Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
umeambiwa kapigwa kwa kuwatetea wachimbaji wadogo wewe unasema alikuwa anatetea wawekezaji? au hujui kusoma. Nenda gumbaru kajifunze a e i o u kwamnza.
anataka kutoka kwa staili ya hovyo hovyo
Kuna thread ilianzishwa ilikuwa ikielezea yaliyojiri jana Nzega lakini huyo mbunge alipondwa sana kuwa ni ndumilakuwili na ndiyo maana alipibondwa! Halafu hebu cheki hiiSidhani!...HATUJAFIKIA HUKO!
Kuna jambo hapa linafichwa!
riz mwekezajiwana jf nipo nzega nikitoka mwanza katika ziara ya ndg ridhwani kikwete.
Usikuu huu nikiwa napata chakula nikasikia risasi zinalia mjini nikaamua kufatilia na kupata taarifa kuwa kuna mgodi ambao unaitwa isunga ngwanda ambao siku mbili zilizopita mbunge na wananchi waliungana kuufunga.
Leo kilicholeta vurugu ni pale mbunge wa nzega alipoenda kuwafata wananchi alioshirikiana nao kuufunga mgodi na kuwataka kuufungua mgodi na yeye akijiunga na polisi kuwataka wananchi wale waondoke wamuachie muwekazaji.
Wananchi walipandwa na hasira na kumvamia mbunge na kuanza kumpiga na kuvunja gari ya daktari wa wilaya ambayo aliazima naambiwa akiwa nzega huazima gari ya daktari wa wilaya na kuitumia.
Wananchi hao wenye hasira waliamua kumpiga mbunge kwa kitendo chake cha kuwasaliti wananchi hao na leo kuungana na polisi na wawekezaji.polisi ilibidi kutumia silaha za moto kumuokoa na na kuwakamata baadhi ya watu na kuwepeleka polisi jambo lilifanya wananchi kuandamana kwenda kuvamia kituo cha polisi na matokeo yake polisi kutumia risasi kuwatawanya wananchi wao.
Liliwaudhi wananchi nitukio la mbunge kigwangala kuwageuka wananchi na kujiunga na wawekezaji na polisi hivi sasa kunavurugu nzega mjini na maeneo ya isunga ktk mgodi huo.
Director huyo asikudanganye sisi tunamjua,LIJIDAI ETI ATAWATETEA WATU WA HAPO ISUNGANGWANDA kwenye kampeini fulani!!!!!!!!! Lakini hakufanya hivyo, hiyo ya Isungangwanda ni msg tosha kwa maghamba!!!!!!!! Wakiendelea kunyanayasa wananchi kama walivyofanya Dodoma watu watachukia na itakuwa ndio basi tena!!!!!!!mkuu jana ulisema wewe ni mwalimu huko mwanza,umeamua kutembea na huyo rizone?mwenzio mtoto wa mjini huyo
Kingwangalla ni kigeugeu mwanzo mwisho. Kwa muda amekuwa anawasema CHADEMA kuwa wanataka nchi isitaliwake, kisa? kwa sababu wanafanya maandamano. Sasa week kala matapishi yake na kuandamana na wananchi kufunga mgodi. True to himself, siku mbili baadae anajitokeza na msimamo tofauti na aliokuwa nao wakati akifunga huo mgodi na wananchi!
Rewinding the tape, ni huyu huyu Kingwangalla aliyejiapiza huko nyuma kuwa angewahamasisha wananchi ili wafunge mgodi wa Resolute, lakini Kingwangalla being Kingwangalla akavamia ka-mgodi kadogo kabisa na sio Resolute. Kama kuna machafuko huko Nzega Kingwangalla atakuwa right in the middle of it kwa sababu ya kung'ata na kupiliza. Leo anasema hiki kesha anafanya the opposite. Kiongozi gani asiyesimamia anachosema?
Huyu bwana angeendeleza ujuzi wake wa kujitingaza jinsi alivyo 'msomi', lakini kwa muda huu mfupi amabapo amekuwa kwenye public eye anaonekana kuwa very immature in his thinking.
Wana Jf nipo nzega nikitoka Mwanza katika ziara ya Ndg ridhwani kikwete.
