CCM kumbomoa Mbowe
Wadai watatumia mbinu iliyommaliza Sumaye
Na Mwandishi Wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza mkakati wa siri wa kubomoa upinzani, na sasa imedhihirka kwamba mlengwa nambari wani ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na chama chake.
Habari zilizoifikia Tanzania Daima zimeonyesha kwamba mkakati wa kumbomoa Mbowe ulianza kusukwa rasmi tangu Novemba mwaka jana, wakati wa kampeni za kugombea urais, baada ya Mbowe kuonyesha makali yake.
Katika uchaguzi huo, Mbowe alikuwa anagombea urais, na alipata nafasi ya tatu nyuma ya Jakaya Kikwete wa (CCM) na Profesa Ibrahim Lipumba wa Civic United Front (CUF).
Vyanzo vyetu ndani ya CCM, ambavyo havikutaka kutajwa majina, vimesema kwa nyakati tofauti kwamba kilichomponza Mbowe ni kauli aliyoitoa akiwa Mererani, mkoani Manyara, akimtuhumu mgombea wa CCM kupewa sh milioni 40 na wawekezaji wa mgodi wa TanzaniteOne, kwa ajili ya kampeni.
Katika mkutano wa Mbowe uliohudhuriwa kwa wingi na wachimbaji wa madini wa mgodini hapo, Mbowe alisema Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgombea wa CCM, asingeweza kuwafanya lolote Wazungu wa TanzaniteOne - kama walivyokuwa wanataka wachimbaji - kwa kuwa mwekezaji huyo amechanga sh milioni 40 kwa ajili ya kampeni za CCM.
Mbowe aliwaomba wampe kura ili akiwa rais aweze kuangalia upya mikataba ya madini na hatima ya wachimbaji wazalendo.
Vyanzo vimesema kauli hiyo ilimzulia chuki isiyo ya kawaida miongoni mwa viongozi waandamizi ndani ya CCM, huku wengine wakijiapiza kwamba wakishapata madaraka, kazi yao ya kwanza ni kummaliza Mbowe.
"Sisi tulikuwa tunamwona Mbowe kuwa ni mstaarabu, hana siasa za kubomoana; lakini baada ya hapo tuliona ameanza mambo ya Mrema ya kulipua mabomu.sasa sisi tuko madarakani. Lazima atutambue," kilisema chanzo cha habari.
Kingine kilisema kauli hiyo imeharibu hata uhusiano mzuri uliokuwa unaonekana kuwapo kati yake na Rais Kikwete, kwani hivi sasa Rais Kikwete ni miongoni mwa watu 'wanaomchukia' mno Mbowe, na hawezi kumuachia afurukute. Wengine wamefika mahali pa kusema anamwogopa.
"Unajua hata sisi tumeshangaa. Mzee anamwogopa sana Mbowe.sijui imekuwaje, kwa sababu sisi wengine tunamwona Mbowe kama anatupa changamoto.lakini sasa tumefika mahali hata jina lake linatajwatajwa kwenye vikao vikubwa ndani ya chama chetu.wanamhofia," kilisema chanzo kingine.
Chanzo hicho kilitoa mfano kwamba hata katika hotuba yake kwenye vikao vikuu vya CCM mwezi uliopita, lilipokuwa linajadiliwa suala la mgawanyiko ndani ya CCM na hatima ya watu wanaojiita wanamtandao, baadhi ya viongozi waandamizi walifika mahali pa kumtaja Mbowe kwamba ndiye anayepandikiza dhana ya mgawanyiko ndani ya CCM.
Hata hivyo, msimamo huo umepingwa na baadhi ya wajumbe, wakisema CCM ikitaka kusimama imara isimsingizie Mbowe au kutafuta wachawi nje ya chama, bali ikubali kujikosoa.
Vyanzo vya habari vinasema macho ya watendaji wa CCM sasa yanaelekezwa kwa Mbowe kuliko kwa mwanasiasa yeyote wa upinzani, kwa kuwa ndiye anaonekana kuwa na hoja zenye mvuto mbele ya umma akilinganishwa na wapinzani wenzake.
Kinachosubiriwa sasa ni mabadiliko ya uongozi wa juu ndani ya CCM, ili waanze kujipanga namna ya kumbomoa, kwa kuwa kazi ilishapangwa.
"CCM mpya haitakuwa na simile juu ya Mbowe..nakuhakikishia, baada ya miaka minne CHADEMA haitakuwa ile ile, wala Mbowe hatatamba tena," kilisema chanzo kingine.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, CCM inadhamiria kumbomoa Mbowe kisiasa na kibiashara kupitia njia mbalimbali za propaganda na kisheria, na kwa kutumia vyombo vya habari.
