Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Kuna taaluma jeshini zinazohitaji elimu, lakini si zote. Hata mtu asiyemaliza la7 anaweza kuwa mwanajeshi na akafanya kwa ufanisi mkubwa.
Na ujajiri jeshini ulikuwa wa holela tangy enzi za Nyerere hadi tu juzijuzi.
Kwa nini wanaweka kigezo cha elimu kwenye interview? achane hizo, kila idara ihakikiwe.
 
Kuna taaluma jeshini zinazohitaji elimu, lakini si zote. Hata mtu asiyemaliza la7 anaweza kuwa mwanajeshi na akafanya kwa ufanisi mkubwa.
Na ujajiri jeshini ulikuwa wa holela tangy enzi za Nyerere hadi tu juzijuzi.
Sawa na walee walio foji vyeti na wanataaluma nyingine nao waachwe tu uko jeshini ???!!!
 
Hii ya kwanza ni wale waliothibitika kufoji vyeti vyao. Lakini kumbuka kuna wengine wana matatizo mbalimbali mf. watu wawili kutumia cheti kimoja, kupotewa na cheti. Hao wametakiwa kumaliza matatizo yao 15 may kabla hawajafutwa kwene payrol.
Yani bado siamini kwamba TPA hamna aliyekutwa na cheti feki. Hiyo list iliyobaki ina watu wangapi?
 
Ndo mfumo tuliona kwa sasa wa kibabe. Ni kweli wamefanya makosa lakini watu 9000 na mifumo yetu mtu mmoja anabeba watu zaidi ya watano. Sasa 9000×5 wakosa mahitaji. Busara ingetumika itafutwe njia nyingine.
Unashanga haya ya kawaida tu,na Mahakama nchini Misri iliyotoa jukumu ya kifo kwa watu 500 kwa Mara moja
 
Ni uonevu sana, hatusemi hivyo kwa kuwatetea waovu, bali kuonea waovu wengine na kuacha wengine ni zaidi ya uovu!!

Kama suala la Bashite haki ya Mungu linaniuma hatari...

Kabisa yaani raisi anampa kichwa bashite mtu ukweli upo na bado anamlinda ila mkuu ajue binadamu unamponyanyasa sana unampa akili ya ziada ya kujikwamua
 
Lakini Mkuu nao wanaajiriwa kutokana na sifa ya Elimu, na wao ni watushi vile vile ktk sekta ya Umma, sasa iweje wasiguswe?

Hawaguswi kutokana na sababu niliyoitaja, humpati mrusha ndege ya kijeshi n.k kupitia matangazo Magazetini
 
Naomba utumishi watuwekee majina ya watu wenye Vyeti feki ili tuanze kusepa mapema. Siwezi nikaacha kaz kabla sijaona jina langu.

Ni bahati mbaya sana! Ni bahati mbaya sana! Kujitekenya na kucheka mwenyewe. Kwa orodha iliyopatikana - kuna utata mtupu. Mosi, kwa kuwa wameweka majina haya kwa Xl, spelling tofauti inafanya orodha ionekane ni kubwa- majina kama Stela kuonekana Stella next row, licha ya majina mengine mawili yaliyobaki kuwa sahihi. Majina Magreth kuonekana Margareth. nk Makosa ya kiuandishi

Lakini pia wapo nilioenda nao shule hadi wamemaliza bila kubadili majina na walishinda. Naona majina yao. Kumbe walichelewa kutafuta vyeti vyao- yaani NECTA hawana taarifa zao, kwa maana wangekuwa wameweza kupata cheti chao huko majumbani kwao, wakakipeleka NECTA basi pengine majina yao yasingekuwepo. Hawa ni walimu walikuwa huko vijijini vyeti vimepotea, sasa hatuna jinsi ya kuverfiy. Kwani faili lake hakuna vyeti?

Zoezi hili litawanyanyasa wale ambao hawaweki kumbukumbu zao vizuri. Wezi wa vyeti ni waangalifu sana hawatakuwa wamepoteza! Je hatuna njia mbadala ya kuwahakiki? Je kazini kwao hawapimwi kuona kama wanafanya kazi kwa weledi unaotegemewa na mwenye cheti. La hasha sitetei ufeki feki lakini tuwe wangalifu tusije tukawatumia watu feki kuhakiki feki!
 
Mi nashauri kama umeondolewa kwa cheti cha kufoji gombea udiwani, ubunge, au omba ukuu wa wilaya, mkoa nk huko hakuna zengwe, mlango mmoja ukifungwa mwingine unafunguliwa.
 
Hawaguswi kutokana na sababu niliyoitaja, humpati mrusha ndege ya kijeshi n.k kupitia matangazo Magazetini
Basi hatujatatua tatizo mkuu nafahamu mrusha ndege wa kijeshi anapewa training akiwa kazini (jeshini) au akiwa ameshasoma (kupata trainingi ya kurusha ndege) uraiani na kule anaenda kuongeza ujuzi wa hizo jet fighter, lakini bado kama kafoji cheti ni kosa au kosa linachaguwa watu kufoji kunachaguwa watu kwamba ww ruksa ww hapana???
 
Naona shida kubwa sana ilikuwa halmashauri, taasisi nyingi zinazojitegemea tatizo si kubwa kama halmashauri. Yawezekana tatizo liko kwenye tume ya ajira wanaoajiri watumishi wa Serikali
 
Back
Top Bottom