Panya Road 116 wanaotumia silaha za jadi wakamatwa Dar es Salaam katika msako wa siku 3

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,796
11,958
a8d5d8d4-8fe4-44e9-9496-234d5943a77c.jpg

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na jitihada za kuzuia uhalifu na kufanya misako mikali ya kuwafuatilia wahalifu mbalimbali wa makosa ya jinai. Tarehe 12 Septemba 2022 majira ya saa 22:40 huko maeneo ya Mwasonga limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya rifle iliyokatwa mtutu ikiwa na risasi mbili.

Taarifa ya awali, ni kwamba tarehe 12 Septemba 2022 majira ya saa 21:30 usiku huko kijiji cha Marogoro, Mkuranga, Mkoa wa Pwani Majambazi wapatao watano wakiwa na silaha aina ya rifle walimjeruhi Denis Ivo Komba (23) mfanyabiashara wa hardware na miamala ya kifedha na kumpora pesa kiasi cha Shilingi 2,000,000 na simu ndogo ya mkononi na kutokomea kusikojulikana.

Polisi kwa kutumia wataalamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi waliwafuatilia majambazi hao na kugundua kuwa walikuwa wakielekea eneo la Mwasonga Kigamboni, Dar es salaam.

Askari Polisi waliweka mtego katika eneo hilo na majambazi hao walipokaribia katika eneo aligundua kufuatiliwa hivyo kutupa begi lililokuwa na silaha na kutokomea porini na katika upekuzi katika begi hilo ilipatikana silaha hiyo ikiwa na risasi mbili.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawasaka majambazi hawa popote watakapo kimbilia kwani jitihanda za kupambana na uhalifu hazina mipaka.

PANYA ROAD KUKAMATWA
Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche dhidi ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam katika hatua hiyo Jeshi la katika kipindi cha siku tatu kuanzia tarehe 10-12

Septemba 2022 limewakamata wahalifu 116 wa makosa ya uvunjaji nyumba na uporaji wa makundi kwa kutumia na silaha za jadi.

Wahalifu hao wamekamatwa wakiwa na vielelezo mbalimbali; mapanga, visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia, na Televisheni mbalimbali, Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano ya kina na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuhuma zao.

Oparesheni hii kali inaendelea, usiku na mchana, dhidi ya mtu au kikundi cha kihalifu, uvunjaji nyumba na uhalifu mwingine.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi katika kutoa taarifa za kuwabaini wahalifu na Jeshi la Polisi linaahidi kutunza siri.

Pia linawataka viongozi wa serikali za mitaa kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika mitaa yao pia linawataka wananchi kuimarisha mifumo ya ulinzi ikiwa ni pamoja na kufuata falsafa ya ulinzi shirikishi katika kuzuia vitendo vya kihalifu.

Wiliam Mkonda – ACP
KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
 
View attachment 2355671
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na jitihada za kuzuia uhalifu na kufanya misako mikali ya kuwafuatilia wahalifu mbalimbali wa makosa ya jinai. Tarehe

12 Septemba 2022 majira ya saa 22:40 huko maeneo ya Mwasonga limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya rifle iliyokatwa mtutu ikiwa na risasi mbili.

Taarifa ya awali, ni kwamba tarehe 12 Septemba 2022 majira ya saa 21:30 usiku huko kijiji cha Marogoro, Mkuranga, Mkoa wa Pwani Majambazi wapatao watano wakiwa na silaha aina ya rifle walimjeruhi Denis Ivo Komba (23) mfanyabiashara wa hardware na miamala ya kifedha na kumpora pesa kiasi cha

Shilingi 2,000,000 na simu ndogo ya mkononi na kutokomea kusikojulikana.

Polisi kwa kutumia wataalamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi waliwafuatilia majambazi hao na kugundua kuwa walikuwa wakielekea eneo la Mwasonga Kigamboni, Dar es salaam.

Askari Polisi waliweka mtego katika eneo hilo na majambazi hao walipokaribia katika eneo aligundua kufuatiliwa hivyo kutupa begi lililokuwa na silaha na kutokomea porini na katika upekuzi katika begi hilo ilipatikana silaha hiyo ikiwa na risasi mbili.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawasaka majambazi hawa popote watakapo kimbilia kwani jitihanda za kupambana na uhalifu hazina mipaka.

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche dhidi ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam katika hatua hiyo Jeshi la katika kipindi cha siku tatu kuanzia tarehe 10-12

Septemba 2022 limewakamata wahalifu 116 wa makosa ya uvunjaji nyumba na uporaji wa makundi kwa kutumia na silaha za jadi.

Wahalifu hao wamekamatwa wakiwa na vielelezo mbalimbali; mapanga, visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia, na Televisheni mbalimbali, Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano ya kina na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuhuma zao.

Oparesheni hii kali inaendelea, usiku na mchana, dhidi ya mtu au kikundi cha kihalifu, uvunjaji nyumba na uhalifu mwingine.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi katika kutoa taarifa za kuwabaini wahalifu na Jeshi la Polisi linaahidi kutunza siri.

Pia linawataka viongozi wa serikali za mitaa kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika mitaa yao pia linawataka wananchi kuimarisha mifumo ya ulinzi ikiwa ni pamoja na kufuata falsafa ya ulinzi shirikishi katika kuzuia vitendo vya kihalifu.

Wiliam Mkonda – ACP
KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
Haya ndio mambo polisi wanapaswa kupambana nayo.

Sio kupambana na chadema na wapinzani ili kulinda serikali ya walamba asali..huku wao wakiishi kwa kutegemea hela za kiwi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Rudisheni machinga barabarani hali tete mtaani angalau iliwasaidia kupunguza makali ya maisha
 
Back
Top Bottom