtu wako.
Epuka kuongea ongea maneno ya kishakunapu na matusi.
Epuka kuvaa nguo za kukudhalilisha.

Epuka kudhurura hovyo mitaani pasipo mpàngo maalumu.
Epuka kushinda Bar au kwèñye masaluni Kúpiga umbea.

Epuka kuzozana zozana na Watu mtaani.
Epuka matani na Watu hovyohovyo. Wewe siô Mwanaume. Sisi Baba zako ndîo tunataniana na kuwa na jokes hata za hovyohovyo.

7. Ikiwa utapata Mume mwambie wazi Hana wajibu wa kuwafikiria Watoto aliowakuta. Ila humzuii kukusaidia kama vile wewe utakavyosaidia Watoto wake.

8. Epuka Kúpigania Mali za Mwanaume atakayekuoa Ambazo ulizikuta. Hiyo ni dhulma. Labda upewe Kwa Upendo tuu.

9. Andaa Watoto wako kuwa wake na waume Wazuri.
Kamwe usihamasishe kuishi bila Ndoa.
Watoto wajifunze tàbia Njema kupitia wanavyokuona.
Hawatakuwa na sababu ya kukuuliza Kwa nini wewe NI single mother alafu unawataka waô wawe kwèñye Ndoa kwani tàbia zako zitakuwa Majibu tosha.

10. Waandalie Watoto Urithi.
Akili yako Ikiwa na wazo la kuwaachia Watoto wako Urithi itakuchochea kuzidisha juhudi za kufanya Kazi na kuweka Akiba. Kisha kuandaa Urithi Kwa Watoto wako.

Hivyo ndîvyo Binti za Tibeli hufanya pale àmbapo Bahati mbaya ya kutelekezwa na kuwa single mother inapowatokea.
Huna haja ya kuwa Feminists.

Kutetea haki zako binti yàngu ni kufanya wajibu wako na kujitegemea.
Huwezi pigania Haki zako alafu unamtegemea mtu Mwingine.

Acha nipumzike sasa
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imeona kuongezeka kwa idadi ya wanawake ambao ni mama wanaolea watoto pekee( Single Mother).
Hali hii inaathiri jamii kwa namna nyingi, ikiwa ni pamoja na kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni. Katika makala hii, tutajadili chanzo na sababu za ongezeko hili, suluhisho zinazoweza kupatikana, na wajibu wa jamii na serikali katika kushughulikia tatizo hili.

Chanzo na Sababu za Ongezeko la Mama Wanaolea Watoto Pekee(single mother)

1. Mabadiliko ya Kijamii: Moja ya sababu kubwa za ongezeko la mama wanaolea watoto pekee ni mabadiliko ya kijamii. Katika jamii nyingi, wanawake wanapata fursa zaidi za elimu na kazi, hivyo kuamua kuwa na watoto bila kuolewa. Hii inazidisha idadi ya wanawake ambao wanajikuta wakilea watoto peke yao.

2. Ukatili wa Kijinsia: Ukatili wa kijinsia na unyanyasaji ni tatizo kubwa katika jamii nyingi. Wanawake wengi wanaweza kukimbia katika ndoa zenye ukatili, na hivyo kujikuta katika hali ya kulea watoto pekee.

3. Mifumo ya Mazingira: Katika maeneo mengi, mifumo ya kijamii inaweza kuwa na vikwazo kwa wanawake wanapojitahidi kupata msaada. Wakati mwingine, wanawake hawawezi kupata huduma bora za afya na elimu, hali inayowafanya wajikute katika hali ngumu.

4. Mabadiliko ya Kiuchumi: Uchumi wa nchi unakabiliwa na changamoto nyingi, na hii inawafanya wanawake wengi kushindwa kupata ajira nzuri. Hali hii inawafanya wajikute katika hali ngumu ya kulea watoto peke yao bila msaada wa kifedha.

