Ole wenu CHADEMA!

Mkandara,

Kwanza nakubaliana na wewe kabisa kwa michango yako anuwai , ni kweli kabisa kabla ya wapinzani kuanza kutafuta mchawi wao ni lazima waondoe matatizo yaliyopo katika vyama vyao . Tatizo moja kubwa linalowasibu wanasiasa wa afrika ni wanatka kusikia yale wanayotaka kusikia " Very close minded " . Hakuna mwanadamu aliyeperfect kwa hiyo ni michango kama hii inatakiwa itumike kama kioo cha kujikosoa.

Mkandara, umetoa hoja nzito sana lakini nina swali moja tuu ! matatizo ya upinzani umeyahainisha vizuri sasa je kwa mtazamo wako ni vitu vingine zaidi ya vile vile ulivyoainisha hapo juu vinaitaji kufanywa na upinzani ili kuweza kuupa nguvu upinzani ?
 
Rufiji,
Kwanza, ningependa unielewe kwamba sina ubaya na Mbowe isipokuwa najaribu kuwaeleza mapungufu yake. Huyu jamaa yetu ana mazuri mengi sana lakini kama ulivyosema viongozi wanapenda kusikia yale wanayopendeza. Free amejaribu sana kuangalia mahitaji ya wananchi na kuyapa uzito huku nyuma kasahau kabisa kwamba yeye mwenyewe anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba mahubiri yake yanakwenda na vitendo vyake. Kwa hiyo ule msemo wa kutazama nje ya box haina maana kutazama ndani sio lazima. Unaanza ndani kabla ya nje!
Tazama mifano ya nyuma toka Mrema, Sief Sharrif na mchungaji. Wote hawa walikuwa rahisi kuzimwa kwa sababu wao wenyewe hawakuweza kutangaza majina ya watu wengine zaidi yao wenyewe.

Mbowe anafahamu vijana wengi sana waliosoma Mlimani, IFM, Mzumbe na vyuo kibao ndani na nje ambao wote wamepitia Bilicanas ama sehemu nyingine za matanuzi. Vijana hawa karibu asilimia 90 sii wanachama wa CCM au chama chochote lakini vichwa vizuri sana. Mtu kama Michuzi anamfahamu Mbowe kwa ukaribu kuliko JK lakini sidhani kama Mbowe kawahi kumkaribisha Michuzi nyumbani kwake kubadilishana mawazo ya kiushikaji. mambo anayoyafanya J J sijawahi kuona kiongozi yeyote akiyafanya haya na ndio maana blog nyingi za wanasiasa wetu ziko tupu, mapambo mezani.

Radio station hazichukui mamillioni ya fedha na zipo zilizokwisha tumika kwa bei nafuu. Kuna magari ya radio station ambayo yanaweza pia kutumika kukitangaza chama. Tunafahamu wananchi wengi wabongo wanapenda muziki kwa hiyo hata kama station nzima itajishughulisha na muziki zaidi lakini kwa ushirikiano wa chama viongozi hawa wanaweza kupewa vijinafasi vya mgeni maarum ktk vipindi hivyo na kudondosha mawili matatu. Kuwaeleza wananchi sera zao ndogo ndogo ktk maeneo hayo..Kupokea na kujibu maswali kama J J alivyoombwa na Mwanakijiji.
Miswaada ambayo inaletwa bungeni na haimsaidii mwananchi isibakie bungeni, wazushe kasheshe la kitaifa na hata kuomba kamati maalum iundwe kufanya uchunguzi.

Ni kweli kuna scandal millioni ambazo Chadema wangeweza kuzipokea toka bcstimes na hapa TEF kwa kutaka zifanyiwe uchunguzi na wasikubali bunge liendelee kama hakuna suluhu. Scandals kama hizi ndizo hushusha hadhi na jina la chama tawala. Nchi za Ulaya, vyama vingi tawala vimekuja angushwa kutokana na scandals za rushwa ama matumizi mabaya ya fedha za Umma. hata Kenya kanu imeanguka baada ya vyama vya upinzani kuhakikisha maswal ya rushwa yamechukua nafasi kubwa ya utawala mzima wa KANU, hadi kufikia uchaguzi kila mtu Kenya alisha choka! lakini kutokana na kuwepo na vyama vingi walifahamu hapa kwamba serikali ya mgao haiwezi kuwasaidia wananchi kwani rais na ma DC, RC wake ndio watawala. Wakaamua kujiunga na kutengeneza nguvu moja. Hili ndilo tatizo kubwa la popular vote! yaani hata kama JK angekuwa na mbunge mmoja bado angekuwa rais kutokana na popular vote ya asilimia 80. Sasa cha ajabu sijui angechagua vipi baraza lake la mawaziri toka huyo waziri mkuu maanake wote wameshindwa kuchaguliwa na wananchi. In any case, kifupi angekuwa bado ndiye mwamuzi wa mwisho kwa kila muswaada bungeni na commander in Chief wa jeshi la Taifa.. All power to him.

