Uchaguzi 2020 Polisi ihakikishie vyama vya siasa kuwa utekwaji wa mawakala hautakuwepo na Tume iwahakikishie haita waengua bila kufuata sheria na taratibu

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Kuanzia mchakato wa kuwateua Wabunge na madiwani na kukiuka maadili ya chama mengi yameshuhudiwa na malalamiko kwa tume ni mengi sana ambayo hayajajibiwa hadi leo. Maswali ni mengi na imekuwa kama siri, sasa kama tume inafanya siri sisi wananchi tutaiamini au ni njama za upendeleo. mfano wa maswali ambayo hayajawahi kujibiwa ni yafuatayo:

1. Kwenye ratiba zote za uchaguzi kutoka tume Hakuna sehem imemuonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa atakuwa na Mkutano wa Kampeni kupitia chama tawala, ratiba hiyo inamuonyesha Mgombea Urais na Mgombea Mwenza tu. Majaliwa anatokea wapi kufanya kampeni nchi nzima akiwa hana mamlaka hiyo. Malalamiko wanayo tume na haijaawhi kujibu hili.

2. Kura zitakazo pigwa tar 27, nani atakayelinda masanduku hayo ya kura usiku wa tar 27 hadi kufikia tar 28 ili kura zote zihesabiwe kwa pamoja.

3. Kwenye stoo za Box tupu za kura wameweka Polisi kuwa walinzi wa box hizo na usiku wa tar 27 baada ya watumishi kupiga kura tume itawahakikishiaje wa tanzania kuwa box hizo hazitabadilishwa na kuwekwa zingine nani atakayekuwa anazisindikiza kutoka kituoni hadi zitakapo hifadhiwa, hiyo ni mali ya watanzania tayari kwann wenye vyama wasilale nazo wakiwa na polisi na asubuhi wasindikize kwenye kuzirudisha kwenye kituo kwa ajili ya kuhesabiwa.

4. Tume inawahikikishiaje vyama vya siasa kuwa hakutakuwa na uzembe kwa watumishi wao kwa kufanya makusudi kuwahengua na kutengeneza watu wa kuwasilisha pingamizi ya wasimamizi, na hakutakuwa na kuwahengua kwa matakwa yao ya kutaka kuwabeba chama flani.

5. Kazi ya polisi ni kuwalinda raia na mali zao, je wako tayari kuihakikishia tume kuwa maswala ya kuwateka wasimamizi hayata tokea kamwe na watadhibiti?

6. Je, tume itakuwa tayari kuwateua wengine endapo watakaokuwa wametekwa hawataonekana kabisa maana huu mpango huwa unasukwa ki aina wanao ujua ni wale wanao panga njama.

MUNGU BARIKI UCHAGUZI HUU UWE WA HAKI NA AMANI
 
Tume ya uchaguzi mmetangaza mawakala kuapishwa siku 7 kabla ya uchaguzi, kwanini msiwaapishe katika maeneo yao ya kusimamia siku hiyo kabla ya uchaguzi kuanza.

Hawa wasimamizi ndani ya siku 7 wakiapishwa na wakianza kupotezwa yani kutekwa mnataka mtupe majibu kuwa hamna muda mwingine wa kuwaapisha mawakala kama wakala hajatokea basi ili mruhusu yafanyike ya kufanyika.

Kusema ukweli mnadhambi kubwa sana, mnataka muoshe mikono yenu kuwa sio jukumu lenu kuwapa ulinzi mawakala? kinacho tengenezwa ni dhambi kubwa sana.

MUNGU IPONYE TANZANIA
 
Yaani katika mkeka ambao Unaweza kubeti na kula ni huu (Kuwa mawakala watatekwa na watanyiwa fomu za utambulishi) sijui why makampuni ya kubeti hayajaweka hii kitu.
 
Back
Top Bottom