Usikuu huu nikiwa napata chakula nikasikia Risasi zinalia Mjini nikaamua kufatilia na kupata taarifa kuwa Kuna Mgodi ambao unaitwa Isunga Ngwanda ambao siku Mbili zilizopita Mbunge na Wananchi waliungana Kuufunga.
Leo Kilicholeta Vurugu ni Pale Mbunge wa Nzega alipoenda kuwafata wananchi alioshirikiana nao kuufunga Mgodi na kuwataka kuufungua mgodi na yeye akijiunga na Polisi.
Hii habari haijakaa sawa, lazima kuna spinning ya kitoto hapa. Hao wawekezeji wako wangapi? Kuna uwekezekano Kingwangalla 'alikopa' watu toka eneo tofauti waje wapambane na wenjeji hapo ili ionekane wawekezaji wanapambana na mbunge?
soma tanzania daima!!!!!!!!!kuna watu wawili wameripoti tukio hili mpaka sasa kupitia JF. Wote wako nzega lakni maelezo yao tofaut kabisa. Sasa tumwamini nani
Halafu hata hivyo ina maana kutokana na habari yenyewe wawekezaji nao walikuwa wanarusha mawe? Na kwa muonekano wa story yenyewe Kigwangwallah akawa kama mtu kati. Halafu hata hiyo gari inayotajwa mbona tofauti na iliyoelezewa awali? Mwanzoni ilionekana kama Range Rover lakini hapo inaongelewa gari ndogo Toyota Caldina.
HTML:Ndugu zangu wanaJF, Tusiichezee nguvu ya wananchi hata siku moja, kwa usalama wa Taifa letu. Toka juzi nimekuwa nikifanya jitihada mbalimbali za kutuliza munkari ya wananchi wa kijiji cha Mwabangu. Watu wakichoka ni hatari sana. Mimi sijawaangukia Resolute na wala siwezi kuwaangukia hata siku moja. Wananzega wanachotaka ni maendeleo na haki yao ya kulipwa fidia kwa mali yao iliyohodhiwa na ama kuvunjwa miaka 15 iliyopita, wananzega hawataki mbunge mwehu anayeambiwa sasa tutawajengeeni shule kadhaa, maabara kadhaa, tutawawekeeni lami, tutawalipeni fidia zenu n.k na mbunge huyo akakataa akang'ang'ania maandamano tu! Tulichokifanya sisi ni kukubali kwenda mezani na kuanza mazungumzo na mpaka sasa tupo katika hatua mbalimbali, tukishindana tutaingia Barabarani mpaka mgodini. Nyie subirini tu na mtaona!
HTML:Ndugu zangu wanaJF, Tusiichezee nguvu ya wananchi hata siku moja, kwa usalama wa Taifa letu. Toka juzi nimekuwa nikifanya jitihada mbalimbali za kutuliza munkari ya wananchi wa kijiji cha Mwabangu. Watu wakichoka ni hatari sana. Mimi sijawaangukia Resolute na wala siwezi kuwaangukia hata siku moja. Wananzega wanachotaka ni maendeleo na haki yao ya kulipwa fidia kwa mali yao iliyohodhiwa na ama kuvunjwa miaka 15 iliyopita, wananzega hawataki mbunge mwehu anayeambiwa sasa tutawajengeeni shule kadhaa, maabara kadhaa, tutawawekeeni lami, tutawalipeni fidia zenu n.k na mbunge huyo akakataa akang'ang'ania maandamano tu! Tulichokifanya sisi ni kukubali kwenda mezani na kuanza mazungumzo na mpaka sasa tupo katika hatua mbalimbali, tukishindana tutaingia Barabarani mpaka mgodini. Nyie subirini tu na mtaona!
Mbona unachanganya habari Mkuu, Ndasa ipo Kahama, na iliypo Nzega ni Ngasa.keli hata mi niko nzega niliskia risasi wakati napata mlo hapa ndasa. Nilijua wazee wa kazi wemevamia mahali....hapa hapa ndasa wakati ffu wamepaki risasi ilifyatukia hewani kidogo tutoke nduki.....ova