Kwa hiyo Chadema, CUF na TLP wana njia ndefu sana na sii rahisi kwani wote wanataka wao kufika Ikulu sii swala la kuhakikisha dhulma kwa wananchi imekwisha. ten years under Mkapa ilikuwa ishara kubwa kwangu kwamba viongozi wote wa upinzani macho yao ni Ikulu, kuipata hiyo popular vote. Mwaka wa kwanza wa Mrema alilenga majimbo akafanikiwa sana lakini akaja kushindwa pale alipoweka nguvu zake IKULU kwani CUF walitumia mbinu yake ya majimbo. CUF walipofanikiwa kushika nafasi ya Pili wakahamishia macho yao Pemba na uhakika wa Ikulu, hapo tena Chadema wakaingia taratibu waki-focus Ikulu. CUF na Chadema wakaja gongana vichwa wenyewe ktk kiti cha ikulu ambacho hukaliwa na mtu mmoja tu.

Kuanguka kwao JK kachukua kiulaini na sikubaliani kabisa na hoja kwamba JK katumia mitulinga kupita yeye. Nooo way, nakubali kupita kwa baadhi wabunge wa CCM lakini kiti cha Ikulu jamani Lipumba na Free walichemsha wenyewe na kukiacha kiti kitupu.

Hata leo hii ikipigwa kura za maoni kwa popular vote ya mtu sio chama, JK atachukua nafasi ya kwanza mbele ya Free na Lipumba (Combined votes). Watanzania walimchagua JK sio CCM na ndio maana viongozi wa CCM wenyewe walikubali kwamba JK ndiye kawapa ushindi.
 
Nimeendelea kuifutilia hii mada. Wachangiaji wengi wamejikita katika kuamini kile kilichoandikwa katika gazeti la Tanzania Daima. Mimi ni mojawapo. Wapo pia ambao hawaamini kilichoandikwa katika hili gazeti. Ni vizuri na inapendeza kuwa na mtazamo tafauti katika mambo. Tatizo nililo nalo na hili kundi la pili ni sababu zao za kutoamini kilichoandikwa katika gazeti la Tanzania Daima. Moja ya sababu walizotoa ni kwamba Mbowe na CHADEMA kwa CCM si chochote. Hii hoja imekwisha kujibiwa sana na wazi kuwa CCM kama chama au baadhi ya viongozi wa juu wana hofu kubwa na CHADEMA na Mbowe. Siitaji kufafanua zaidi hili maana wachangiaji wa kundi la kwanza wameliweka vizuri sana.

Hata hivyo nataka nichangia zaidi katika maoni ambayo Mkandara na Mzee ES wamerudia mara nyingi. Haya ni maoni yao kuhusu Mbowe. Wameandika mengi ya kumbeza Mbowe na inaonekana wanamjua kwa kiasi fulani. Hata hivyo inaonekana Mkandara na Mzee ES waujua upande mmoja tu waMbowe ambao ni mfanyabiashara. Tena biashara wanayoijua sana ya Mbowe ni ile ya Blicanas. Ni wazi kabisa hawa wanamjua Mbowe yule wa enzi za ujana wao, kabla hajawa mwanasiasa. Katika hoja zao kwa nyakati tofauti, Mkandara na Mzee ES wanasema Mbowe sio mwanasiasa, anapenda umaarufu na kwamba hataki mtu mwingine katika chama apae.

Kwanza ni muhimu kutambua kuwa kila taasisi lazima iwe na kinara wake. Ukikuta kila mtu katika taasisi ni kinara basi ujue hiyo taasisi ama yenyewe ni dhaifu au uongozi wa taasisi hiyo ni dhaifu. Kiongozi asiye ng’ara katika taasisi ni kiongozi butu, hana maono, ni goigoi na hafanya kazi zake za kiongozi sawasawa. Kwa ufupi kiongozi asiye ng’ara haoneshi njia. Vivyo katika chama cha siasa, kuna kinara wake. Hapa nilipo kinara wa Tory ni David Cameron. Kinara wa Labour ni Tony Blair. Kinara wa Liberal Democrats ni mzee Mckenzie. Kukicha, kukichwa utawasikia sana hawa kuliko mtu mwingine yeyote katika vyama vyao. Mafanikio na mapungufu ya vyama vyao yanahusishwa moja kwa moja na mafanikio au mapungufu yao binafsi. Hata wakipata watoto ni habari kubwa.

CCM walikuwa na kinara huko nyuma, Mwalimu Nyerere. Ulikuwa ukitaja CCM unamtaja Nyerere. Ukitaja Nyerere unaitaja CCM. Hii haina maana kwamba viongozi wengine hawakuwepo. Walikuwepo wakiwemo wale aliowataja Mzee ES. Tatizo baada ya Nyerere kuondoka CCM ilikosa dira, ikakosa mwelekeo. Yote hii ni kwa sababu ilikosa kinara. Kwa kifupi ccm haina uongozi. Ina kundi la watu lenye kuundwa na magenge tofauti tofauti kwa maslahi binafsi tofauti. Wamejipa majina mbalimbali likiwemo hilo la mtandao. Kwa utaratibu huu hawawezi kuwa na kinara wa chama. Wana vinara wa magenge mbalimbali kama hao kina JM, JK

