Nzega: Risasi zatumika kumuokoa Mbunge Kigwangalla

huyu kigagula ni kigeugeu.wakati anasoma pale muhimbili,mwaka 2002 uliitishwa mgomo na serikali ya wanafunzi kushinikiza kuondolewa kwa aliyekua mkuu wa chuo wakati huo,prof mtabaji.huyu kigagula akatusaliti,ishu zote zilizohitaji uwakilishi wa rais wa wanafunzi akawa anaenda yeye kwa siri na kusign doccuments zote wakati hakua kiongozi kwenye serikali ya wanafunzi,so sishangai leo akiwageuka wana nzega.
 
Nilishasema ukimsikia Mwana-CCM anaongelea kuhusu maslahi ya Wananchi basi muangalie kwa karibu zaidi.Unafiki mtupu
 
Wakuu naomba kueleweshwa hii habari ya kwenye Gazeti inaonyesha Mbunge alikuwa shujaa.., Mvua Gamba amepaint picha tofauti sasa ukweli ni upi na uongo ni upi tafadhari Mvua Gamba naomba uweke hii story sawa...

Unampaka matope Mbunge au Hili gazeti linaficha uongo na kujaribu kumsafisha Mbunge...,

Which is Which :(
 
Argue with a fool and end up being a fool...
Hii habari ipo kwa ajiri ya kuwachanganya tu wasomaji humu.
 
Its very rare kwenye post moja kunakuwa na contradictions.., maswali ni mengi.!!

Aliwageuka wananchi wake na ku-side na wawekezaji au hakufanya hivyo..?
Anashikiliwa na polisi au hashikiliwi na polisi..?
Kwenye list ya majina 17 aliyoongezea watu mpaka mia nne na kitu imejaa ndugu zake au haijajaa ndugu zake..?
Na yeye mwenyewe yupo wapi sasa ..!!?

Ukweli ni kwamba ukisoma hii thread maswali yanazidi kuwa mengi kuliko majibu.., kwa faida ya watakaosoma hii kesho na keshokutwa alietoa post ange-tweak kidogo post yake ili isiwe na hizi contradictions...
 
Hivil lile tatizo la kutumia jina la mtu lishaisha? Kweli geugeu, watatumaliza, daktari kigeugeu
 
Sasa mnashangaa nini kwa wawekezaji kushambuliana na wanakijiji wakati tumesema saaaana kuhusu uwekezaji usio na tija kwa taifa? sasa wananchi wameona wanadhulumiwa ardhi yao ndio maana wameamua kutokubali kuibiwa kila kitu, na bado mengi tutashuhudia kadiri siku ziendavyo. Hivi ni nitu ambavyo serikali yetu itarajie kuvipata kwa kasi ya ajabu kama wao vile vile wanavyouza ardhi kwa wageni kwa kasi zaidi na hali zaidi. Kazeni buti watanzania msikubali kunywang'anywa tena, walivyochukua vinawatosha sasa kilichobaki ni mali yetu.
Tusipoinua vichwa juu tutachelewa sana wananchi watapoteza maisha na mali zao
.
 
Its very rare kwenye post moja kunakuwa na contradictions.., maswali ni mengi.!!

Aliwageuka wananchi wake na ku-side na wawekezaji au hakufanya hivyo..?
Anashikiliwa na polisi au hashikiliwi na polisi..?
Kwenye list ya majina 17 aliyoongezea watu mpaka mia nne na kitu imejaa ndugu zake au haijajaa ndugu zake..?
Na yeye mwenyewe yupo wapi sasa ..!!?

Ukweli ni kwamba ukisoma hii thread maswali yanazidi kuwa mengi kuliko majibu.., kwa faida ya watakaosoma hii kesho na keshokutwa alietoa post ange-tweak kidogo post yake ili isiwe na hizi contradictions...
Well said and great advice, hebu fikiri and may be to reason a little, its known that we lack the art of good listening, kwa kuwa badala ya kumsikiliza mtu, sisi huwa tunajiandaa kuongea, ungeweza kufikiri labda katika hilo la kuongea na ku-present tunalimudu matokeo yake ndiyo hayo muwasilishaji anazidi kutupeleka mbali na ukweli na mwisho anakuwa amefanikiwa kujigeuza kuwa mpiga filimbi Hemelin...
 
