Kweli pesa sabuni Leo, tuongeze juhudi kuzitafuta. pesa hainuniwi.Mi mkristo RC yeye mkristo Mlutheri ndoa za pili hatunaga. Halafu angekua na mihela ningemkubali niwe wa pili tu nisikose vyote. Sasa hela hamna nikawe mke wa pili akuuu. Sijajikatia tamaa bado
Nani tena kaliwa?Hii tabia unamtokea mtu unamdanganya uko single wakati una mke au mahusiano yenye furaha na amani ni UBINAFSI. Wewe utasema unanipenda kwa dhati ndio maana umeamua kunidanganya huwazi nitakavyoumia siku nikiujua ukweli?
Halafu utetezi wenu ni "Ooh bby nilijua nikikuambia ukweli utanikataa". Unaona kukukataa na kuniumiza moyo wangu Bora uniumize ili utimizie lengo lako?
Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nawaomba mseme tu ukweli ili mtu ajue anajiingiza kwenye nini Kuliko unidanganye.
Mimi mwenyewe muhanga wa hili jambo na nilikua head over heals kwa huyu mkaka kumbe moyoni mwenzangu anajua kabisa mimi anapita ana mtu wake. Na baada ya kuujua ukweli akaanza kuniambia hana furaha na huyo mwanamke ananipenda mimi. Ila kwa jinsi nilivyompenda nilishindwa kuvumilia nikamwambia tuachane tu siwezi kukushare maan nilimwambia kama huna furaha achana nae uwe na mimi akashindwa. Niliumia mpaka nikaamsha vidonda vya tumbo siku hiyo namshukuru Mungu nimemove.
Rafiki yangu juzi tu kajua mtu aliempenda kwa mara ya kwanza toka apate akili ni mume wa mtu. Na alimdanganya eti hajaoa ana baby mama tu kumbe huyo baby mama ndio mkewe. Na alishamuuliza mwanzo akasema hana mahusiano ana mtoto tu ila yeye na baby mama hawana mahusiano. Mungu alivyo mwema last weekend wamekaa bar kaja mtu anaomba msamaha kwa jamaa kuwa alishindwa kuhudhuria harusi mbele ya rafiki yangu. Rafiki wa jamaa alivyondoka alimuapia rafiki yangu miungu yote kuwa hana mke na ndoa ilishindikana kufungwa halafu kwa sababu ya kijinga sijui kwanini rafiki yangu akamuamini. Sasa nikasikia tena jamaa kaoa nikamwambia rafiki yangu.
Kufupisha tu jamaa ni kweli ameoa na anaesema ni baby mama ndio mkewe nae utetezi wake hakutaka kusema alivyomuona rafiki yangu kwa kuwa aangemkataa ila anampenda.
Mwingine mpaka Pete kavalishwa na mchumba wa mtu na jamaa anaoa week ijayo anamuacha mwenzie na mtoto na aibu ya kupeleka mchumba ambae alikua na mtu mwingine.
Ukijijua huna mpango na mtu mwambie ukweli mtuepushie maumivu makubwa wengine kupenda kwetu kwa bahati tukipenda tunapenda kweli sasa kukaa na kugundua wewe ni side chick kwa bwana wa mtu inauma sana.
Samahanini kwa gazeti ila nimesisitiza na hivyo visa viwili kukazia maombi yangu kwenu. MTUONEE HURUMA na mioyo yetu.
Hahahahaaaaa.. kwanza shemeji ako anafunga ndoa mwezi wa Saba. Na yeye ni mmoja wapo waliocheza na moyo wangu avumilie tu akijisoma humu sikumtuma mimi awe muongo kisa papuchi tu. Wakati angeniambia kawaida ningempa wala hakuhitaji kunidanganya.Kwahiyo dada umeamua kumwekea thread shemeji yangu kipenzi!!
Mbona mimi siringi wala sijisikii na nikadanganywa
Sio ukweli sana. Kwa mfano huyo mwenye mke angesema kaoa ila wana matatizo na mke wake ingekua inaendea ukweli hata siku akimwambia rafiki yangu wamemaliza kesi zao na mke wamerudiana ina make sense.Tatzo Wanawake wanapenda kuongopewa.... Mwanaume ukiwa mkweli Sana utahisi una mkosi
Sio ukweli sana. Kwa mfano huyo mwenye mke angesema kaoa ila wana matatizo na mke wake ingekua inaendea ukweli hata siku akimwambia rafiki yangu wamemaliza kesi zao na mke wamerudiana ina make sense.Tatzo Wanawake wanapenda kuongopewa.... Mwanaume ukiwa mkweli Sana utahisi una mkosi
Hahah umetumia code za Python. Hebu ndada vulie kidogo mpenziUnajua na wewe una tabia za ofisi sana mpenzi?
Bora huyo umtoe taratibu asijue umeoa maana ataumia na kama ni chizi anaweza kuja mpaka kwa mkeo eti akukomeshe kwa kumuumiza.Aisee Mzigua90 kuna mtu nampenda na sitaki kumuumiza hajui kama nna mke na ananiamini sana, najua siku akija kugundua anaweza hata kujidhuru (uoga wangu huko hapa) ananipenda sana, namna pekee nilioona inafaa sasa ivi ni kumpiga matukio mpaka atakapoamua kuanza mahusiano mapya na kuniacha, niko sahihi?for the sake of her life
Kuna mwingine nae baada ya kuoa akaamua kuanza mahusiano mengine aniache ila juzi kati kanicheki anauliza ninaendeleaje na ndoa yangu, nikaongea kwa kutania tuu, “we sijui uliniloga things are not going well” now anataka tuyajenge tena sasa akija kujua baadae mimi na mke wangu tupo okay kosa litakuwa langu
Hakika, ila sasa ndio kama hivyo mama. Ushajiuliza watu kama mimi wapo wangapi jukwaani hapa na huko mtaani?Wewe najua unae gf ukinila ni genye zangu tu wala sitakulaumu
Khaaaah, haufundishiki wewe.
Nimekuambia siyo "asiyejuwa" ni "asiyejua"
Wewe ni mtanzania kweli mkuu?