Kama nilivyosema awali, Mkandara na Mzee ES, kama walivyosema katika maoni yao, wanamjua Mbowe kama mfanyabishara na hawamjui hata kidogo katika uanasiasa wake. Ubaya wao ni pale wanapotaka kulazimisha kila mtu aamini kuwa Mbowe ni mfanyabiashara tu na sio mwanasiasa. Mantiki ya kawaida inatufundisha kuwa kutokulijua jambo haina maana kwamba hilo jambo halipo. Mzee ES na Mkandara kutokuujua uanasiasa wa Mbowe haina maana kwamba Mbowe sio mwanasiasa! Mimi nimemjua Mbowe katika uanasiasa wake. Sikumjua sana kama mfanyabiashara hasa wa hiyo Bilcanas. Hii ni kwa sababu katika ujana wangu mambo ya disco yalinipiga chenga maana nimekulia kijijini. Nimemjua Mbowe kama mwanachama mahiri wa CHADEMA, kama mbunge makini wa upinzani na baadaye kama Mwenyekiti madhubuti na mpevu wa CHADEMA. Sio siri kuwa nilisita kuingia CHADEMA kwa zaidi ya miaka kumi hadi Mbowe alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti ambapo maono ya CHADEMA kama chama cha siasa yalianza kuonekana. Na kilichonivutia sana kuingia CHADEMA ni falsafa ya Mbowe ya kuvuta vijana wenye kutaka kutumika katika siasa waingie CHADEMA. Baada ya Mbowe kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA sio siri kwamba CHADEMA inaongoza kwa kuwa na vijana wengi waliosoma ndani ya chama wakitumika katika nyanja mbalimbali. Vyama vingi vya upinzani viliwakwepa vijana wasomi kama kina JJ na Zito kwa muda mrefu wakiishia katika NGOs ambapo vipaji vyao havikuonekana. Leo hii mtu akiniambia Mbowe anapenda umaarufu peke yake simshangai tu ila namhurumia pia kwa umbumbu wa kutomjua Mbowe. Mbaya ni pale ambapo wanajifanya wanamjua wakati hawamjui. Hamna ujinga mkubwa kama kufikiri unajua jambo wakati jambo lenyewe hulijui!

Kuna hoja pia Mkandara aliigusia kwamba Mbowe hawezi kumchagua mtu kama Mwanakijiji kuwa mwakilishi wa CHADEMA huko aliko, nafikiri ni Amerika. Nafikiri hapa alimtumia mwanakijiji kama kiwakilishi cha watu makini. Hii nayo sio kweli. Moja ya mikakati ya CHADEMA ni kuweka mwakilishi wake katika kila kanda. Katika kutekeleza hili tulianza na kikao cha kwanza kilichofanyika Mei London chini ya uenyekiti wa Mbowe. Walijitokeza wanachama wengi wa CHADEMA na wengine wengi wasio wanachama. Walikuja pia wanaCCM na mojawapo akaamua kujiunga na CHADEMA baada ya kumsikiliza Mbowe. Pale iliundwa kamati ya kuratibu uandikishaji wa wanachama, wafuasi na washabiki wa CHADEMA waliopo EUROPA. Bahati nzuri mimi niliachiwa hilo jukumu la kuratibu hizo shughuli za uandikishaji. Hapa nilipo nina majina ya watu 66 kutoka UK, Uholanzi, Spain na Ubelgiji. Bado tunaendelea na jitihada ku-mobilise wanachama, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA kwa upande wa EUROPA. Tukikamilisha usajili tutaitisha mkutano mwezi wa kumi kwa ajili ya kuchagua mwakilishi wa CHADEMA. Kuna juhudi pia za kuweka wawakilishi katika kanda zingine za dunia hii ikiwemo America. Kama kuna wanachama na wapenzu wa CHADEMA wajitokeza; wawasiliane na mimi katika private message na tutapeana utaratibu. Tunaanda pia tovuti itakayorahisi haya mawasiliano. Kwa vyovyote vile wawakilishi hawa hawatarajiwi kwamba watateuliwa na Mbowe. Ikumbukwe kuwa moja ya sera na falsafa za CHADEMA ni kupunguza vyeo vya uteuzi na kuwapa wananchu mamlaka ya kuchagua viongozi wao. Sasa hii dhana ya kwamba Mbowe haandai viongozi au hataki mtu mwingine apenye katika chama inatoka wapi?

Wapinzani wanapokea kwa unyenyekevu changamoto zinazotolewa katika forum hii na kwingineko. Hata hivyo propaganda za kukatisha tama hazitakubalika.
 
Ofa yangu ya kumhoji JJ bado ipo. KLH News sasa tumepata vifaa vinavyotuwezesha kurekodi mahojiano mahali popote na kuyarusha kwenye mtandao.. Nimeanza kufanyia majaribio na mambo siyo mabaya. Ningerufahi sana kama ningeweza kufanya mahojiano na Mnyika kabla hajaondoka huku.... tatizo sina contact zake.. if anybody can help I'll appreciate...
 
Mzee Mwanakijiji said:
Ofa yangu ya kumhoji JJ bado ipo. KLH News sasa tumepata vifaa vinavyotuwezesha kurekodi mahojiano mahali popote na kuyarusha kwenye mtandao.. Nimeanza kufanyia majaribio na mambo siyo mabaya. Ningerufahi sana kama ningeweza kufanya mahojiano na Mnyika kabla hajaondoka huku.... tatizo sina contact zake.. if anybody can help I'll appreciate...