Mhe. Dk Kigwangalla sikujua kama ulikuwa huwajui polisi hasa ukiingia anga zao na wakiwa wametumwa na mabosi wao, ona sasa unavyolalamika kama mtoto.

"Nimeshangazwa na polisi hasa OCD, kunibambikia makosa ambayo hayana ukweli na kunidhalilisha kwa kunipiga vibao kama mtoto mdogo na dhihaka mbalimbali kwa wananchi wangu ambao walikuwa wakidai haki yao ya msingi. Hii si haki, sikutendewa haki katika hili ni uonevu mtupu!''alilalamika Dk Kigwangalla.

Nafikiri kuanzia sasa utakuwa na heshima na Chadema, kwani kwao hii imekuwa ni zaidi yako, haha ahaha wamekuchapa vibao lol...kweli polisi kiboko.

.......................................
Mwandishi wetu, Nzega
MBUNGE wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla, amekamatwa na kuswekwa rumande kisha kufikishwa mahakamani jana kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

Habari zimeeleza kuwa mbunge huyo alikamatwa juzi jioni na kuwekwa mahabusu ya polisi katika Kituo cha Nzega ambako alilala hadi jana asubuhi alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Nzega kujibu tuhuma hizo.

Alikamatwa pamoja na watu wengine watatu, Mrisho Hamisi, Mathew Dotto na Mwanja Mwandu, wote wakiwa wakazi wa kata ya Nata ambao ni wachimbaji wadogo, waliodaiwa kushiriki vurugu zilizotokea juzi katika kijiji cha Mwabangu.

Wakisomewa mashtaka yao jana mbele ya hakimu Ajali Mlanzi waendesha mashtaka wa polisi, Merito Ukingoji na Joseph Mbwana, walisema kwa pamoja watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali Oktoba 23 mwaka huu, katika mgodi mdogo wa wachimbaji wadogo uliopo kijijini hapo.

Waendesha mashtaka hao waliieleza mahakama kuwa mbali na kufanya mkusanyiko usiokuwa wa halali, watuhumiwa hao pia, waliingia katika mgodi huo mdogo unaomilikiwa na wawekezaji bila idhini ya wamiliki na kuvamia Kituo cha Polisi cha Nzega.

Waendesha mashitaka hao, walisema washtakiwa hao pia wanatuhumiwa kufanya njama katika ofisi ya wilaya ya CCM na kufanya maandamano kisha kuvamia kituo cha polisi.

Dk Kigwangalla na Mwandu pia wanakabiliwa na shitaka la kupiga na kujeruhi. Waendesha mashtaka hao waliwataja waliopigwa katika tukio hilo kuwa ni Moses Kichambi na Ferdinald Yusuph.

Hata hivyo watuhumiwa wote wanne walikana shtaka na wako nje kwa dhamana baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa bado unahitaji muda kuendelea na upepelezi wa tukio hilo.

Mbali na hakimu Mlanzi kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 18 mwaka huu, amemzuia mbunge huyo kufika katika eneo la mgodi huo ili kuondoa uwekezakano wa kutokea kwa machafuko mapya.

"Mahakama inatambua kuwa ni wewe (Kigwangalla) ni mbunge wa jimbo na unapaswa kutembelea wananchi wako lakini kwa sababu suala hilo sasa liko mahakamani, hutakiwi kufika kwenye eneo la mgodi huo," alisema hakimu Mlanzi.

Adai rumande imemdhalilisha

Dk Kigwangalla aliliambia gazeti hili nje ya mahakama kuwa hakujua kama angehusishwa kwenye kesi hiyo na kuswekwa rumande kwani alifika kituoni hapo kwa nia ya kuwadhamini wenzake.