Uchunguzi unaonyesha kwamba hata sasa kazi hiyo imeanza, lakini inahitaji kuendelezwa kwa kasi hapo baadaye.
Chanzo kimoja kimedokeza kwamba watambomoa kwa mbinu ile ile waliyotumia kummaliza aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye.
"Ngoja nikwambie. Unadhani kilichommaliza Sumaye ni nini? Propaganda.Alishughulikiwa mpaka ikafika mahali kila mtu ukimuuliza anasema Sumaye hafai, hata kama hana maelezo. Lakini si kwamba hafai.alishughulikiwa. Bila vyombo vya habari, leo angekuwa mtu tofauti. Kazi iliyopo sasa ni kushusha umaarufu wake kisiasa," kilisema chanzo.
Hata hivyo, baadhi ya wana CCM wanasema Mbowe ni mtu muhimu, kwa kuwa anatoa changamoto zinazowasukuma hata wao kufikiri mara mbili, na kwamba nyingine serikali iliyopo imezitumia kurekebisha kasoro zilizokuwapo. Wanasema kwamba kinachoogopwa kwa Mbowe ni uwezo wake wa kujenga hoja.
"Tofauti ya Mbowe na wenzake ni kwanza, anajua kujenga hoja. Ukimsikiliza utakubaliana naye. Pili, ndiye mwanasiasa ambaye umri unamruhusu kuweka mikakati ya muda mrefu. Halafu usisahau, hana njaa kama wengine hawa. Hatuwezi kumhonga au kumnunua Mbowe.njia rahisi ni kummaliza kisiasa," kilisema chanzo kingine.
Baadhi ya wana CCM wamekiri kwamba chuki dhidi ya Mbowe ilipandikizwa hata miongoni mwa wabunge tangu mwanzo, na ndiyo maana Mbunge wa CHADEMA wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alifanyiwa njama akashindwa kwenye uwakilishi wa Bunge la Afrika, Desemba mwaka jana.
"Kwa kuwasikiliza tu, Zitto alionyesha ni mpevu kuliko washindani wenzake. Lakini tulishaamua kumnyima, kwa sababu tuliona kumpa yeye ni kuikuza CHADEMA na Mbowe. Ile tulifanya kisiasa tu.lakini tulijua," kilisema chanzo kingine cha habari.
Habari zinasema kwamba huko nyuma, mbinu zilizotumika kuwamaliza wapinzani ni pamoja na kupenyeza watu wao ndani ya vyama vyao ili walete vurugu, jambo wanaloweza kulifanya kwa CHADEMA pia, ili viongozi na wanachama wagombane, wafukuzane.
Mbinu hiyo ilifanikisha kuimaliza makali NCCR - Mageuzi, kilichokuwa chama kikuu cha upinzani kati ya 1995 na 2000. Baada ya NCCR-Mageuzi kusambaratika kwa tofauti kati ya viongozi wakuu, viliibuka vyama vingine viwili; Tanzania Labour Party (TLP) na CUF, vikiwa vimevuna maelfu ya wanachama waliokuwa NCCR - Mageuzi.
Uongozi mbovu, dharau kutoka kwa jamii na migogoro isiyoisha imeimaliza TLP, huku CUF ikiathiriwa zaidi na propaganda kwamba ni chama cha kigaidi na cha Kiislamu, jambo ambalo limekifanya kihusishwe na baadhi ya matukio yasiyopendeza, kibaki na wanachama wale wale, au wapungue, kisikue zaidi.
Hata idadi ya kura kilizopata mwaka jana, ikilinganishwa na ya mwaka 2000, ukweli unaonyesha kwamba kimedumaa, hakikui.
Chama kinachoonekana kukua, hasa upande wa Bara, ni CHADEMA chini ya Mbowe, huku kikiwa na sera kuu mbili - ya majimbo na elimu - ambazo baada ya ufafanuzi wa Mbowe, zimekitofautisha na vyama vingine.
Mitaani, mwanasiasa anayezungumzwa sana kwa upande wa upinzani, huku akipewa nafasi ya kukua zaidi ni Mbowe.
Vyanzo vya habari vinasema CCM wamefanya utafiti, wamelijua hilo , na hawawezi kumwachia akashamiri, kwa sababu hawataki kusumbuliwa katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Chanzo: http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/06/11/habari1.php