Tumia email yake atawasiliana na wewe kuna ile ya yahoo aliitoa na mnyika@chadema.net
 
Mwanasiasa,
Safi sana. Jingine ambalo sikubaliani na Mkandara ni kuhusu matumizi ya helikopta. Tukifuata matokeo yaliyopikwa ya uchaguzi ambapo JK aliibuka na 80% ya kura unaweza kweli kusema helikopta haikusaidia. Lakini ukizungumza na watu hasa vijijini kule kwetu Mara helikopta ilikuwa na kishindo chake. Na kama unaamini kweli kwamba JK alipata 80% basi huijui Tanzania. Alichokifanya Mahita kuhusu CUF ndiyo waliyofanya vijana wa usalama kuhusu hesabu za kura. Heri niachie hapo. Good to see you again, mwanasiasa.
 
Mwanasiasa,

nayapokea malelezo yako kama wewe ni Chadema kwa hiyo tayari umeisha nipa upande uliosimama.

Mimi binafsi sijasema Mbowe sii mwanasiasa, na kweli simfahamu kama mwana siasa. Na tatizo kubwa hapa ni kwamba uanasiasa sio elimu bali ni kipaji cha mtu na mimi natambua hilo. Lakini kipaji cha kuwa mwanasiasa hakina maana ya UONGOZI pia. Kawawa na mzee Kingunge ni wanasiasa wazuri sana lakini hakuwahi kutawala ama kuongoza nchi, hali Mkapa ambaye sii mwanasiasa lakini kaitwa mwanasiasa na kashinda/kashindwa

kuongoza pia. Rais wa Marekani Bush Jr. alichambuliwa sana kwa kutokuwa mwanasiasa lakini kwa kupitia mafunzo kajaribu kwenda na wakati huku amezungukwa na wataalam wa siasa. na hata siku moja Bush na marais wote wa Marekani, Ulaya na nchi zilizoendelea ukiondoa Ulaya ya mashariki, marais wao wote hawakuwahi kuongoza chama.

Ni nchi maskini na zile zilizopitia mfumo wa Kikommunist ndizo zina kichwa kimoja. Kikiondoka basi watasimama kama Al-qaeda ya Iraq hadi hapo atakapochaguliwa mwingine.

Unajua tabia ya mtu hubadilika lakini sio hulka. Mimi nachojaribu kuwaeleza ni vitu ambavyo havinisaidi mimi kitu zaidi yenu nyie wana Chadema. Ukisoma kwa makini, mambo yote niliyoyasema yanaepukika. Ni tahadhari kwenu kutoendesha chama chenu kama wakommunist wengine, na pia jaribuni kuifunga nia yake ya Ikulu kuwa ya kichama. CCM hawakupoteza mwelekeo isipokuwa wamejichanganya wenyewe. Hadi leo hii rais wa nchi ndiye mwenyekiti, na uchambuzi wa mgombea bado unafanywa na wazee CC yao. Kikwete alikuwa na ari ya kiti cha Ikulu kama Mbowe, na uumeyaona mwenyewe aliyoyafanya pindi alipoona picha inataka kubadilika, tofauti yao kichama ni kwamba JK alikuwa na watu nyuma yake ambao wangeweza kugombea na bado CCM ikapata ushindi..Kwa hiyo unaweza kuona tofauti zilizopo kati ya vyama hivi na sikulazimishini mkubali maneno yangu ama mfanye mabadiliko, laa Mbowe anaweza kuendelea kugombea nafasi yake lakini kumbuka kichwa cha mada hii kinasema nini?

Yote niliyoyasema ni kujaribu kuwapa mwanga lakini kama bado mmelala na hoja zangu zinawapunguzia usingizi basi nakuombeni radhi. Mbowe mshikaji wangu na naona aibu kubwa kuingilia swala zima isipokuwa mwanya kautoa mwenyewe kwa kugombea urais wa jamhuri. Hapa ananigusa moja kwa moja na kama amebadilika kwa nini yote nayoyawekea wasiwasi ndiyo hali halisi ndani ya Chadema.?

Mwanasiasa, ikiwa wewe umechaguliwa na Mbowe kuwa mwakilishi wa Ulaya basi kosa kubwa sana kwa sababu hujulikani!...na kwa sababu hiyo ndio maana una wanachama 66 tu. Hapo London kuna jamaa kibao wengine wamepewa majina ya Umeya, wote hawa anawafahamu kwa ukaribu kwamba wanaweza kuvuta watu lakini sielewi sababu.

Na wewe lazima uwe mtu wa watu na kujichanganya muhimu, tembelea club za Kibongo ipo moja pale east London. Mimi nakumbuka siku za nyuma nimemjua JK kwa kumuona New Africa. Alikuwa akija anabana kona na kikopo chake cha Ginger ale halafu anatoa offer kishenzi hali yeye mwenyewe hanywi pombe. Akitoka hapo kaingia uswahilini, mara utamsikia Kinondoni. Wengi walisema alikuwa akitafuta mabinti lakini mbona offer zake nyingi zilikuwa kwa makundi ya wanaume?.... because he was smart! aliweka goals zake za kuuza jina lake kwani chama tayari kilikwisha jitangaz vya kutosha.

