Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,405
Reaction score
88,864
Hii tabia unamtokea mtu unamdanganya uko single wakati una mke au mahusiano yenye furaha na amani ni UBINAFSI. Wewe utasema unanipenda kwa dhati ndio maana umeamua kunidanganya huwazi nitakavyoumia siku nikiujua ukweli?

Halafu utetezi wenu ni "Ooh bby nilijua nikikuambia ukweli utanikataa". Unaona kukukataa na kuniumiza moyo wangu Bora uniumize ili utimizie lengo lako?
Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nawaomba mseme tu ukweli ili mtu ajue anajiingiza kwenye nini Kuliko unidanganye.

Mimi mwenyewe muhanga wa hili jambo na nilikua head over heals kwa huyu mkaka kumbe moyoni mwenzangu anajua kabisa mimi anapita ana mtu wake. Na baada ya kuujua ukweli akaanza kuniambia hana furaha na huyo mwanamke ananipenda mimi. Ila kwa jinsi nilivyompenda nilishindwa kuvumilia nikamwambia tuachane tu siwezi kukushare maan nilimwambia kama huna furaha achana nae uwe na mimi akashindwa. Niliumia mpaka nikaamsha vidonda vya tumbo siku hiyo namshukuru Mungu nimemove.

Rafiki yangu juzi tu kajua mtu aliempenda kwa mara ya kwanza toka apate akili ni mume wa mtu. Na alimdanganya eti hajaoa ana baby mama tu kumbe huyo baby mama ndio mkewe. Na alishamuuliza mwanzo akasema hana mahusiano ana mtoto tu ila yeye na baby mama hawana mahusiano. Mungu alivyo mwema last weekend wamekaa bar kaja mtu anaomba msamaha kwa jamaa kuwa alishindwa kuhudhuria harusi mbele ya rafiki yangu. Rafiki wa jamaa alivyondoka alimuapia rafiki yangu miungu yote kuwa hana mke na ndoa ilishindikana kufungwa halafu kwa sababu ya kijinga sijui kwanini rafiki yangu akamuamini. Sasa nikasikia tena jamaa kaoa nikamwambia rafiki yangu.
Kufupisha tu jamaa ni kweli ameoa na anaesema ni baby mama ndio mkewe nae utetezi wake hakutaka kusema alivyomuona rafiki yangu kwa kuwa aangemkataa ila anampenda.

Mwingine mpaka Pete kavalishwa na mchumba wa mtu na jamaa anaoa week ijayo anamuacha mwenzie na mtoto na aibu ya kupeleka mchumba ambae alikua na mtu mwingine.

Ukijijua huna mpango na mtu mwambie ukweli mtuepushie maumivu makubwa wengine kupenda kwetu kwa bahati tukipenda tunapenda kweli sasa kukaa na kugundua wewe ni side chick kwa bwana wa mtu inauma sana.

Samahanini kwa gazeti ila nimesisitiza na hivyo visa viwili kukazia maombi yangu kwenu. MTUONEE HURUMA na mioyo yetu.
 
Mwanaume gani ambaye alikuja kukwambia ukweli hana hela ukamkubali? mazingira ya kudanganywa unayaweka wenyewe hii yote kwa sababu ujinga umeweka makazi ktk vichwa vyenu ukiabudia umbo au muonekano badala ya akili na maarifa watu watakuja kama ujiwekavyo

ovar
 
Bora unidanganyie hela nitakuelewa maana na mimi nitapenda hela zako. Ila ukija kwa mapenzi bila hela wala nini halafu nikupende kumbe unanidanganya utaniumiza sana.
Ukinidanganya una hela kumbe huna sitaumia sana wala nini ila kuniongopea moyo wangu nitaumia mno mno
 
Hii tabia unamtokea mtu unamdanganya uko single wakati una mke au mahusiano yenye furaha na amani ni UBINAFSI. Wewe utasema unanipenda kwa dhati ndio maana umeamua kunidanganya huwazi nitakavyoumia siku nikiujua ukweli?

Halafu utetezi wenu ni "Ooh bby nilijua nikikuambia ukweli utanikataa". Unaona kukukataa na kuniumiza moyo wangu Bora uniumize ili utimizie lengo lako?
Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nawaomba mseme tu ukweli ili mtu ajue anajiingiza kwenye nini Kuliko unidanganye.

Mimi mwenyewe muhanga wa hili jambo na nilikua head over heals kwa huyu mkaka kumbe moyoni mwenzangu anajua kabisa mimi anapita ana mtu wake. Na baada ya kuujua ukweli akaanza kuniambia hana furaha na huyo mwanamke ananipenda mimi. Ila kwa jinsi nilivyompenda nilishindwa kuvumilia nikamwambia tuachane tu siwezi kukushare maan nilimwambia kama huna furaha achana nae uwe na mimi akashindwa. Niliumia mpaka nikaamsha vidonda vya tumbo siku hiyo namshukuru Mungu nimemove.

Rafiki yangu juzi tu kajua mtu aliempenda kwa mara ya kwanza toka apate akili ni mume wa mtu. Na alimdanganya eti hajaoa ana baby mama tu kumbe huyo baby mama ndio mkewe. Na alishamuuliza mwanzo akasema hana mahusiano ana mtoto tu ila yeye na baby mama hawana mahusiano. Mungu alivyo mwema last weekend wamekaa bar kaja mtu anaomba msamaha kwa jamaa kuwa alishindwa kuhudhuria harusi mbele ya rafiki yangu. Rafiki wa jamaa alivyondoka alimuapia rafiki yangu miungu yote kuwa hana mke na ndoa ilishindikana kufungwa halafu kwa sababu ya kijinga sijui kwanini rafiki yangu akamuamini. Sasa nikasikia tena jamaa kaoa nikamwambia rafiki yangu.
Kufupisha tu jamaa ni kweli ameoa na anaesema ni baby mama ndio mkewe nae utetezi wake hakutaka kusema alivyomuona rafiki yangu kwa kuwa aangemkataa ila anampenda.

Mwingine mpaka Pete kavalishwa na mchumba wa mtu na jamaa anaoa week ijayo anamuacha mwenzie na mtoto na aibu ya kupeleka mchumba ambae alikua na mtu mwingine.

Ukijijua huna mpango na mtu mwambie ukweli mtuepushie maumivu makubwa wengine kupenda kwetu kwa bahati tukipenda tunapenda kweli sasa kukaa na kugundua wewe ni side chick kwa bwana wa mtu inauma sana.

Samahanini kwa gazeti ila nimesisitiza na hivyo visa viwili kukazia maombi yangu kwenu. MTUONEE HURUMA na mioyo yetu.
Asante mkuu, PM yangu umeiona...!!??[emoji39][emoji39]
 
Back
Top Bottom