Suluhisho

1. Elimu na Uhamasishaji: Ni muhimu kuendelea kutoa elimu kuhusu haki za wanawake na umuhimu wa usawa katika ndoa. Jamii inapaswa kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa kusaidia wanawake na watoto wao, ili kuweza kujenga mazingira bora ya kulea watoto.

2. Huduma za Kijamii: Serikali inapaswa kuimarisha huduma za kijamii kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na huduma za afya, elimu, na msaada wa kifedha. Hii itawasaidia wanawake kuweza kujimudu kiuchumi na kijamii.

3. Ulinzi wa Kisheria: Ni muhimu kuwepo na sheria zinazowalinda wanawake dhidi ya ukatili na unyanyasaji. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa sheria hizi zinatekelezwa ipasavyo ili wanawake waweze kujihisi salama katika jamii.

4. Mfuko wa Msaada: Kuanzishwa kwa mifuko ya msaada kwa wanawake wanaolea watoto pekee kutawasaidia kupata rasilimali zinazohitajika. Hii inaweza kuwa katika mfumo wa mikopo ya riba nafuu au msaada wa moja kwa moja.

Wajibu wa Jamii na Serikali

1. Jamii: Jamii ina wajibu wa kubadilisha mtazamo kuhusu wanawake wanaolea watoto pekee. Ni muhimu kuondoa unyanyapaa na kuwasaidia wanawake hawa kwa njia mbalimbali, kama vile kutoa msaada wa kifedha au huduma za kijamii.

2. Serikali: Serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa sheria zinazowalinda wanawake zinakuwepo na kutekelezwa. Aidha, inapaswa kuwekeza katika elimu na huduma za afya ili kuweza kusaidia wanawake na watoto wao.

3. Mashirika Yasiyo ya Kiserikali: Mashirika yasiyo ya kiserikali yanaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa kutoa elimu na msaada kwa wanawake. Haya yanaweza kuanzisha programu za uhamasishaji na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake.

Hitimisho

Tatizo la ongezeko la mama wanaolea watoto pekee ni changamoto kubwa inayohitaji kushughulikiwa kwa umakini. Kwa pamoja, jamii na serikali wanaweza kufanya kazi kwa karibu ili kuleta mabadiliko chanya. Kwa kutoa elimu, msaada wa kifedha, na kulinda haki za wanawake, tunaweza kusaidia kuboresha maisha ya wanawake na watoto wao, na hivyo kujenga jamii yenye nguvu na yenye usawa.
 
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Unaambiwa katika dunia kila kitu kina hasara na faida. Hivyo kabla ya kufikilia kufanya unashauliwa kuangalia pande zote mbili yaani (ADVANTAGE na DESADVANTAGE ) kimombo changu kinaweza kisiwe sawa ni kutokana na kiwango chagu cha elimu.

Basi bwana ndugu msomaji leo ngoja nikupe Hasara za kuoa mwanamke mwenye mtoto/watoto ambao si wa kwako.

Hapa nitazungumia wale watoto/mtoto ambao bado ni wadogo, na hata kama wakubwa ni wale watoto ambao bado hawajiwezi. Yaani wahitaji uangalizi wa mama na baba ili waweze kusavaivu.

1. UPENDO
Kwa asilimia kubwa wamama wengi wenye watoto wadogo upendo wao huwa kwa watoto wao kwanza alafu ndio mumewe.

Hii hujibadilisha na kuwa zarau kwako mume, mfano mtoto analilia kuoga na wewe unahitaji chakura kwa mda huo huo mmoja, amini amini nakueleza anaanza shughulika na mtoto wake kwanza huku ukiachwa umeduaa.

2. WAZAZI WENZAO
Hapa ndio kwenye mtihani mkubwa kuliko ule wa kwanza.
Nikisema wazazi wenzao namaanisha mababa rasmi wa watoto tunaowaongelea.