Utanisamehe sina maana na wewe hufai kuwa kiongozi lakini nachosema ni kwamba makosa kama haya ndiyo hu-cost chama kizima na lazima ubadilishe tabia na kuwa mtu wa watu vijiweni kwa manufaa ya chama na sio mapenzi yako.
 
Mwanasiasa,

Kumjua kwako Free kisiasa na kutomjua kwangu as of your claim, haibadili ukweli kwamba alishindwa vibaya sana katika uchaguzi uliopita na kwamba yeye personal au chama chake, sio tishio kwa CCM, na hasa Mtandao!

Upinzani pamoja na Free na nyinyi wote wa Chadema mna safari ndefu sana mbele yenu, kwa sababu Watanzania ni lini watawachukulia nyinyi kuwa serious! Kitu kidogo tu kama kuungana kinawashinda I mean so far kitu kimoja tu kidogo cha kuwa-convince wananchi hakuna? Unajua you are right sihitaji kuujua upande wa siasa wa Freeman baada ya kuona Helikopta, guess what? Wananchi wamekataa kuwa Helikopta sio hoja, ni afadhali CCM ambao sio perfect lakini hawana helikopta!, ndio maana ya kura za 80%, leo 2006! Aibu!

Ni kweli mimi kama wananchi wengine hatujui the political side ya Freeman ndio maana tumekataa kumpigia kura, hatujui kwa sababu ameshindwa ku-communicate as politician tukamuelewa, yaani point yako inamfanya hata JK aliyekuwa haaahidi tu kuwa na nafuu kuliko asiyeweza kueleweka kabisaaa, maana angalau wananchi walimuelewa JK ingawa utekelezaji ndio hivyo!

CCM as chama kina mikakati na mipango yake, so tuntegemea na upinzani nao wawe nayo sio kulia lia tu where does it stop? Toka vimeanzishwa ni kulia aaaaaaa tu yaani unajua kuna wananchi wameanza kuamini kuwa huenda kulia lia ni moja ya fundamentals za kuitwa chama cha upinzani. Lets say hili gazeti linasema ukweli kama unavyoamini, now kwa nini upinzani nao wasikae kikao na kuanzisha mbinu za kuiua CCM?

Lets say, ni kweli Mzee Jakaya Kikwete rais wa Jamhuri, ameitisha kikao cha NEC, CCM na kuwaomba wajumbe 2,000 msaada wa namna ya kummaliza Freeman na Chadema, aliowashinda kwa kura 80% katika uchaguzi ulioisha karibuni, sasa anawaomba wamsaidie kummaliza ksisiasa maana ni tishio sana katika utawala wake, hebu tuseme kama unavyosema kuwa ni kweli, je kuna sheria ya nchi Tanzania iliyovunjwa?

Unajua na nyinyi upinzani wakati mwingine ni nyinyi wenyewe mnajivunjia heshima mbele ya wananchi, hivi kweli kuna Mtanzania au mbongo anayeweza kuamini kuwa huu ujinga uliondikwa na hili gazeti kuwa ni ukweli? Si kuna maswali ya kujiuliza tena ya haraka haraka, Je kuwa mmaliza BM, JM, SAS, Mangula, Mwandosya, JK alifanya kikao na kumuomba nani msaada? Mbona hli gazeti halikujua? Imekuwaje mpaka likajua hii ya safari hii ya kummaliza mtu na chama alivyovishinda tayari?

I mean CCM sio malaika, na mimi sio mnazi wa kupenda tuu kama mjinga lakini jamani upinzani hebu njooni na issues, real issues, sio huu ujinga, tena ninawatahadharisha kuwa mkifanya mchezo hawa CCM watatawala milele, yes look at your issues? Wabunge wenu wanakuja bungeni na kusema upumbavu usiokuwa hata na miguu, eti viongozi wa CCM wana nyumba SA, get real guys hawa wanaiba hela mbuzi tu za kuweza kujenga Mbezi na kujiuzia nyumba za serikali, za kununua nyumba Madiba au bondeni hawana, labda mmoja tu Yona ambaye ninajua kuwa ana nyumba DC, otherwis eni hadithi za chooni tu!

Nyinyi upinzani kina Mwanasiasa na wenzio kazaneni muimarishe vyama vyenu, hawa wafanya biashara kina Mtei, Ndesamburo, Lwakatare, Slaa, na Freeman wanachotafuta ni masilahi yao tu, toka hivi vyama vianze ninaamini viongozi genuine walikuwa ni Brown Ngwilulupi, Kaborou, na sasa JJ, basi wengine wote ni watafutaji tu kama CCM, kwa hiyo chungeni tena msije kushangaa kuwa wakati mnabishania huu ujingwa wa hlili gazeti wenzzenu walikuwa wanapitisha sheria za mkao wa kula zaidi! Haya magazeti uchawara hayawezi kuwa ndio chanzo cha agenda zenu kisiasa mnahitaji more than this kuwashawishi wananchi, ama sivyo mtakuwa on defensive side daima, kama alivyosema Chadema mwenzio hapo juu jitahidini kuweka mikakati ya kuiweka CCM on the defensive katika issue muhimu, lakini sio hizi issue za kubuniwa kati ya makundi ya CCM na upinzani!

