Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Unaona, mda mwingine unaweza kuepusha mambo kama haya kwa kukaa kimyaView attachment 1087112

So mtusamehe kwa kweli
Mwambie mwanzoni achague..mda mwingine ukute mtu anahitaji married person...like nje aonekane single ila in private her needs are met

Mana married person mko free kwny gari ama chumbani baas kuzurura na mme wa mtu bar inahusuu.?au awe mtu maarufu .?hutaweza

I ever been with a married guy zamani
Alisema ukweli, kwa vile sikua na mtu mda huo and i really needed regular bed times nkakubali...it was a peaceful and good arrangement cz kila mtu alijua yupo kwny nini..kila mtu akimmiss mwenzie we arrange we meet badae kila mtu anaamsha kwao usiku no stress


And we agreed the day i meet sm1 serious ndo mwisho wetu...na kweli ilikua na hamna aloumia ama kuleta beef..i was happy actually cz nlisahau mastress yote

Utu uzima is also telling the truth na mjue mnataka nini...

Bora umwambie
Js be with me nikucomfort ili uchague mume bila presha kabisaa..
Muwe makini tu na contraceptive..kuzaa nje njee
 
Hii tabia unamtokea mtu unamdanganya uko single wakati una mke au mahusiano yenye furaha na amani ni UBINAFSI. Wewe utasema unanipenda kwa dhati ndio maana umeamua kunidanganya huwazi nitakavyoumia siku nikiujua ukweli?

Halafu utetezi wenu ni "Ooh bby nilijua nikikuambia ukweli utanikataa". Unaona kukukataa na kuniumiza moyo wangu Bora uniumize ili utimizie lengo lako?
Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nawaomba mseme tu ukweli ili mtu ajue anajiingiza kwenye nini Kuliko unidanganye.

Mimi mwenyewe muhanga wa hili jambo na nilikua head over heals kwa huyu mkaka kumbe moyoni mwenzangu anajua kabisa mimi anapita ana mtu wake. Na baada ya kuujua ukweli akaanza kuniambia hana furaha na huyo mwanamke ananipenda mimi. Ila kwa jinsi nilivyompenda nilishindwa kuvumilia nikamwambia tuachane tu siwezi kukushare maan nilimwambia kama huna furaha achana nae uwe na mimi akashindwa. Niliumia mpaka nikaamsha vidonda vya tumbo siku hiyo namshukuru Mungu nimemove.

Rafiki yangu juzi tu kajua mtu aliempenda kwa mara ya kwanza toka apate akili ni mume wa mtu. Na alimdanganya eti hajaoa ana baby mama tu kumbe huyo baby mama ndio mkewe. Na alishamuuliza mwanzo akasema hana mahusiano ana mtoto tu ila yeye na baby mama hawana mahusiano. Mungu alivyo mwema last weekend wamekaa bar kaja mtu anaomba msamaha kwa jamaa kuwa alishindwa kuhudhuria harusi mbele ya rafiki yangu. Rafiki wa jamaa alivyondoka alimuapia rafiki yangu miungu yote kuwa hana mke na ndoa ilishindikana kufungwa halafu kwa sababu ya kijinga sijui kwanini rafiki yangu akamuamini. Sasa nikasikia tena jamaa kaoa nikamwambia rafiki yangu.
Kufupisha tu jamaa ni kweli ameoa na anaesema ni baby mama ndio mkewe nae utetezi wake hakutaka kusema alivyomuona rafiki yangu kwa kuwa aangemkataa ila anampenda.

Mwingine mpaka Pete kavalishwa na mchumba wa mtu na jamaa anaoa week ijayo anamuacha mwenzie na mtoto na aibu ya kupeleka mchumba ambae alikua na mtu mwingine.

Ukijijua huna mpango na mtu mwambie ukweli mtuepushie maumivu makubwa wengine kupenda kwetu kwa bahati tukipenda tunapenda kweli sasa kukaa na kugundua wewe ni side chick kwa bwana wa mtu inauma sana.

Samahanini kwa gazeti ila nimesisitiza na hivyo visa viwili kukazia maombi yangu kwenu. MTUONEE HURUMA na mioyo yetu.
Muda huu ndio natambua kumbe wewe ni KE! Siku zote nilijua ni ME
 
Hizo nyapu hampati kwenye mahusiano yenu ya serious mpk kutesa wengine hisia bila kuwafikiria?!
Mama tukiwaambia ukweli hawataki sasa sisi tufanyeje tunadanganya tukipata nyapu tunapita hiv
 
Ukimueleza ukweli hasa kama HAUNA pesa utampata nani?
Hawa wanapenda sana pesa na lzm ujitutumue siku za kwanza kama pesa ipo.
 
Back
Top Bottom