Dk Kigwangalla alisema kuwa baada ya kuwatuliza wananchi ambao walikuwa wakielekea kwenye Kituo cha Polisi Nzega Mjini, aliwaweka kchini katika ofisi ya CCM wilaya na kuwataka wamsubiri aende kuwawekea dhamana wenzake waliokamatwa.

"Tulipokuwa tunaelekea kituoni, askari wakawa wanazungumza kwa jazba na kusema mimi ndiye niliyeanzisha vurugu na nilipofika kituoni ghafla nikaambiwa nivue viatu na kuelezwa nitalala rumande," alisema Dk Kigwangalla.

"Leo (jana) wamenitoa rumande na kunipeleka mahakamani nikiwa nimefungwa pingu na watu wengine niliokuwa nimeenda kuwadhamini," alisema Dk Kigwangalla.

"Nilikataa kutoa maelezo nilipokuwa kituoni lakini (leo) jana nilipelekwa Mahakamani na kufunguliwa mashtaka kama nane hivi, moja likiwa kujeruhi na mengine ya jinai," alisema Dk Kigwangalla.

Dk Kigwangalla alilalamika "Nimedhalilishwa sana na hawa polisi kwa kuninyima hata nafasi ya kupiga simu kwa mtu yeyote kabla sijawekwa rumande."

....................................................................
 
Nadhani siku nyingine akisikia wanasiasa na hasa wabunge wenzake wa upinzani wakilalamika kuhusu jinsi polisi wanavyowadhalilisha atakuwa na mtazamo tofauti sana na ule aliokuwa nao kabla. Yeye kupigwa kibao tu analalamika vipi kuhusu Profesa Lipumba ambaye alivunjwa/kuteguliwa mkono na polisi au Maalimu Seif Sharif na wenzake waliopigwa na kuwekwa ndani wakituhumiwa kuwa wahaini dhini ya serikali ambayo haipo?
 
Kigwangala wasamehe bure polisi walidhani ni mkutano wa Chadema....
Weigh before you take side.
 
Zambi ya kubambikiza kesi ni kama kula nyama za watu ukishaanza ni lazma utaendelea huwezi kuacha na wakiisha wa kuwabambikiza unjikuta unajibabambikizia mwenyewe.
 
Pole sana mh Kigwangala,unavuta shuka wakati kumepambazuka! hao ndio police ambao wananchi wanawalalamikia kila cku kuwa wananyanyasa raia na kuwabambikia kesi nakuwapiga na nyinyi watunga sheria mnapuuza,sasa leo unapigwa kibao unalalamika, wenzio wanapigwa na marungu na kuporwa mali zao,ama kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu.
 
Mhe. Dk Kigwangalla sikujua kama ulikuwa huwajui polisi hasa ukiingia anga zao na wakiwa wametumwa na mabosi wao, ona sasa unavyolalamika kama mtoto.

"Nimeshangazwa na polisi hasa OCD, kunibambikia makosa ambayo hayana ukweli na kunidhalilisha kwa kunipiga vibao kama mtoto mdogo na dhihaka mbalimbali kwa wananchi wangu ambao walikuwa wakidai haki yao ya msingi. Hii si haki, sikutendewa haki katika hili ni uonevu mtupu!''alilalamika Dk Kigwangalla.

Nafikiri kuanzia sasa utakuwa na heshima na Chadema, kwani kwao hii imekuwa ni zaidi yako, haha ahaha wamekuchapa vibao lol...kweli polisi kiboko.

.......................................
Mwandishi wetu, Nzega
MBUNGE wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla, amekamatwa na kuswekwa rumande kisha kufikishwa mahakamani jana kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

Habari zimeeleza kuwa mbunge huyo alikamatwa juzi jioni na kuwekwa mahabusu ya polisi katika Kituo cha Nzega ambako alilala hadi jana asubuhi alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Nzega kujibu tuhuma hizo.

Alikamatwa pamoja na watu wengine watatu, Mrisho Hamisi, Mathew Dotto na Mwanja Mwandu, wote wakiwa wakazi wa kata ya Nata ambao ni wachimbaji wadogo, waliodaiwa kushiriki vurugu zilizotokea juzi katika kijiji cha Mwabangu.