Halafu mumwambie Freeman kuwa aache kukata deal kama ile ya kumuachia Mzee JK, kama angeshindwa CCM au mnafikiri tumesahau, ilikuwaje akakata naye deal si ndio ufanya biashara wenyewe huo? Halafu leo eti huyo JK aliyefanya naye deal kupitia kwa Kingunge, sasa amebadilika anataka kummaliza na mnategemea sisi wabongo ni wajinga sana tuamnini hayo mazingombwe? Acheni filimbi vijana fanyeni kazi za kuimarisha vyama vyenu vibovu na uchwara, kazi kukimbilia Ikulu tu! na kugombea ruzuku, na kuwasaliti wananchi kina Marando!
 
Mkandara: tatizo lako unapenda kuwawekea watu maneno midomoni. Mimi sikusema kuwa Mbowe alinichagua kuwa mwakilishi wa ulaya. Soma hoja ya mtu between line-nimesema nilipewa jukumu la kuratibu uandikishaji wa wanachama na wala sikuteuliwa kama mwakilishi! Usinilishe maneno. Unaposema sijulikani kwa nani? Na nani amekwambia kwamba watu wote waliopo UK lazima wakae east london? Ni ugonjwa mwingine kufikiri kuwa karibu na watu lazima uende club za usiku na utoe offer kama alivyofanya JK. Unajuaje kama value system yangu hainiruhusu kwenda katika club kama hizo? Kuna watu wengi waliofanikiwa kisiasa na sio wote waliotumia hizo club za usiku kama JK. In a civilised society hiyo ni disqualification wala sio sifa!

Tatizo la Mzee ES ni pale anapojibu hoja kwa jazba. Kwenye post yako hapo juu Mzee ES umeongea mambo mengi mno ambayo hayana hata uhusiano na mada. Yaani tukikujibu hoja ndio kusema kwamba tunalia tunalia? Kwani unataka mkisema kitu tuseme tu ndio bwana, hata kama hatukubaliani na maoni yenu. Yaani wewe ndio kusema unawafahamu sana wananchi wa TZ kuliko mtu mwingine yeyote na kwamba wewe ni mwarobaini wa matatizo ya upinzani? Siamini hivyo!
 
Mwanasiasa,

Samahani naona nimekutia mwiba nyayoni na labda hukutaka kuyasoma maelezo yangu mimi kabla la majibu yako.

Nilisema Mbowe hawezi kumchagua Mwanakijiji kuwa mwakilishi wa nje. Jibu lako lilikuwa hiyo sio kweli na ukatoa mfano wako. Nadhani kwa kuelewa kwangu hilo lilikuwa jibu la hoja yangu.

Pili, niliposema hujulikani ilikuwa kwa lengo la jukumu ulilopewa -Kuandikisha watu uanachama. Sijasema qualification za kuongoza Chadema. Kwa hiyo issue hapa ni kuwapata watu wajiunge na chama. Sikusema lazima ukaishi east London isipokuwa nimeitoa kama mfano mmoja wa sehemu za kujichanganya na kuwakamata watu.

Mwanasiasa, hoja yangu inahusu value ya chama na sio yako binafsi na kama kweli value system yako haikuruhusu wewe kwenda club, kisha ukaiweka mbele ya chama basi kweli kazi hiyo haikufai. Bado nitaendelea kusema hii haina maana wewe huwezi kuongoza kamati za Chadema...

Nimemtaja Mwanakijiji kwa sababu zangu za kimsingi kwani jitihada zake kuwavuta watu zinajitokeza wazi,hii haina maana mwanakijiji ni mzuri ktk uongozi. trust me, nafasi ndogo sana kujieleza mengi lakini sina maana nakuponda ama namponda Mbowe, natazama maslahi ya chama na sio yenu binafsi. Wanachama 66 ulaya nzima mshikaji huifanyi kazi inavyotakiwa, samahani sana na hiyo civilized world yenu.

Hiyo civilized society unayozungumzia ni ipi hiyo?...Hivi wewe unataka kuwaandikisha uanachama wazungu wa Uingereza ama Watanzania wanaoishi London na Ulaya?. Je, Chadema inawalenga hao civilized society zaidi hali asilimia 80 ya Watanzania bado tunaitwa uncivilized kwa mtazamo wenu. Nimesema JK alikuwa akija New Africa kujichanganya na watu na sio jana wakati anapigania urais..Hii nazungumzia miaka ya 80's mshikaji wala New africa sio club kama unavyofikiria wewe. Sijui hizi tafsiri unazipata wapi?.

Jaribu sana kuoanisha maneno kabla hujaenda nje na kuleta maana mbaya kwani sina malengo ya kukushusha hadhi wewe ila macho yangu yako upande wa chama.
 
Mkandara na Mzee ES
Acheni vitisho vyenu kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake kwenye hii forum. Msijifanye mnajua sana siasa kuliko wengine. Wacha vijana watoe mawazo yao. Wao wanatanguliza uzalendo zaidi ya uchama. Nyie mmekulia kwenye u-dictetor, wenyewe wanamawazo ya kisasa. Naomba tuwape mwanya. Pia acheni matusi yeenye kejeri.
 
