Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,125
4,168
Alikuta taifa lake likiwa na uharifu mkubwa sana alipoingia madarakani mwaka 2016. Wauza unga walikuwa wengi, wakabaji wa kutumia siraha na majambazi.

Alitumia njia moja tu kama mkuu wa vyombo vya ulinzi. Mhalifu mwenye silaha awe kibaka, muuza unga au jambazi akiwa na silaha frontline ni kula risasi tu.

Hawa vijana wanatembea na mapanga na kukata watu kama wanakata miti ni kuwachapa risasi
halafu mnaita wazazi wao kubeba maiti.

Leo hii Uhalifu umepungua sana huko Phillipines. Hii ni kwa sababu wahalifu sio wa kuchekea.
 
Style hiyo ni nzuri. Ila shida ya mfumo wetu wa Africa wanaweza kuuliwa watu wasio na hatia kisa tu una beef na mtu fulani akakuchomea kwa Police au whatever itakavyo kuwa.

Nashauri wale risasi baada ya mahakama kutoa hukumu kuwa wanahatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu mm hawa ni wale watoto walokosa malezi ya wazazi wao ama kuzembea kwenye ulezi au watoto wa mitaani.

Lakini kubwa ni hili jambo ambalo watu wanaliona ni la kawaida ni jambo la Zinaa au kuzaa nje ya ndoa. hili jambo kiukweli linasababisha street children wengi mno hlf jamii wala haijali kuhusu ilo jambo ndo kwanza linashabikiwa mno.

Watoto wa Mitaani ambao hutelekezwa na Wazazi wao hasa hawa wa nje ya ndoa ndo hua wanaishia hivi lkn Kumbe maangamivu tunayasababisha sisi wenyewe hlf tunakaa tunalaumu Uongozi. Tukitaka kubadilika kwanza tuanze kubadilisha yaliyomo kwenye nyoyo zetu ndipo Mungu nae atatuongoza .

Naomba kuwasilisha mawazo yangu.
 
Style hiyo ni nzuri. Ila shida ya mfumo wetu wa Africa wanaweza kuuliwa watu wasio na hatia kisa tu una beef na mtu fulani akakuchomea kwa Police au whatever itakavyo kuwa.

Nashauri wale risasi baada ya mahakama kutoa hukumu kuwa wanahatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo sheria ya kuwapiga risasi vibaka haipo Tanzania. Pia kuua kwa risasi bila kufuata sheria ni mob justice. Binafsi ninaamini watanzania kuna mahali tumekosea kwa ujumla wetu, kuanzia kwa viongozi wa juu wa kisiasa mpaka kwenye ngazi ya familia.

Hao panya road ni watoto waliozaliwa na wazazi watanzania au tuamini kuwa ni wavamizi kutoka nje ya nchi? Hawa ni watanzania wenzetu wanaolindwa na sheria hizi hizi tulizotunga kwa ajili yetu. Tusiwahukumu kabla ya kuangalia tulipokosea.

Baada ya kukosea katika malezi na kupuuza uwepo wao kati yetu, tukiwashuhudia wakikua wakirandaranda mitaani bila uelekeo huku tukipita bila kuchukua hatua. Sasa wamekua wamefikia pale tulipokuwa tunajua watafika. Tusikimbilie kuwakatia hukumu za haraka, bali tuwawajibishe kulingana na sheria.

Vyombo vya usalama viwajibike ipasavyo bila kuvunja haki ya kuishi ya mtu yeyote. Binafsi sizipendi hukumu za barabarani (mob justice) ziruhusiwe miongoni mwetu. Hukumu za aina hii zitatusababishia madhara zaidi ya faida. Ninaamini hukumu hizi zinaweza kusababisha taifa kuangukia kwenye civil conflicts na kuibuka kukua kwa makundi ya kihalifu. Kila mtu/kundi wakiamini ndiyo njia pekee ya kuhakikisha haki inakuwepo au kulinda maslahi yao na uwepo wao.

Tusiposimama kwa haki tutaangamia.
 
Vyombo vya usalama viwajibike ipasavyo bila kuvunja haki kuishi ya mtu yeyote. Binafsi jisingependa hukumu za barabarani (mob justice) ziruhusiwe miongoni mwetu. Ninaamini hukumu hizi zinaweza kusababisha taifa kuangukia pua. Kila mtu akishika akiamini ndiyo njia pekee ya kuhakikisha haki inakuwepo.

Tusiposimama kwa haki tutaangamia.
Wao kupiga watu mapanga ya kichwa ni sheria??
 
Hujakutana nao wewe na hivyo viinereza vyako. Ipo siku utakutana nao (nakuombea) Utakuja kufuta hiki ulichoandika. Amini haya
 
Shida ni pale mnapotaka kuitumia demokrasia ya Mzungu aliyestaraabika kwa mwafrica mweusi ambaye bado ni primitive....

Africa bado ni primitive, huwezi kideal na primitive people kwa diplomasia na demokrasia ya civilized part of the world... huku watu wanahitaji maelekezo ya vitendo, viboko, risasi na utemi mwiingi ili wakae kwenye njia..

Huko mbele tukishakuwa civilized mambo yatakaa sawa..
 
Hiyo sheria ya kuwapiga risasi vibaka haipo Tanzania. Pia kuua kwa risasi bila kufuata sheria ni mob justice. Binafsi ninaamini watanzania kuna mahali tumekosea kwa ujumla wetu, kuanzia kwa viongozi wa juu wa kisiasa mpaka kwenye ngazi ya familia.

Hao panya road ni watoto waliozaliwa na wazazi watanzania au tuamini kuwa ni wavamizi kutoka nje ya nchi? Hawa ni watanzania wenzetu wanaolindwa na sheria hizi hizi tulizotunga kwa ajili yetu. Tusiwahukumu kabla ya kuangalia tulipokosea.

Baada ya kukosea katika malezi na kupuuza uwepo wao kati yetu, tukiwashuhudia wakikua wakirandaranda mitaani bila uelekeo huku tukipita bila kuchukua hatua. Sasa wamekua wamefikia pale tulipokuwa tunajua watafika. Tusikimbilie kuwakatia hukumu za haraka, bali tuwawajibishe kulingana na sheria.

Vyombo vya usalama viwajibike ipasavyo bila kuvunja haki ya kuishi ya mtu yeyote. Binafsi sizipendi hukumu za barabarani (mob justice) ziruhusiwe miongoni mwetu. Hukumu za aina hii zitatusababishia madhara zaidi ya faida. Ninaamini hukumu hizi zinaweza kusababisha taifa kuangukia kwenye civil conflicts na kuibuka kukua kwa makundi ya kihalifu. Kila mtu/kundi wakiamini ndiyo njia pekee ya kuhakikisha haki inakuwepo au kulinda maslahi yao na uwepo wao.

Tusiposimama kwa haki tutaangamia.
Usipofunzwa na wazazi wako dunia itakufunza!

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kama polisi wameshindwa kazi yao hizo bunduki watupatie raia tuwashone hao panya. Haiwezekani panya wachache watusumbue wananchi
 
Back
Top Bottom