Hawa mababa ndugu yangu huwaga wabishi sana kuelewa tena ukifanya masihara utaacha mke hivihivi. Umelala na mke wako usiku jamaa atapiga simu, mchana mkeo yupo jikoni jamaa atapiga simu na mke ataongea nae huku simu IMEBANWA SIKIONI NA BEGA huku akiendelea kupika au kufua.

Ukijaji sana utawekewa na loud spika kabisa ili umsikie mwanaume mwenzio.

3. HUDUMA ZA MTOTO/WATOTO
Hapa kuna mambo mawili ambayo yote ni mabaya.

!) Uwahudumie watoto kwa kila kitu mpaka ukubwa wao

!!) Baba yao mzazi awe anahudumia watoto wake.

!!) Je atakuwa anahudumia kwa mfumo upi?

!) kuwasiliana na wewe
!!) kuwasiliana na mama watoto moja kwa moja?

Na je uaminifu utatoka wapi?

Nilale mie
🚪🛏️🛋️
 
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Unaambiwa katika dunia kila kitu kina hasara na faida. Hivyo kabla ya kufikilia kufanya unashauliwa kuangalia pande zote mbili yaani (ADVANTAGE na DESADVANTAGE ) kimombo changu kinaweza kisiwe sawa ni kutokana na kiwango chagu cha elimu.

Basi bwana ndugu msomaji leo ngoja nikupe Hasara za kuoa mwanamke mwenye mtoto/watoto ambao si wa kwako.
Hapa nitazungumia wale watoto/mtoto ambao bado ni wadogo, na hata kama wakubwa ni wale watoto ambao bado hawajiwezi. Yaani wahitaji uangalizi wa mama na baba ili waweze kusavaivu.

1. UPENDO
Kwa asilimia kubwa wamama wengi wenye watoto wadogo upendo wao huwa kwa watoto wao kwanza alafu ndio mumewe.
Hii hujibadilisha na kuwa zarau kwako mume, mfano mtoto analilia kuoga na wewe unahitaji chakura kwa mda huo huo mmoja, amini amini nakueleza anaanza shughulika na mtoto wake kwanza huku ukiachwa umeduaa.

2. WAZAZI WENZAO
Hapa ndio kwenye mtihani mkubwa kuliko ule wa kwanza.
Nikisema wazazi wenzao namaanisha mababa rasmi wa watoto tunaowaongelea,
Hawa mababa ndugu yangu huwaga wabishi sana kuelewa tena ukifanya masihara utaacha mke hivihivi,. Umelala na mke wako usiku jamaa atapiga simu, mchana mkeo yupo jikoni jamaa atapiga simu na mke ataongea nae huku simu IMEBANWA SIKIONI NA BEGA huku akiendelea kupika au kufua.
Ukijaji sana utawekewa na loud spika kabisa ili umsikie mwanaume mwenzio.

3. HUDUMA ZA MTOTO/WATOTO
Hapa kuna mambo mawili ambayo yote ni mabaya
!) Uwahudumie watoto kwa kila kitu mpaka ukubwa wao
!!) Baba yao mzazi awe anahudumia watoto wake.
!!) Je atakuwa anahudumia kwa mfumo upi ?
!) kuwasiliana na wewe
!!) kuwasiliana na mama watoto moja kwa moja?
Na je uaminifu utatoka wapi?

Nilale mie
🚪🛏️🛋️
Ni chakula mkuu sio chakura*
 
Mimi nimeoa mwanamke mwenye wajukuu.
 
(ADVANTAGE na DESADVANTAGE ) kimombo changu kinaweza kisiwe sawa ni kutokana na kiwango chagu cha elimu.
Wala usianze kujistukia, wewe andika tu, sisi tutajua tu kiwango chako cha elimu baada ya kusoma ulichoandika.

Kwa hiyo usijistukie tutajua tu kama ni mbivu ama ni mbichi
 
Back
Top Bottom