Last edited by a moderator:
Kwasakwasa,
Hivi hapa anayepingwa ni nani. Nani anayetoa mawazo yake na hakubaliki!...vitisho mnavyo nyie hasa mnapowekwa kibano. Tunasema Chadema wanahitaji kujijenga kichama kwa kutumia mbinu mpya, hamtaki mnang'ang'ania kwamba Chadema ni safi hali kimeshika nafasi ya tatu. Dhulma imefanyika hakuna anayekataa lakini mnafanya nini kuhakikisha uchaguzi ujao mtakuwa tayari kukabiri dhulma hiyo.

Mzee Es kawambieni kilio hakisaidii kitu, mbinu za kuiangusha Chadema zichukulieni kama kweli na mzifanyie kazi pia ikiwa hamna mbinu tumejaribu kuwapeni. Hamtaki kwa sababu mbinu hizo zinawakosoa ktk maombolezi hali chama hakijafa.

Zanzibar wamelia sana sasa tunakaribia miaka ishirini, kila siku wakirudia makosa yaleyale. Tukisema Seif Sharrif hawafai wao ndio kwanza wanamchagua tena na kumweka mbele. Twenty years my brother huo umri wa mtu hasa ktk dunia hii ya ukimwi na bado hawajaona mwanga kwa sabu tu ushauri wetu unatoka bara. Think about that!
 
Mkandara;
Hata ungelikuwa wewe kwa hali ya mazingira ya TZ kisiasa, si rahisi kuishinda CCM. Mimi uwanasema bila kubadiri katiba ya nchi, CCM itatawala mpaka milele. Viongozi wakuu kuanzia Rais, RC, DC, wanamadaraka makubwa mno, wanaweza kufanya wanalotaka, pia mjue hao ni makada wa chama. Pia vyombo vyote vya dora vinaongoza na makada wa CCM. Mahita alituhakikishia bila yeye mambo CCM yangekuwa mengine, tumeshuhudia huko Unguja, Pemba, Karagwe, BKB Mjini, Tarime, kigoma etc. Mtaendelea kuwasema Wapinzani na kutoa maoni, lakini bila ya kubadiri katiba, hakuna upinzani wa maana utajitokeza. Ndiyo maana hawa vijana wanalia na System wewe na ES mnajitia kuwashambuli, yeyote anayewapinga mnasema ni CHADEMA. Tunapojadiri vitu hizi jamani,lazima tuweke taifa mbele, hawa vijana wanauchungu jinsi Economic Management ya nchi inavyoendeshwa ki-Pwagu, masirahi ya nchi hayatiliwi mkazo,tumeshuhudia kashfa nyingi kipindi kilicho pita. Watanzania kwa sasa ni kama watoto yatima.

GOD BLESS TZ.
 
Kwasakwasa,

Nadhani unatoka nje ya mada sasa hivi.

Nionyeshe sehemu ambayo tumezungumzia katiba na sisi tumepinga.

Je, katika mbinu za CCM kumbomoa Chadema - katiba inatumika? sioni uuwiano hapa.

Katiba kweli mbovu inahitaji marekebisho hasa swala la nguvu ya rais na hao ma RC na DC lakini nadhani bcstimes na vijiwe vingine wananchi wamelizungumzia kwa mapana kuliko vyama vya upinzani inapofikia utaratibu wa kura. Na mbaya kuliko yote wapiga kura huingia vibandani wenyewe bila mahita nyuma yao, kwa hiyo uchaguzi ni wa raia sio Mahita.

Kinachonishangaza, hawa wanachama hasa wa Zanzibar huanzisha vagi hata kabla ya upigaji kura hivyo kuwapa CCM sababu ya kuingiza polisi. Na Seif Sharrif mwenyewe huanza kusema kuwa safari hii damu itamwagika ikitokea dhulma, maneno kama hayo huchangia kila fujo na kiongozi kama yeye alitakiwa kuelewa zaidi.

Nambie mara ngapi tumesikia swala la majimbo, udini, ukabila, takrima na wagombea binafsi hali tatizo kubwa ni nguvu ya rais hasa CCM kuingilia uchaguzi.. Aghalabu kumsikia kiongozi wa Upinzani akidai marekebisho ya katiba hasa ktk kifungu hicho.

Vyama vya upinzani watachukua fomu za kugombea hali wakifahamu katiba haitoi ushindi kwa mpinzani, na mkatumia mamillioni kujitangaza ndani ya katiba mbovu, hapo tumlaumu nani?...lakini angalia basi baada ya uchaguzi viongozi wengi wa vyama hivi hivi walisimama na kusema wananchi wote ni mbumbumbu bado wamelala wakiwa na maana wananchi hawakuchagua vyama vyao. Na pongezi za ushindi watazitoa hali kuna kesi nyingi za maonezi kwa wabunge. Hii nikiwa na maana wamekubali wao kushindwa ktk kura za popular ktk kiti cha urais hao wabunge watajiju. ndi hao akina JJ leo hii bado wanapigana kupata haki zao na sioni kabisa kiongozi zaidi yake mwenyewe akisimama kusema maoni hayo lazima yatafutiwe dawa.

Kwa nini wasiwe wakweli kama tunavyoangusha madongo humu! kwa nini wanababaisha huku na kule hali katiba inatakiwa kurekebishwa.