Wakisomewa mashtaka yao jana mbele ya hakimu Ajali Mlanzi waendesha mashtaka wa polisi, Merito Ukingoji na Joseph Mbwana, walisema kwa pamoja watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali Oktoba 23 mwaka huu, katika mgodi mdogo wa wachimbaji wadogo uliopo kijijini hapo.

Waendesha mashtaka hao waliieleza mahakama kuwa mbali na kufanya mkusanyiko usiokuwa wa halali, watuhumiwa hao pia, waliingia katika mgodi huo mdogo unaomilikiwa na wawekezaji bila idhini ya wamiliki na kuvamia Kituo cha Polisi cha Nzega.

Waendesha mashitaka hao, walisema washtakiwa hao pia wanatuhumiwa kufanya njama katika ofisi ya wilaya ya CCM na kufanya maandamano kisha kuvamia kituo cha polisi.

Dk Kigwangalla na Mwandu pia wanakabiliwa na shitaka la kupiga na kujeruhi. Waendesha mashtaka hao waliwataja waliopigwa katika tukio hilo kuwa ni Moses Kichambi na Ferdinald Yusuph.

Hata hivyo watuhumiwa wote wanne walikana shtaka na wako nje kwa dhamana baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa bado unahitaji muda kuendelea na upepelezi wa tukio hilo.

Mbali na hakimu Mlanzi kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 18 mwaka huu, amemzuia mbunge huyo kufika katika eneo la mgodi huo ili kuondoa uwekezakano wa kutokea kwa machafuko mapya.

"Mahakama inatambua kuwa ni wewe (Kigwangalla) ni mbunge wa jimbo na unapaswa kutembelea wananchi wako lakini kwa sababu suala hilo sasa liko mahakamani, hutakiwi kufika kwenye eneo la mgodi huo," alisema hakimu Mlanzi.

Adai rumande imemdhalilisha

Dk Kigwangalla aliliambia gazeti hili nje ya mahakama kuwa hakujua kama angehusishwa kwenye kesi hiyo na kuswekwa rumande kwani alifika kituoni hapo kwa nia ya kuwadhamini wenzake.

Dk Kigwangalla alisema kuwa baada ya kuwatuliza wananchi ambao walikuwa wakielekea kwenye Kituo cha Polisi Nzega Mjini, aliwaweka kchini katika ofisi ya CCM wilaya na kuwataka wamsubiri aende kuwawekea dhamana wenzake waliokamatwa.

"Tulipokuwa tunaelekea kituoni, askari wakawa wanazungumza kwa jazba na kusema mimi ndiye niliyeanzisha vurugu na nilipofika kituoni ghafla nikaambiwa nivue viatu na kuelezwa nitalala rumande," alisema Dk Kigwangalla.

"Leo (jana) wamenitoa rumande na kunipeleka mahakamani nikiwa nimefungwa pingu na watu wengine niliokuwa nimeenda kuwadhamini," alisema Dk Kigwangalla.

"Nilikataa kutoa maelezo nilipokuwa kituoni lakini (leo) jana nilipelekwa Mahakamani na kufunguliwa mashtaka kama nane hivi, moja likiwa kujeruhi na mengine ya jinai," alisema Dk Kigwangalla.

Dk Kigwangalla alilalamika "Nimedhalilishwa sana na hawa polisi kwa kuninyima hata nafasi ya kupiga simu kwa mtu yeyote kabla sijawekwa rumande."

"Nimeshangazwa na polisi hasa OCD, kunibambikia makosa ambayo hayana ukweli na kunidhalilisha kwa kunipiga vibao kama mtoto mdogo na dhihaka mbalimbali kwa wananchi wangu ambao walikuwa wakidai haki yao ya msingi. Hii si haki, sikutendewa haki katika hili ni uonevu mtupu!''alilalamika Dk Kigwangalla.
....................................................................
nimekumbuka semi ya siku nyingi " MKUKI NI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU'' sijui wahenga walimaanisha nini
 
Back
Top Bottom