Ebu jaribu kuangalia maisha ya hao wagombea wa vyama vya upinzani baada ya kutokuwepo haki. Mwai Kibaki na Moi hawakuwa karibu miaka yote ya kunyanyaswa wananchi. Urafiki mahala ambapo wewe ni representative wa wanyonge waliopoteza maisha yao kwa kupigania haki ni udanganyifu mkubwa. kama uchaguzi ungekjuwa wa haki fare and free ningekubali urafiki wa aina yeyote lakini ikiwa kumetokea maonezi kwa wananchi, kupigwa na hata wengine kupoteza maisha sijui hawa viongozi wanawakilisha maslahi yao ama ya wananchi!
 
Mwanakijiji,

nimekujibu. Tazama kwenye anauni pepe yako unipigie urgently, niko bado NY.

Wengine,

Nitapitia post zote na kujibu mtondogoo, ratiba ngumu!.

Mkandara,

Sitaweza kuja kwako safari hii, inabidi niwahi nyumbani haraka. Kuna tukio ambalo sipaswi kulikosa.

JJ
 
Hii ni great debate kwa sababu kila siku inaleta wazee wapya wa upinzani, great, mzee Kwasakwasa karibu,

(1). Hapa hatishwi mtu, na wala hatishiki mtu, hata siku moja halafu Bob Mkandara ni neutral man sio mwanachama wa CCM hajasema hivyo, isipokuwa mimi ni CCM, damu damu na niko hapa kusema ukweli wa ninachoona katika siasa ya nchi yangu bongo. CCM imeoza, lakini upinzani umeoza zaidi, kama huwezi mhimili kaa pembeni hapa wote ni watu wazima hakuna watoto wala vijana, wote watu wazima registration ya hii forum inasema watoto ni miaka 13 zaidi ya hapo ni midume kwa hiyo acha u-UNICEF hapa weka chini mambo yako yapimwe, tutaendelea kuweka chini ukweli wa mambo, na sio lazima kuwa upinzani ili kuwa na uchungu wa nchi yetu!

(2). Mwanasiasa, nimekusikia ila hakuna jazba ni siasa ya agenda kuwekwa na magazeti uchwara ndio tatizo hapa, lakini anyway nimekusikia mkuuu!
 
Mzee Es,

Kusema upinzani umeoza unakosea, sema UNANUKA!!!, kushindwa kuweka umoja baina yao inathibitisha UBINAFSI walionao. Wengi wao wapo kwa ajili ya matumbo yao tu!!.

Kwasakwasa, Sifahamu kama ndio kwanza unashiriki humu au umesaini kwa jina lingine, nimekuwa nikisisitiza watu kujadili maoni ya mtu na sio kumshambulia mtu binafsi. Shambulia maoni ya Mkandara na Mzee Es, sio wao. Kwa tabia hiyo ndio maana Upinzani wanakosa hoja za msingi za kuwaeleza wananchi. Mnabaki na Huyu ana nyumba wapi, yule ana share kule, Njooni na hoja, jengeni sera, ziuzeni kwa wananchi, wasisitizeni wazinunue na kisha wazile(wawapigie kura).

Back to the topic, Hakuna anayetaka kumfanyia Mbowe chochote acheni propaganda, hivi darasani ukiwa unakuwa wa kwanza kila mara utakuwa na wasiwasi na wa tatu tean tofauti ya maksi ikiwa ni karibu 75%!!, ebu leteni uchambuzi wa maana na acheni hizo, siku zote mtabaki mnalialia tu hamna jipya. Katiba mbaya, lini mmesusa uchaguzi? tena ingekuwa wakati muafaka mkashirikiana na kususa uchaguzi kwa kama miaka kumi hivi huku mnapigania katiba ibadilishwe na huku mkijijenga hadi vijijini!!

Nasema viongozi wa upinzani karibu wote ni wababaishaji!!

Karibu sana Kwasakwasa kwenye hii forum
 
Mzee FD,

Poa, unajua sometimes inachukua muda kwa wengine kuelewa kuwa hii ni forum, na uhai wake unategemea malumbano sasa hata yakielekezwa kwenye ubinafsi hakuna noma kwani siku zote kutakuwepo na majibu, kwa hiyo usiwe na wasi wasi it takes time kabla ya some of us kuelewa msimamo wa malumbano!

ukisoma nyuma utaona kuna baadhi yetu walikuja na vitisho na ngebe lakini sasa wametulia, siku zote lazima kuwa na uvumilivu wa kuwapa nafasi wageni ku-develop na ku-fit in!

As of the rest, sina cha kuongeza ubarikiwe!
 
Fikiraduni;
Mimi Mkandara na Mzee ES siwajui, siwezi ku-wa attack wenyewe, mimi ninapinga hoja zao, ambazo mara kwa mara zinaelekezwa kuwakejeri wapinzani na watu wote wanaosupport kuwepo upinzani chini. Isiwe na wewe huko kwenye hilo kundi. Kama kweli upinzani ni dhaifu, udhaifu wake unatokana ukilitimba wa serikali wa kutowapa upinzani mazingira ya kuwawezesha kupata viti vingi Bungeni. Mashambulizi ya Mkandara na ES yaelekezwe kwwenye serikali yao. Kama nilivyosema upinzani una-operate kwenye mazingira magumu. Najua humu kuna watu walikuwa wanaishambulia hii furum eti ya Iddi Simba, baada ya BCS kufungwa wakajikuta wako hapa, sasa wanajitia kukaribisha watu wengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom